Ajali Tanzania: Mawazo mbadala kuhusu udhibiti wa ajali Tanzania

Ajali Tanzania: Mawazo mbadala kuhusu udhibiti wa ajali Tanzania

Heshima kwenu Wakuu,

Hakika nimefurahishwa na hii mbunu mpya jeshi letu la Polisi ambayo wanaitumia.

Polisi katika kuwaelimisha Madereva, wameamua kuwafuata huko huko barabarani. Wamefunga Spika kubwa kwenye magari ya Patrol na kufungulia muziki mkubwa wenye kuelimisha.

Mkiwa kwenye foleni kwa upande wa Dar, Utasiki tangazo likihamasisha Usalama barabarani na kisha unawekwa ule muziki pendwa wa Walevi na Madereva.

Naomba mwinye kuujua huu wimbo atuwekee hapa.

Wimbo wenyewe unaimbwa hivi
"Dereva kalewa pombe sawa hiyo??...hata hiyo si sawa Dereva acha Vituko". Dereva kalewa pombe sawa hiyo??..mwanadada mwenye sauti nzuri anajibu..haataaa...hiyo si sawa Dereva acha vituko. Mia
Ha haaa nimekumbuka mbali sana
 
Habarini wakuu!

Hili janga linazidi kuongezeka kila uchao, na sababu kubwa inayotolea na vyombo vya dola ni mwendo kasi, najiuliza swali, je Tanzania peke yake ndio magari yanakimbia sana, au ni wanaojiita madereva ndio wasiokuwa makini? Mbona kuna nchi magari yanakimbia mpaka over 100 na ni nadra kusikia ajali?
My take; (1)kitengo cha usalama barabarani wanatakiwa kuchunguza vizuri hili swala, kwani kuna watu wengi wanaendesha magari kwa kujua kuyaendesha tu lakini sio madereva,
(2) kitengo cha usalama barabarani kisiwe chanzo cha kukusanya mapato ya serikali, hili nalo linachangia ongezeko la vihiyo maana wanajua lolote likitokea atalipa faini. Tunapoteza ndugu zetu kila uchao.
(3) kitengo cha usalama barabarani kukusanya mapato mengi ni dhahiri kwamba barabarani hakuna usalama wa kutosha.
Kama una sababu nyingine za kuongezea ongeza hapo.
 
Dareva anaua kwa mwendokasi halafu anafunguliwa kesi ya kuua bila kukusudia( traffic case) ..... Madereva waanze kunyongwa uone kama hizi ajari haziwi history
 
Dareva anaua kwa mwendokasi halafu anafunguliwa kesi ya kuua bila kukusudia( traffic case) ..... Madereva waanze kunyongwa uone kama hizi ajari haziwi history

Ziwekwe sheria kali barabarani ndio njia pekee ya kuzuia ajali, lakini kugeuza makosa ya barabarani ni chanzo cha mapato ya serikali, hili sio sahihi ajali hazitaisha.
 
Wanabodi
Hakuna kinacho nikera kama mwendelezo wa ajali za Mabasi/Magari ambazo zinachinja watu kila siku. Sioni mkakati wa maana uliopo kwa Wizara ya mambo ya ndani /Polisi/na vyombo vya kuratibu Usafiri.
Mhe. Mwigulu kapwaya kabisaa......... na Kamanda Mpinga hana jipya tena.
Natambua swala la ajali barabarani ni Multifactorial, lakini polisi, vyombo vya usafiri vilitakiwa vije na mkakati wa dharura , wa kati na wa muda mrefu kupunguza hii hali.
Kwa nini tuendeelee kufa kama vifaranga? Hivi mnajua ajali hizi zinauwa watu wengi kuliko hata kipindupindu na hata wagonjwa wanaokufa hospitali za Muhimbili? Ni muda sasa wa uhai wa Mtanzania uthaminiwe hata kama ni mmoja tu.

Nchi zingine hata mtu mmoja akifa huwa ni issue…….sisi hapa tunaona kawaida tu
No, ni vizuri tushauri Serikali.. Mhe, Mwigulu kashindwa….. hana kipaumbele, Kamanda Mpinga Kachoka, watu wengine waje…..type kama za akina Mwaibula, Mhe Kangi Lugola n.k

Jamani, tuamuke, hili swala la ajali ni janga kubwa, ingawa wengine hamulioni. Tutaisha, tutaisha… bila mkakati makini. Ukipanda bus/gari ,,lazima moyo ukudunde kama utafika salama.

Kweli tuendelee kufa hivi? Rushwa nayo mpaka lini barabarani?Ukipata ajali au akifa ndugu yako ndo hasa mtaelewa ninachokisema
 
KWANI WAO NI MADEREVA?KWA NCH ZETU HIZI KILA KITU KIDOGO UNAONDOA WATU HATUWEZI KUFIKA.WEWE SEMA UMEKUWA HUWAPENDI HAWA WAHESHIMIWA
 
na rais amesema matuta Yaondolewe barabarani,kama tukiendelea kulaumu waziri wa mambo ya ndani na matrafiki hatutofika na tutakufa wote kwanini tusibadilike na kujiongoza wenyewe?,hadi hili la usalama wa vyombo vyetu wenyewe nalo tuseme serikali jamani?
 
Ndugu
Swala la ajali ni mulyifactorial, Drivers wana matatizo yao, lakini kama policy za nchi zimekaa vyema na zinasimamiwa, ajali zinapungua sana. Elewa bila mikakati na usimamizi makini, hali hii itaendelea na hata wewe huenda kuna siku utayaona machungu. Driver hawa hawa wakiendesha magari nchi zingine wanakuwa tofauti na wanatia adabu kwa sbb viongozi wao wanasimamamia ipasavyo na mikakati ipo. Sasa hawa waheshimiwa , unaona nini kipya,?hakuna creativeness na supervision
 
Ajali zote za barabarani husababishwa na makosa ya kibinadamu kwa asilimia 99.9,Asilimia 0.9 pekee ndio tunaweza kumsingizia muumba.Usalama barabarani unaanzia kwenye ujenzi wa miundombinu ya barabara kwa kuzingatia hali ya hewa,tabia nchi,upana wa barabara lengwa,unene wa kifusi au lami inayotakiwa kuwekwa katika eneo husika n.k. Haya yote hupangwa na binadamu kabla magari hayajaanza kuitumia barabara hiyo. Wizara ya miundombinu na polisi trafiki wanakuja kusimamia na kudhibiti mienendo na tabia za waendesha vyombo vya moto,pamoja na watembea kwa miguu ambao kwa namna yoyote ile wanalazimika kupita katika hizi barabara sambamba na magari. Kwa kuangalia picha hiyo kubwa tunagundua kuwa ili kupunguza ajali hapa Tanzania au hata kuzikomesha, inabidi elimu ielekezwe kwa madereva kwa kiwango kikubwa na kwa kila dereva anayeingiza chombo cha moto barabarani awe amepitia mafunzo na mazoezi kiasi cha kujiridhisha kuwa ni mahiri kweli na aendelee kudhibitiwa kwa karibu sana kwa maana ya kuwa akifanya makosa mfano matatu anyang'anywe leseni kabisa. Inatakiwa itumike dhana ya ''Ni vigumu sana kupata leseni ya kuendesha gari na ni rahisi sana kunyang'anywa leseni daima". Kama kutakuwa na ugumu wa kuingiza gari barabarani na udhibiti ukawepo pamoja na adhabu kali kwa wakosaji na hasa kunyang'anywa leseni,faini au kifungo,hizi ajali zitapungua tu. Hebu angalia hii video jinsi huyu dereva alivyojisababishia ajali kwa mpango wake mbovu wa kulipita gari kubwa TIR .Hii inaonyesha wazi jinsi alivyokosa uzoefu pamoja na kuwa na elimu ya kuendesha gari au hata kuwa na leseni.
 
Attachments

Ajali zitapungua kwa mambo kadha moja madereva wote wakisoma bila rushwa ktkt vyuo vya udereva, teknolojia ya touch kufungwa kwenye kona na mitelemko mikali, wasimamizi wa sheria (askari) watakapo kataa rushwa, serikali itakapojenga barabara pana, kuondoa Magari chakavu, makazi ya watu kuwa mbali na barabara, kuwadhibiti wamiliki wa mabasi wakati wa kuajiri Dereva n.k
 
Ungewaza kidogo tu ungeona kwamba waziri Mwigulu na kamanda Mpinga sio watu wa kuwaweka list ya kushindwa kufanya majukumu yao ila zaidi naona una hoja mbovu na chuki dhidi ya watu hawa.

Ajali katika nchi hii kwa mtazamo mpana ni matokeo ya ujinga wetu watanzania kuanzia dereva mpaka abiria plus ujenzi wa barabara usiokidhi viwango. Zaidi ya hayo pia matumizi ya mabasi kwa umbali mkubwa wa kufikia 1500km ambao basi hupaswa litembee kwa siku ili kesho lirudi tena katika barabara za kiwango cha chini zenye mitaro na vihatarishi kila kona ni sababu nyingine.
nchi za wenye akili tungeweka kipaumbele katika usafiri wa tren na mabasi yasafirishe watu kwa safari fupi tu hasa mkoa hadi mkoa.

Hio akili ya kuchukia watu wa maeneo flani koma!
 
Wanabodi
Hakuna kinacho nikera kama mwendelezo wa ajali za Mabasi/Magari ambazo zinachinja watu kila siku. Sioni mkakati wa maana uliopo kwa Wizara ya mambo ya ndani /Polisi/na vyombo vya kuratibu Usafiri.
Mhe. Mwigulu kapwaya kabisaa......... na Kamanda Mpinga hana jipya tena.
Natambua swala la ajali barabarani ni Multifactorial, lakini polisi, vyombo vya usafiri vilitakiwa vije na mkakati wa dharura , wa kati na wa muda mrefu kupunguza hii hali.
Kwa nini tuendeelee kufa kama vifaranga? Hivi mnajua ajali hizi zinauwa watu wengi kuliko hata kipindupindu na hata wagonjwa wanaokufa hospitali za Muhimbili? Ni muda sasa wa uhai wa Mtanzania uthaminiwe hata kama ni mmoja tu.

Nchi zingine hata mtu mmoja akifa huwa ni issue…….sisi hapa tunaona kawaida tu
No, ni vizuri tushauri Serikali.. Mhe, Mwigulu kashindwa….. hana kipaumbele, Kamanda Mpinga Kachoka, watu wengine waje…..type kama za akina Mwaibula, Mhe Kangi Lugola n.k

Jamani, tuamuke, hili swala la ajali ni janga kubwa, ingawa wengine hamulioni. Tutaisha, tutaisha… bila mkakati makini. Ukipanda bus/gari ,,lazima moyo ukudunde kama utafika salama.

Kweli tuendelee kufa hivi? Rushwa nayo mpaka lini barabarani?Ukipata ajali au akifa ndugu yako ndo hasa mtaelewa ninachokisema
Ninaiman nao sana Nchemba pamoja na Mpinga madereva ndio shida
 
Kwahy tatzo hili limeshndkana au naanza mie :
1.Abiria unapopanda gari hakikisha unachunga mzgo wako ulioingia nao achia mbali ulioungiza kwenye sehm y mzgo.

2.kagua tiket ako, funga mkanda muombe mola kadr huezavyo.

3.safari imeanza ukiona dereva amelewa, yuko mwendokas simama Anza kumwambia kondakta aspomwambia dereva mwambie ww nadhan ukiendelea kuongea lazma Kuna watu watakusuport.

4.Ussubir mpate ajali upo hospital unaanza kulalamka et dereva alikuwa amelewa /mwendokas haitasaidia ushaarbu ningejua iz to rate.

5.Watu wa usalama barabaran gari likipata ajali kw uzembe wa dereva kampun huska piga fain kubwa ili iwe fundsho Kwa wengne.

6.Usalama barabaran mskubali kuingizwa mkenge naiman mmenielewa.
7.Tukifuata utaratibu huu nadhan tutapunguza ajali kama Co kumalza kabisa.

NI HAYO TU. muleba mchana mwema na safar njema mlioko safarin mfike Salam.
 
Binadam sjui tumeumbwaje

Wakati unasimama umwambie dereva apunguze mwendo

Yupo anaesema dereva tumwage dereva tuwahishe

Gari ikienda slow wenyewe tunaanza dereva mwendo gani ongeza speed tunachelewa ajali ikitokea dereva ndio wa kwanza kulaumiwa[emoji26][emoji26][emoji26][emoji26]
 
Namba tano ni ngumu sana, assume wewe ni mmiliki wa gari na umempata dereva makini ukamkabidhi gari yako...soon akapata ajari na akafariki yeye na baadhi ya abiria, wanausalama wakaja sema kosa ni la dereva, na wakati huohuo gari yako imeisha kabisa huna matumaini ya kuirudisha uzimani, je utakubali kulipa faini?.

Mwisho jana nimeona ajari ya gari ya Noah ikiwa inatokea Mto wa Mbu kwenda karatu (Mkoa wa ARUSHA), kilomita chache kabla ya kufika Karatu mjini ile Noah ikapata ajari. Maswali yamekuwa mengi kupita maelezo maana kwa nyuma yake ni kituo wasimamapo maafisa usalama, mahali ambapo gari imepata ajari ni sehemu nzuri tu kwa usalama,

Isipokuwa kuna watengeneza barabara wamemwaga kokoto na walikuwa bado hawajaweka kibao kuonyesha kazi ikiendelea........na pia nae dereva pale inasemekana alipita asubuhi route ya kwanza na ile ilikuwa route ya pili na alipaona. Sasa watu wamekosa majibu kwamba yule bwana alikuwa mwendo kasi sana, je traffic walihongwa pale nyuma?,

Eneo la ajali imekuaje dereva amepata ajari pale maana gari ilihamia upande wa pili ndiko lilikoangukia. Hapohapo upande wa juu ndiko nyumbani kwao huyo dereva.......na huyo dereva hiyo ni gari yake ameinunua mda mfupi toka ajichangechange kutoka ktk biashara ya bodaboda na kuuza shamba. Dereva hawajampata hadi leo na majeruhi wapo hospital, waliofariki ni RIP tu.

Sasa hiyo faini hata wakimdai atalipa ataitoa wapi? maana ule ni uzembe wa dereva na uzembe wa trafiki aliyepangiwa kile kituo ile siku husika
 
Back
Top Bottom