Wanabodi
Hakuna kinacho nikera kama mwendelezo wa ajali za Mabasi/Magari ambazo zinachinja watu kila siku. Sioni mkakati wa maana uliopo kwa Wizara ya mambo ya ndani /Polisi/na vyombo vya kuratibu Usafiri.
Mhe. Mwigulu kapwaya kabisaa......... na Kamanda Mpinga hana jipya tena.
Natambua swala la ajali barabarani ni Multifactorial, lakini polisi, vyombo vya usafiri vilitakiwa vije na mkakati wa dharura , wa kati na wa muda mrefu kupunguza hii hali.
Kwa nini tuendeelee kufa kama vifaranga? Hivi mnajua ajali hizi zinauwa watu wengi kuliko hata kipindupindu na hata wagonjwa wanaokufa hospitali za Muhimbili? Ni muda sasa wa uhai wa Mtanzania uthaminiwe hata kama ni mmoja tu.
Nchi zingine hata mtu mmoja akifa huwa ni issue…….sisi hapa tunaona kawaida tu
No, ni vizuri tushauri Serikali.. Mhe, Mwigulu kashindwa….. hana kipaumbele, Kamanda Mpinga Kachoka, watu wengine waje…..type kama za akina Mwaibula, Mhe Kangi Lugola n.k
Jamani, tuamuke, hili swala la ajali ni janga kubwa, ingawa wengine hamulioni. Tutaisha, tutaisha… bila mkakati makini. Ukipanda bus/gari ,,lazima moyo ukudunde kama utafika salama.
Kweli tuendelee kufa hivi? Rushwa nayo mpaka lini barabarani?Ukipata ajali au akifa ndugu yako ndo hasa mtaelewa ninachokisema