Ajali Tanzania: Mawazo mbadala kuhusu udhibiti wa ajali Tanzania

Ajali Tanzania: Mawazo mbadala kuhusu udhibiti wa ajali Tanzania

Namba tano ni ngumu sana, assume wewe ni mmiliki wa gari na umempata dereva makini ukamkabidhi gari yako...soon akapata ajari na akafariki yeye na baadhi ya abiria, wanausalama wakaja sema kosa ni la dereva, na wakati huohuo gari yako imeisha kabisa huna matumaini ya kuirudisha uzimani, je utakubali kulipa faini?.

Mwisho jana nimeona ajari ya gari ya Noah ikiwa inatokea Mto wa Mbu kwenda karatu (Mkoa wa ARUSHA), kilomita chache kabla ya kufika Karatu mjini ile Noah ikapata ajari. Maswali yamekuwa mengi kupita maelezo maana kwa nyuma yake ni kituo wasimamapo maafisa usalama, mahali ambapo gari imepata ajari ni sehemu nzuri tu kwa usalama,

Isipokuwa kuna watengeneza barabara wamemwaga kokoto na walikuwa bado hawajaweka kibao kuonyesha kazi ikiendelea........na pia nae dereva pale inasemekana alipita asubuhi route ya kwanza na ile ilikuwa route ya pili na alipaona. Sasa watu wamekosa majibu kwamba yule bwana alikuwa mwendo kasi sana, je traffic walihongwa pale nyuma?,

Eneo la ajali imekuaje dereva amepata ajari pale maana gari ilihamia upande wa pili ndiko lilikoangukia. Hapohapo upande wa juu ndiko nyumbani kwao huyo dereva.......na huyo dereva hiyo ni gari yake ameinunua mda mfupi toka ajichangechange kutoka ktk biashara ya bodaboda na kuuza shamba. Dereva hawajampata hadi leo na majeruhi wapo hospital, waliofariki ni RIP tu.

Sasa hiyo faini hata wakimdai atalipa ataitoa wapi? maana ule ni uzembe wa dereva na uzembe wa trafiki aliyepangiwa kile kituo ile siku husika
Uzalendo kwanza mambo mengne badae, maiti nayo hulaumiwa
 
Binadam sjui tumeumbwaje

Wakati unasimama umwambie dereva apunguze mwendo

Yupo anaesema dereva tumwage dereva tuwahishe

Gari ikienda slow wenyewe tunaanza dereva mwendo gani ongeza speed tunachelewa ajali ikitokea dereva ndio wa kwanza kulaumiwa[emoji26][emoji26][emoji26][emoji26]
Kwahy ikitokea ajali tuslalamike tuwe wapole maana cc wenyewe tunapenda iwe hvyo
 
Hii picha haisemi kila kitu, inategemea na hali, wakati mwingine inawezekana dereva huyo wa lorry aliona mbele kuko vizuri akawaruhusu wapite, na wa kwanza alivyopita akawaita na wenzake.
 
Hii picha haisemi kila kitu, inategemea na hali, wakati mwingine inawezekana dereva huyo wa lorry aliona mbele kuko vizuri akawaruhusu wapite, na wa kwanza alivyopita akawaita na wenzake.

Hakuna kitu kama hicho. Angalia mistari iliyochorwa hapo barabarani. Hapo hata kama mbele kweupe haruhusiwi kuovateki
 
Shida kubwa kazi ya udereva imechukuliwa kama kazi ya mwisho sana, mimi sioni tofauti ya dr na dereva wote wanadeal na roho za watu. Inatakiwa tubadilishe fikira za madereva watambue dhamana wanayokuwa nayo safarini.
 
Hata hawajui hizo double line barabarani zina maana gani?
 
Na wewe mtamamchungu inaoneka wewe hata sheria za barabarani hujui! Hiyo picha ya pili yenye mabasi 2 huyo mwenye lori unavyomuona hapo anaona kinachoweza kutokea kwenye kona? Kwanza hilo lori hata kwenye kona halijafika. Huyo fala wa basi anaovertake!
 
Halafu pia haruhusiwi kuovateki kwa kumfuata mwenzako. Kwavile unakuwa huoni mbele. Hapo na abiria wanachekelea tu.
 
Mipando kama hiyo inatakiwa iongezewe extra lane kwa ajili ya slow moving vehicles kama malori nk.
 
Hakuna kitu kama hicho. Angalia mistari iliyochorwa hapo barabarani. Hapo hata kama mbele kweupe haruhusiwi kuovateki
Ndio maana nikasema hii picha haisemi kila kitu. Hayo maeneo ya Iyovi na Kitonga kuna sehemu chache sana ambazo ni safe ku-overtake, haya maeneo yanataka timing, ndio maana muda mwingine madereva wanategemea kuongozwa na madereva wenzao. Sasa wewe bishana lakini hio ndio ukweli. Period
 
Na wewe mtamamchungu inaoneka wewe hata sheria za barabarani hujui! Hiyo picha ya pili yenye mabasi 2 huyo mwenye lori unavyomuona hapo anaona kinachoweza kutokea kwenye kona? Kwanza hilo lori hata kwenye kona halijafika. Huyo fala wa basi anaovertake!

Kuna sheria na kuna uhalisia, ndio maana nikasema hiyo picha haisemi kila kitu. Hayo maeneo sehemu za ku-overtake ni chache sana, wakati mwingine madereva huwa wanasaidiana. Inawezekana mwenye lorry ndio kawaambia wapite. Hivi ndio watu wanaendesha magari.
 
Ndio maana nikasema hii picha haisemi kila kitu. Hayo maeneo ya Iyovi na Kitonga kuna sehemu chache sana ambazo ni safe ku-overtake, haya maeneo yanataka timing, ndio maana muda mwingine madereva wanategemea kuongozwa na madereva wenzao. Sasa wewe bishana lakini hio ndio ukweli. Period

Kenye sheria za usalama barabarani hakuna kitu kinaitwa taiming.
Mambo ya taiming hakuna
 
Kuna sheria na kuna uhalisia, ndio maana nikasema hiyo picha haisemi kila kitu. Hayo maeneo sehemu za ku-overtake ni chache sana, wakati mwingine madereva huwa wanasaidiana. Inawezekana mwenye lorry ndio kawaambia wapite. Hivi ndio watu wanaendesha magari.

Kwahiyo mwenye lori kuwaambia wavunje sheria nao wakakubali.
 
Mkuu umesomeka vizuri, naona hapo Nganga aliamua kujificha nyuma ya lori,angalau hakufanya upuuzi huu walioufanya Sai Baba, Abood na Ilasi zote za Tunduma hizo. Iyovi ni sehemu ya hatari tupu lkn jamaa wanalala na kona zile wakipiga overtake za kufa mtu! kimsingi madereva wetu chanzo kikubwa sana cha ajali kwa careless driving yao,followed by ubovu wa barabara na magari yenyewe!
Pia hapo huwezi kuona mita mia ili umruhusu wa nyuma apite, na kwenye kona hairuhusiwi kuovertake,tatizo madereva wetu wengi uendesha kimazoea na hawataki gari iwe mbele yao hata ajali nyingi sababu kubwa ni mazoea
 
Kaendeshe kwanza kwenda mkoani halafu utaona maana ya nilichokwambia. Ni abiria wachache sana ambao huwa wanajua nini kinaendelea barabarani
 
Kaendeshe kwanza kwenda mkoani halafu utaona maana ya nilichokwambia. Ni abiria wachache sana ambao huwa wanajua nini kinaendelea barabarani
wacha umaandazi aisee...unatetea ujinga waziwazi, eti timing...ndio mdudu gani huyu katika sheria za barabarani..
 
Back
Top Bottom