Habari enyi wapendwa!
"Uchungu wa msiba usikie kwa jirani tu"
Kabla ya yote natanguliza pole kwa ndugu na jamaa wote wenye simanzi na majonzi ndani ya mioyo yao kutokana na misiba mbalimbali iliyowahi kuwakumba, Yaliyopita yamepita lakini hapa naomba sasa tujadili ili kuepuka kama si kupunguza misiba hii kabisa.
Ni rahisi sana kwa mtu Mtanzania asiyejali akutapo msiba au ajali Apite pembeni pasipo hata kuuliza msiba upoje. (Hakuna msiba usiofunza jambo)
Watanzania tubadilike, tusikimbilie kuandika koment nyingi zenye neno PUMZIKA KWA AMANI NA R.I.P na hoja za mapenzi kwa wingi, Twaweza jadili kwa wingi pia usalama wetu na ni namna gani ajali hizi tutaziepuka AHSANTE!
…ACCIDENTS ARE AVOIDABLE WHEN THE SITUATION IS ALARMING…
TAFAKARI (yawezekana kabisa Mtu aliyebuni kuwepo kwa SAFETY BELT, Alipata wazo hilo baada ya kuona ajali na akagundua Umhimu wa kufunga mkanda" wiki iliyopita niliandika makala hii;
UJINGA WETU TANZANIA NA AJALI HIZI ZA KIZEMBE, TUJIPANGE KUZITOKOMEZA
Kutokana na aina ya wasomaji, nililazimika kuandika makala hii kwa ufupi sana kama ifuatavyo;kwanza pitia maana ya maneno haya kabla;
AJALI ni tukio lolote la ghafla linalotekea na kuumiza vitu au watu;
HATARI/HAZARD ni ile hali ya kwamba kuna tukio au ajali itatokea.
KIWANGO CHA HATARI/RISK ni ule uwezekano uwe mkubwa au mdogo wa kwamba kuna tukio la hatari litatokea.
HATARI YA KITU AU JAMBO/DANGEROUS ni ile hali ya kitu au jambo kusababisha /kuleta maumivu au ajali.
Ebu pitia mifano hii;
1. Wanakijiji wa MBONDORE wanaishi karibu na ghala la mabomu yaliyo isha mda wake . (wanakiji wa mbondore wapo kwenye RISK) (Mabomu kuisha mda wake ni DANGEROUS) (Mabomu yakilipuka ni AJALI itayoleta HAZARD kwa wananchi).
2. Roli bovu lililo simama Msituni pembezoni mwa barabara bila tahadhari, Limegongwa na bus kwakuwa dreva wa roli aliliwa na Simba punde kabla ajali. (Gari bovu ni DANGEROUS, Kusimama Msituni ni RISKY, roli kupaki na Bus kuendeshwa bilaTahadhari ni HAZARD,Dreva wa roli kuliwa na simba na Bus kugonga roli ni AJALI.
AJALI NYINGI TANZANIA NI ZA KIZEMBE ASILIMIA 98%
Naomba kuanza kwa kusema waafrika wengi hasa watanzania tuko bize sana kushughulika na ajali na si vyanzo vyake, TUJAFANYA KAMA ZIMA MOTO TU Hatujishugulishi kutatua tatizo kabla ya ajali hata kama tupo katika hali ya hatari, mara nyingi ajali inapotokea Hujifariji kwa kauli “AJALI HAINA KINGA” hii kauli mimi huwa naiona waliyo ibuni walikuwa wazembe kabisa na Huwa siipendi kabisa na wanangu nawafundisha kuichukia kauli hiyo kwa nguvu zote, Kwakuwa karibu ajali zote 98% huwa zina chanzo chake, kwanini tusijikite kuwa makini na vyanzo vinavyoleta ajali?
Mfano wa ajali zilizo tokea majuzi morogoro na Singida:
AJALI za juzi; Bila kuwa na chembe ya kumumunya maneno; zile ajali zote zinathibitisha uzembe wa hali ya juu kabisa kuanzia kwa MADREVA, TRAFFIKI NA ABIRIA; Ajali zile zimetoa taswira na kuthibitisha tu uzembe wa nyuma.
SERIKALI INAMAKUSUDI GANI?
Kwakweli naomba mamlaka husika zichue hatua za kudumu kunusuru haya matatizo, Nashauri wasitegemee TOCHI za bararani pekee, Yamkini Tochi zikawa chanzo cha ajali zinapotumiwa kama mradi, wakumbuke madreva wanapeana taarifa kwahiyo pale panapostahili hutembea zaidi, na kufanya tochi kuwa kama matuta ya barabarani yalivyo, Wafikilie Kuweka control ya kudumu, yaweza ikawa kwenye mafunzo ya udereva, mikataba ya ajira,uchakavu wa magari na rushwa kwa askari wetu.
NINI KIFANYIKE?
Kuna mambo mengi sana, lakini yanahitaji wataalamu wakae na kujadili, twaweza weka hata sheria za kulazimisha GPS Monitoring kwa mabasi yote Au wanaweza boresha kukawa na mfumo wa log book Bus transportation-Yaani kila kituo kuwepo mda maalum wa kufika kwa kila basi, sheria kali ziwekwe kwa dreva yeyote atakaye kamatwa na kosa la ulevi au kuvunja sheria n.k
Hivi mtu anaendesha gari hana leseni, kalewa na anatembea speed kubwa hadi dash bod inapitisha jeneza, Sasa hapo ajali ikitokea tuseme HAINA KINGA? MABASI yanatembea speed kubwa kwenye barabara mbovu halafu tunasema AJALI HAINA KINGA? Hivi kweli kabisa kabisa haina kinga? Mi nakataa kabisa kauli za kizembe kama hizi na ningekuwa na mamlaka ningeifuta kauli hii kwenye orodha ya Kiswahili.
MAPENDEKEZO
Usafili wa Tanzania kwakweli siyo wa uhakika kabisa kwa asilimia kubwa, Ni vyema japo bunge walau mara moja moja likajadili mambo haya, Matokeo ya ajali tanzania ni makubwa sana ukilinganisha na inchi za wenzetu walivyo.
Watu wengi tumeishauli serikali namna ya kupunguza ajali barabarani, labda huenda wengine ujumbe hawakuupata kutokana na changamoto mbalimbali- naomba serikali iandae warsha hata ya kiushindani, Mtu au Taasisi itakayo andaa PROJECT itakayo onekana nzuri kunusuru AJALI za barabarani mwenye project apewe MOTISHA kama si pesa basi hata Ile project ipewe jina lake tu wakati serikali inapoitekeleza itaweza kuwa kama Motisha kwao.
VIONGOZI WANAFANYA NINI?
Kuna viongozi wanajisahau kabisa katika hili na kuona kama AJALI haziwahusu;
Lakini ukiangalia Viongozi wengi sana wamekufa katika AJALI mbalimbali za barabarani, lakini naomba waelewe kwamba MWENYE AKILI HUWEZI UKAWA SALAMA KUENDESHA GARI LAKO KWENYE BARABARA MBOVUINAYOTUMIWA PAMOJA NA WAJINGA WENYE LESENI ZA KUGUSHI
karibuni!.