Ajali Tanzania: Mawazo mbadala kuhusu udhibiti wa ajali Tanzania

Ajali Tanzania: Mawazo mbadala kuhusu udhibiti wa ajali Tanzania

11081186_591751634293582_2018160420856435859_n.jpg


:becky::becky::becky:
 

Attachments

  • alshabab.jpg
    alshabab.jpg
    104.8 KB · Views: 427
Mpwa wangu MziziMkavu mimi napingana na hizo picha, hata jana niliandika hapa jukwaani jinsi viroba vilivyosaidia kupunguza ajali.

Njiani/barabarani kuna mambo mengi sana ya ajabu, kama hauko vizuri utapata ajali nyingi sana, Vizuri kwa maana mbili, kwamba kama hukumshika MUNGU wako vyema na vizuri kwa maana ya kwamba uwe na "mtaalamu"

Sasa wengi wetu wanaamini kuwa ni majini/mashetani/makafara yanafanyika, na wapo watu wengi sana wanaamini kuwa POMBE haipatani kabisa na Majini/mapepo/maruhani hayo. Kwahio ilikuaondokana na madubwana hayo yanayoleta ajali njiani these Guys walikua wanatumia Pombe kabla ya kuanza safari na baadae waka-adavance kwakuweka kwenye Chupa as if wanakunywa maji kwahio pepo/majini au kitu kingine kibaya kisingeweza kuwafikia.
In recent days, waliwakataza madereva kunjywa pombe na kukataza kabisa kuweka Chupa za "maji" pale mbele wakati wanaendesha maana iliaminika kuwa ni Pombe.

Kitendo hicho ndio kimewapa majini na mashetani nafasi ya kufanya mambo hayo, kwahio, VIROBA vilisaidia sana kupunguza ajali na baada ya kukatazwa ndio rate ya ajali imeongezeka. Huo ni mtazamo kutoka upande wa pili, sio lazima wote tuwe na mtazamo mmoja. karibu Lunch
 
Last edited by a moderator:
Kwako Kamanda Mpinga,

Juzi katika ufunguzi wa wiki ya nenda kwa usalama umeongelea mambo mengi yenye manufaa kwa jamii ya Watanzania wa leo.
Pamoja na yote nina swali moja linalonisumbua sana akilini. Hivi ni kweli kuwa speed gun ndiyo muarobaini wa ajali za Tanzania?
Kwa maelezo mafupi ili tusipate jibu la mkato hapa mimi ninaona kuwa Traffic police sasa akili yote ni speed guns tu. Kwa nini? Kwa vile kuna hela ya harakaharaka, kataa kubali hiyo ndiyo hali halisi. Ukaguzi wa magari ni pale wanapojisikia. Na ukaguzi ni sticker za bima, road licence, mapato, SUMATRA, na ya kwao ya usalama. Ukiwa na hivyo traffic wetu ameridhika kabisa.
Chanzo kikubwa cha ajali siyo over speeding, ni ubovu wa magari, barabara na madereva. Katika hali ka hii ajali hata kama kwa speed ndogo tu, bado zitatokea. Kumbuka enzi zile barabara zetu hazina lami, basi kutoka Mwanza kwenda Musoma ilikuwa ni zaidi ya saa kumi ukilinganisha na tatu za sasa. Jee wakati huo wa speed ya Leyland na Bedford hakukuwepo na ajali? Hapo speed si tatizo hasa la ajali zetu. Traffic Police fanyeni kazi yenu na si kukusanya mapato ya serikali kama core subject yenu!
Barabara zetu, nyingi sasa hivi zina lami lakini kwa sehemu kubwa zina mawimbi, mashimo na hata utelezi achilia mbali kona na maingiliano ya ghafla. Barabara za wenzetu, tena wenye kututengenrzea magari haya haziko hivyo. Wanatengeneza gari nadhani yenye maimum speed ndogo ni 120 kph. Sisi barabara zetu tunasema maximum speed 80 kph tena nafhani kwa kuibia ili tufiche yale madhambi tuliyoyafanya wakati wa ujenzi. Huko si lengo la topic hii. Hapa ina maana kuwa barabara zetu zinachangia kwa kiasi kikubwa ajali za Tanzania.
Kwa habari ya madereva, kwa kweli kuna watu wanaendesha magari kwa sababu ni yao, maana hakuna mtu mwingine yeyote anayeweza kumpa gari kwa ubovu.wa udereva wao. Tukubali tukatae, utoaji wa leseni za udereva ni holela sana. Kuna jamaa yangu aliniambia ilimchulua miaka zaidi ya mitatu kupata leseni ya kuendesha taxi huko London Uingereza. Sisi tuna utaratibu gani? Tuwe wakweli tu, huu utaratibu wetu je unatupatia madereva bora au bora madereva?
 
Habarini wadau na heri ya mwaka mpya 2016.
Mimi ni mdau wa hivi vyombo vya usafiri wa umma (i.e mabasi yaendayo mikoani), hivi karibuni pamekuwa na udhibiti wa vyombo hivi kwa sababu ya kupunguza ajali mpaka kupelekea mtu anayetoka Mwanza alfajiri kwa basi kifika Dar saa sita usiku.
Ni kweli kuna haja ya hawa SUMATRA kufanya njia kama hizo lakini njia hizi kwakweli zimekuwa ni za kuumizana tu kwakweli. Maana haiingii akilini, basi linatoka Dar saa 12 asubuhi alafu likaingia Dodoma saa tisa. Hivi huku ni kupunguza ajali au kutaka kurudisha maendeleo nyuma maana muda unaopotea ni mwingi njiani pasipo sababu za msingi. Japo wahenga walisema " Haraka haina baraka" na "Polepole ndio mwendo" ila kwa upolepole huu ni kutaka kunufaishana pasipo kuwa na tija.
Yan haingii akilini kuwa, basi linalotoka Dar asubuhi na mapema lifike Singida saa mbili kasoro!!. Au basi linalotoka Singida alfajiri lifike Dar saa tatu usiku.
Sidhani kama hii sera imekaa vizuri, embu tujaribu kuliona hili swala kwa uzuri zaidi maana inakuwa ni kurudishana nyuma kimaendeleo.
Basi likitembea kwa wastani wa 80km/h mbona haliwezi sababisha ajali na litatumia muda vizuri tu lakini sio kama ilivyo sasa.
Ni hayo tu.
 
Umesikika mkuu, ila siku utakayoamkia hospitali umezungushiwa mipira ya msosi usoni bila shaka utarudi hapa na bandiko lililokaa swsw.
 
Mkuu iyo ni halali kudhibiti ili kupunguza ajali.na matokeo yake msimu huu Wa sikukuu hakuna ajali
 
Siku utakapojikuta upo MOI huku miguu yote ikiwa imefungwa antenna....ndio utajua maana HARAKA HARAKA HAINA BARAKA
 
Kwani kwa sasa speed iliyowekwa ni ngapi......?.....na kama kuna mahali unawahi......si unaondoka mapema zaidi........?......mi naona ili tuweze kuheshimiana na ziraili......twende speed 50-60 kph........Bora tufike bana.......
 
Sasahv mi naona ndio imekuwa kero, yaani Dar to Morogoro masaa manne (4)…!!!
 
Unafanya utani kwenye mchezo mkuu? We endelea kusikia tu kwenye vyombo vya habari kua ajali imetokea usiombe yakufike.
 
Juz kuna basi limewamwaga jamaa kwene midomo ya mamba pale ruaha.hukusikia?
 
1454345015929.jpg

Tunahitaji mjadala wa kitaifa katika hili kila mmoja wetu na kwa umoja wetu liwe ni jukumu letu sote.

JamiiForums ilete msukumo chanya kwenye hili. Nchi inapoteza nguvu kazi wataalam na wazazi wa kesho.

Makaburi yanaongezeka kila uchao, yatima, wajane na wategemezi wanazidi kuongezeka! Ndoto nyingi zinazimika...mapato ya nchi yanazidi kutumika kununulia madawa na vifaa tiba.

Walemavu wanaongezeka! Taifa lina rudi nyuma nchi inahujumiwa na mamlaka zake yenyewe. Kitengo cha polisi wa barabarani kinatakiwa mabadiliko makubwa sana hasa idara ya leseni, zinatolewa kama njugu pesa ndio inaongea.

Shule za udereva: Je zina wakufunzi wanaokidhi vigezo? Je wanafundisha umuhimu wa kukilinda na kukitunza chombo kisilete madhara kwa mtumiaji na wengine? Je wana elimu ya uchumi?

Wazazi walezi ndugu na jamaa: Wanatimiza wajibu kuhusu usalama barabarani? Je hawashiriki kusaidia kupata leseni kwa njia za mkato na kufahamiana?

Vyombo vya habari: Je jukumu Lao ni kuishia kutangaza kwa mbwembwe matukio ya ajali ? Hawa wana jukumu zito sana.

TRA: Walipa kodi wanazidi kuteketea, pokea pesa ya leseni lakini hakikisha huyo mtu ni mjuzi ili isije ikawa ndio pesa yake ya mwisho kupokea! Unahitaji mapato una jukumu kubwa hapa.

Mitandao ya simu hili pia ni lenu mnahitajika sana kwa kuwa ajali nyingi hutokana na kuongea na simu.

Wazalishaji wauzaji na wamiliki wa mabar na vileo: Mnawahitaji hawa wateja muwaone tena na tena mnahusika moja kwa moja

Makundi mengine katika jamii sijayataja, madaktari wetu tuwapunguzie mzigo wa kutibu majeruhi ili nguvu zielekezwe kwingineko.

Misiba siku hizi ni gharama kubwa familia zinaingia umaskini na kupoteza muda mwingi

Ajali za Tanzania ni mjadala wa kitaifa tuna jukumu kuhakikisha tunafanya kitu kwenye hili
 

Attachments

  • 1454345006067.jpg
    1454345006067.jpg
    19.7 KB · Views: 57
kabisa mkuu. Ajali za vyombo vya moto vinachukua sana maisha ya watu wengi kwa sasa. Hili jambo lipewe mjadala wa kitaifa aisee
 
Hivi kamanda Mpinga yupo humu JF?? Huyu mheshimiwa anatakiwa humu tumuulize maswali. Ana mengi sana ya kutuelimisha,na kufafanua.
 
Back
Top Bottom