Ajali ya basi la Ester, Rav4 yaua watatu Kilimanjaro

Ajali ya basi la Ester, Rav4 yaua watatu Kilimanjaro

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Watu watatu wamefariki dunia papo hapo baada ya gari aina ya Toyota Rav4 waliokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na basi la abiria la Kampuni ya Ester Kuxury, mkoani Kilimanjaro leo Jumamosi Februari mosi, 2025.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji mkoani Kilimanjaro, Jeremiah Mkomagi amesema ajali hiyo imetokea eneo la Mdawi, Wilaya ya Moshi.

"Ajali imetokea leo asubuhi eneo la Mdawi, watu watatu waliokuwa kwenye gari dogo aina ya Toyota Rav4 wamefariki dunia baada ya gari hilo kugongana uso kwa uso na basi la kampuni ya Ester Luxury lililokuwa likitokea Moshi kwenda Dar es Salaam," amesema Mkomagi.

Amesema chanzo cha ajali ni baada ya dereva wa gari dogo kuyapita magari mengine bila kuchukua tahadhari na kwenda kugongana uso kwa uso na basi hilo.

Hata hivyo, Kamanda Mkomagi amesema hakuna majeruhi kwenye basi hilo, na miili ya marehemu waliokuwa kwenye gari dogo imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro, Mawenzi.

Siku sheria za barabarani zikifatwa hizi ajali zitapungua sana kama sio kuisha
Juzi Kuna IST imetanua ikala njia yote mi na tvs ikabidi tukae pembeni apite ila nikasema "kuwa makini sio Kila siku utakutana na tvs"
Sijui kwann kuna watu huwa hawajui kabisa kuhis hatar,yaan yeye akiamua anafanya tu bila hata tahadhari
 
Sijui kwann kuna watu huwa hawajui kabisa kuhis hatar,yaan yeye akiamua anafanya tu bila hata tahadhari
Miundombinu haikidhi mahitaji mkuu, ni ngumu mno kwa idadi ya vyombo vya moto kupishana kwenye barabara moja na kwa anaekwenda na kurudi na Watembea kwa miguu kwa wakati mmoja, hasa kwa miji yenye pilika pilika nyingi.

Unakuta ni free way ila Watembea kwa miguu wanakatisha🤫
 
Licha la elimu bado miundo mbinu ya barabara ni finyu sana
Yani miundombinu mi naitetea
Maana driver huwa anafundishwa kuendesha gari kwenye mazingira magumu sana kuliko yaliyopo
Ndio maana tunawekewa zile Koni ili usizigonge na ndio maana Kuna u driver wa kujihami n.k
Huko china watu wanaendesha gari mlimani kati kati na wanavuka driver makini ni mara Chache sana atasema miundombinu
78%ya ajali tz ni kosa la driver 12% miundo mbinu na 10% hali ya hewa
 
Miundombinu, elimu duni, uchakavu wa vyombo vya usafiri , nchi zilizoendelea miundo mbinu ya barabara inachangia kiasi kikubwa usalama barabarani na kupunguza kiwango cha ajali
 
Nawaza hivi hao watu kama wangalijua kwamba leo ndio siku yao ya mwisho kuwepo duniani, je, wangetoka? Je, dereva angeendesha gari kama alivyoendesha? Je, angefanya maamuzi aliyofanya ya kuovateki? Je, angeona kwamba kuwahi hicho alichokua anawahi (kama kipo) ni muhimu kuliko maisha yake na ya watu aliowabeba?

Madereva tuweni makini, maisha hayana mbadala.
 
Back
Top Bottom