Ajali Tanzania: Mawazo mbadala kuhusu udhibiti wa ajali Tanzania

Ajali Tanzania: Mawazo mbadala kuhusu udhibiti wa ajali Tanzania

Breakdowns wanakwambia ndio siku za kazi na hata watu wa bima na magereji pamoja na traffic na vehicle inspectors ndio kipindi cha 'ulaji'
Ajali pia huongezeka kila wiki ya mwisho wa mwezi na kupungua sana katikati ya mwezi
means ajali zipo direct proportion na mshahara
 
Huyo jamaa kasema picha Kali sana ulizotumia, sasa ndo namwambia inaonyesha ni mwoga sana wa hizo picha.
wewe vp? hapa nilikua sijizungumzii mimi, nilikua nazungumzia courtesy ya kawaida ya uwasilishaji wa habari kwa umma ambayo media zote hutumia, na mtoa post kanielewa.
picha za hazitakiwi kuonyeshwa hivyo au kama zinatisha wanatoa tahadhari kwanza, hata movie za kutisha huwa wamezi rate kuwa zinatisha ili mtazamaji ajue na achague kwanza kabla ya kutazama
 
[Sawa E="mshana jr, post: 15233373, member: 98741"]Ulitumia fasihi kali ambayo ni vigumu kuitafsiri kwa haraka[/QUOTE]

Sawa saw a.
 
Tatizo kubwa kwetu sisi mtu anayefuata sheria/utaratibu ni mshamba.

Ilitakiwa adhabu ziwe ngumu pale mtu anapovunja sheria, na zisimamiwe kwa weledi.
 
Nimekuelewa.

wewe vp? hapa nilikua sijizungumzii mimi, nilikua nazungumzia courtesy ya kawaida ya uwasilishaji wa habari kwa umma ambayo media zote hutumia, na mtoa post kanielewa.
picha za hazitakiwi kuonyeshwa hivyo au kama zinatisha wanatoa tahadhari kwanza, hata movie za kutisha huwa wamezi rate kuwa zinatisha ili mtazamaji ajue na achague kwanza kabla ya kutazama
 
mimi naona zile namba za itv wanazotangaza kwenye runinga Sumatra wangafanya zikabandikwa kwenye kila basi sehemu ambayo abiria wataona
maana watu huwa hawazikariri wala kusave ila zitasaidia kumuogopesha dereva apunguze mwendo

Lakini pia nashauri hata namba za simu za wenye mabasi zingebandikwa au kuandikwa kwenye ticket badala ya kuandika namba za simu za mawakala au wasimamizi wa biashara husika wasio wamiliki wa hayo magari, kuna bus linafanya safari zake kati ya Kilombero na Dar linaitwa Kidililo kama sijakosea (mtanisahihisha) mmiliki wa wake ameweka namba zake kwenye ticket na ikitokea una tatizo na wahudumu wa gari lake ukampigia anatoa ushirikiano wa karibu kwa abiria wake, nadhani huo ungekuwa mfano wa kuigwa na wengine wote

Lakini wengine wameweka matangazo yanayopingana kabisa na mambo wanayofanya, kwa wale wanaotumia usafiri huo kwenye picha mtakuwa mashahidi, kuna matangazo kuwa kama bus litazidisha abiria zaidi ya wale walikaa kwenye viti, basi kuna namba wameweka pale mbele zitumike kuwafahamisha watawala wa kampuni husika, kitu cha kushangaza ni pale unaona miongoni mwa hao watawala wanakuja kwa driver na kuchukua kitu mgao wafikapo Chalinze

Madhara ya kuzidisha abiria kwenye ma-bus ni pamoja na:

  • Abiria hao kutokuwa salama itokeapo ajali kwasababu wanakuwa hawana mikanda ya usalama
  • Nauli wanayotoa abiria husika haikatwi kodi (wataalamu wa mambo ya kodi mtanisahihisha) kwa uelewa wangu
  • Abiria wanaozidi kwenye bus wanasababisha uharibifu wa barabara kutokana na kuongezeka kwa uzito wa bus kuwa mkubwa, na ndiyo maana ma-bus mengi hushusha abiria yafikapo Ruvu darajani na kuwapakia kwenye bodaboda ili watangulie wakapandie mbele zaidi ya Kigwaza ambako ndipo ilipo Mizani, na wakati mwingine abiria walioko mbele kabisa husogezwa katikati ya bus hadi bus litakapovuka mizani ndipo abiria hao hurejeshwa kwenye eneo la juu ya injini
  • Rushwa ni moja ya madhara yanayotokana na uzidishwaji wa abiria pia; gari linalozidisha abiria linakuwa ni kichocheo cha rushwa kwa wale ndugu wenye mavazi meupe njiani
Naamin haya niliyochangia hapa wengi wenu mmeyashuhudia yakifanyika humo njiani.

Mapendekezo:

  • Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani awe na kikosi kidogo cha askari wasiokuwa na sare watakaorekodi matukio yote yanayohusiana na uzidishaji wa abiria na kuzifikisha picha au video hizo kwa wamiliki wa magari husika pamoja na vyombo vya sheria ili wahusika wachukuliwe hatua
  • Taasisi inayohusika na mizani pia iwe na timu itakayofuatilia mwenendo wa madereva wanaozidisha abiria na kuwashusha abiria au kuwahamishia nyuma pindi wanapokaribia kwenye mizani, kadhalika video hizo zitumike kama ushahidi mahakamani
  • TRA na Takukuru nao watengeneze kijitimu chao kitakachofanya ufuatiliaji wa hayo yanayofanywa na watoa rushwa na wapokea rushwa
Very sorry picha zimegoma kuinuka
 
mimi naona zile namba za itv wanazotangaza kwenye runinga Sumatra wangafanya zikabandikwa kwenye kila basi sehemu ambayo abiria wataona
maana watu huwa hawazikariri wala kusave ila zitasaidia kumuogopesha dereva apunguze mwendo
 
Madereva wengi hawapo makini!!!!!
Inahitajika mikakati ya dharura na mpango kazi wa muda mfupi wa kati na mrefu kwa kuwashirikisha wataalam na wadau wa sector tofauti bila kuwasahau wananchi
Uzembe wa madereva una vyanzo vingi sana vikiwemo
-stress za kimaisha na kifamilia
-magonjwa wakati mwingine ya akili
-starehe hasa ulevi na ngono
-ulemavu uliofichika hasa wa macho miguu na mikono
-Ubabe ubishi na mashindano
-dharau kiburi na majigambo
-umri na kukosa majukumu
-papara na vurugu za ki maono
-elimu
 
Bingwa hapo umeweka POINTS khaswa !!!
Vizingatiwe:-

Back
Top Bottom