Wanajamii tumekua tukijadili mambo mengi Jukwaani , mingi ya mijadala husika inagusa masuala ya kusiasa! Binafc naumizwa sana kusikia ajali za barabarani kila kukicha! Ukweli ukiona majeruhi, maiti zitokanazo na ajali zinatisha, majeruhi wanatisha!
Wakati watu wanapoteza maisha kila iitwapo leo, wanasiasa wametuweka busy kujadili siasa tu!
Ni ombi langu leo kuomba Wanajamvi, tujadili nini kifanyike kupunguza ama kuondoa kabisa tatizo la ajali, mjadala wetu uzingatie wadau wote wanaohusika na usafiri wa barabarani tu; Sumatra, Traffic pamoja na abiria! Nini kifanyike ili kuondoa tatizo hili?
Ni imani yangu ajali hizi zinaepukika kila mdau akiwajibika kwa nafasi yake! Karibu!
Ajali za barabarani husababishwa na vitu vikuu vitatu:
1.Barabara 2.Vyombo ya usafiri 3.Watu
1. Barabara zinaweza kupunguza ajali kama zitakuwa zinatengenezwa mara zinapoanza kuharibika(pot holes) na sio kuachwa hadi kugeuka mahandaki. Alama za barabarani ziwepo kila mahali penye risk na hizi alama ziwekwe hata kwenye barabara za vumbi ili kuwafahamisha watumiaji hali ya barabara huko mbele ikiwa ni pamoja na speed wanayopendekeza wataalamu kufuatana na profile ya barabara, milima, kona, miteremko, madaraja, upepo mkali, utelezi, maporomoko nk. Sasa hivi ukitoka Mbezi Mwisho kuelekea Mbezi Beach kupitia Goba barabara ina kona nyingi sana na matuta ila hutakutana na alama yoyote ya barabarani tangu mwanzo hadi mwisho kitu ambacho ni hatari kwa watumiaji wote wa barabara.
2. Wengi wetu hatuna uwezo wa kununua magari mapya(0-mileage) hivyo tunanunua magari yaliyotumika nchi zingine na yanapoingizwa nchini hatujui kama huko lilikotoka liliwahi kupinduka (overturn) au la. Mimi sio mtaalamu ila nasikia gari likipinduka kwenye baadhi ya nchi haliruhusiwi tena kurudi barabarani kwa sababu aerodynamics za gari hiyo zinabadilika na kulifanya lisiwe stable barabarani tena. Gari kama hilo linaishia kutolewa spares tu. Tuache hayo. Ni wajibu wa kila mtumiaji kuhakikisha chombo chake chausafiri kiko salama kila siku kabla ya kukiingiza barabarani kama mtumiaji anathamini maisha yake na ya watumiaji wengine wa barabara. Je wangapi kweli huwa tunakagua vyombo vyetu vya usafiri kila siku kabla ya kuingia barabarani? Walau hata level ya coolant, brake fluid, power-steering fluid level tu? Sijui! Ila pia mamlaka husika za usalama barabarani huwa zina taratibu ya kukagua hali ya usalama wa vyombo vya usafiri wa barabarani (Vehicle road-worthy) angalao mara moja kwa mwaka kwa magari yenye umri wa zaidi ya miaka 3 tangu litoke kiwandani. Kwa nchi yetu naona ni tofauti kabisa. Mamlaka inayohusika na usalama barabarani inauza STICKERs za kuonyesha kuwa gari lako limekaguliwa na linafaa kuwepo barbarani bila kuhatarisha usalama wa wengine!! Kwa wenzetu Road-worthness inakaguliwa na Agencies/makampuni/magereji makubwa yenye viwango vilivyokubalika na kukuarifu mmiliki hali ya usalama wa gari lako, na vitu gani unatakiwa urekebishe/ubadili ili kukuhakikishia usalama wako na wa watumiaji wengine wa barabara. Ni hiari yako kutengenezea hapo hapo au kupeleka gari lako kutengenezea chini ya mwembe mradi uimalize checklist waliyokupatia ya vitu vya kurekebisha/kubadili then unarudi tena kwao kwa verification. Wakiridhika wanakupa barua unakwenda traffic kupewa STICKER ya usalama barabarani. Sasa hapa kwetu Tz sijui wenzangu kama magari yenu yana funuliwa hata hiyo bonet? Mimi sijawahi kukaguliwa pamoja na kuhitaji kukaguliwa gari! Madereva wa malori wa safari ndefu nasikia ndio kabisa hata akimwambia tajiri yake gari lina ubovu anaweza kuambiwa arudishe funguo kama hataki kazi. Kwa hali hii naona kwa upande wa vyombo vya usafiri risk ya ajali ni kubwa sana kwa ajili yaUZEMBE!
3. Watu tunachangia pia katika ajali. Unakuta mtu kanunua gari bila hata kwenda driving school. Then anamtafuta dreva wa kumfundha kwenye "Off-roads" siku nne, then tayari wiki inayofuata yuko peke yake anaendesha kuelekea kwenye shughuli zake! Driving Licence wanajua wanakozipata ila nasikia sio issue. Na watu kama hawa wapo wengi tu. Group lingine ni "incompetent drivers" wanaofundishwa chini ya viwango kutoka kwenye utitiri wa driving schools zilizopo. Kuna driving schools zenye "MAADILI" na kuna zingine wanatengeneza fedha tu. Mke wangu bahati mbaya alisomea kwenye hizo zinazotengeneza fedha tu. Basi alipomaliza akarudi nyumbani na leseni yake "halali" kabisa(zile za zamani kama kakitabu). Sasa nilipoanza kumuuliza vipi vehicle inspector kwenye road test amekupa marks gani na maelezo/maoni gani, ndipo nilipotaka kuzimia! Ananishangaa "vehicle inpector? Road-test? Marks? Ndio vitu gani hivyo?" Duh, anasema wao siku wanaanza masomo ya udereva walipeleka picha na siku ya mwishi wa vipindi waliletewa leseni darasani kila mtu bila hata mtihani wa aina yoyote ile! Anyway nilimwambia wife twende lunch Mlimani City tukitokea Kibaha na aendeshe yeye na tulipofika Kibamba aliegesha gari kwa "hasira" za kukosolewa na mimi na madereva wengine waliokuwa wanatupita kwa jinsi alivyokuwa anayumba njia nzima. Ila nashukuru Mungu alikubali kuwa hiyo kozi ya udereva aliyopitia ni ya kitapeli kabisa, na kukubali kuanza upya tena kozi ya udereva katka chuo cha shirika la elimu kibaha. Baada ya kumaliza hapo waliambiwa watakwenda kufaya mtihani wa road-test na nadharia Kituo cha Oysterbay kwa sababu kibaha walikuwa hawajaanza kutoa leseni mpya zinazotumika sasa. Waliambiwa licence mpya hazina forgeries wala upendeleo na "Competence " yako ndio itapelekea upate leseni. Walikwenda wakiwa sita na walipofika tu askari mmoja wa traffic akawauliza kama wana shida na leseni wakamjibu ndio. Basi akawaambia wajichangishe elfu ishirini kila mtu then mmoja wao akampelekea. Kilichofuata: hawakuulizwa hata walikosomea udereva wala kutakiwa kuonyesha udhibitisho wa kusomea udereva, walijaziwa makaratasi na kutumwa kwendaTRA kumwona mtu "Fulani" na kulipia benki then akaja na driving licence!!!! Nilijichokea tu!!! Huu ni mfano hai watu tunavyosababisha ajali kwa uzembe halafu tunaziita ajali!!
Kuna swala la Kilevi kwenye kusababisha ajali, nadhani wote tunalielewa na wadau mbalimbali wanajaribu kuzishauri mamlaka husika jinsi ya kutatua tatizo hili japo sioni bidii ya mamlaka husika kwenye hili zaidi kushupalia spidi kwa kamera na kujificha kwenye vichaka kuwaotea madereva walio kwenye speed. Swala la Ulevi uwe wa pombe, madawa nk ni swala la kuvalia njuga kwani kwa sasa hivi nasikia hata baadhi ya madereva wa masafa marefu hawapumziki njiani inavyoshauriwa na ni watumiaji wa vilevi wakiwa barabarani; sasa ukichanganya na uchovu wa hizo safari ndefu jibu unalo.
BODABODA: Huu ni ukiwa mwingine mkubwa tu. Nimeishi Douala Cameroon 2007, kule ni bodaboda na taxi tu hakuna daladala. Bodaboda ni nyingi ila ajali i nadra mno!! Kwanini? Douala dreva wa bodaboda na dreva wa gari wanasomea sheria za barabarani sawa na lazima wapate leseni kwa kufanya mtihani wa nadharia na road-test. Sasa hapa kwetu naona kidogo ni tofauti. Wanafundishana usiku na asubuhi yuko kituo cha basi anasubiri abiria ili hali haelewi hata alama moja ya barabarani! Kabla ya pikipiki kuanza kutumika kama taxi Tumbi ilikuwa inapokea ajali 2.1 kwa siku, baada ya bodaboda kuanza kutumika kama taxi ajali tumbi ziliongezeka na kufikia 4.9 kwa siku. Nadhani hii inatupa picha kamili ya mchango wa bodaboda kwenye ongezeko la ajali za barabarani. Pamoja na kutokujua sheria za barabarani bado speed zao ni za hatari nasikia vilevile wachache wao huanza kunywa viroba tangu asubuhi kwa hiyo wanaendesha wakiwa wamekunywa(DUI). Baada ya takwimu za Tumbi, shirika la elimu kibaha walianzisha kozi maalumu ya waendesha bodaboda ili kujaribu kupunguza ajali zinazosababishwa nao na athari zake.
Neno la mwisho: Unapomwambia bodaboda awashe taa mchana anapoingia barabarani ili aongeze "VISIBILTY" yake kwa magari yeye anakujibu kwa kejeli kuwa hawezi kuwasha taa kwasababu hajabeba maiti!! Inasikitisha :-(