Ajali ya basi la Ester, Rav4 yaua watatu Kilimanjaro

Ajali ya basi la Ester, Rav4 yaua watatu Kilimanjaro

Ni kweli mkuu ila bado ni mwendo wa kinyoga , huku fedha nyingi zikienda kwenye mambo ambayo sio ya msingi kihivyo, karibu beer 🍺 mkuu😊
mtandao wa km za mraba kwa kiwango cha lami tulizo nazo tukizimwaga pale rwanda hawapati hata eneo la tuta moja la mchicha

tatizo kubwa hata ukimsikiliza kamanda ni udereva wa kutokujihami na kuwapa kipaumbele wengine

BIA INADUMAZA AKILI MEKU 😂
 
mtandao wa km za mraba kwa kiwango cha lami tulizo nazo tukizimwaga pale rwanda hawapati hata eneo la tuta moja la mchicha

tatizo kubwa hata ukimsikiliza kamanda ni udereva wa kutokujihami na kuwapa kipaumbele wengine

BIA INADUMAZA AKILI MEKU 😂
Sijakataa kuwa barabara ipo, je ina kiwango cha kukidhi mahitaji ya vyombo vya moto? Hapa naongelea mult line road haswa kwa mnispaa mbalimbali ili kupunguza misongamano , mbona kwa uchumi wetu tukijifunga mikanda anasa zikapunguzwa tunaweza?

Bia nachangia uchumi mkuu.😁😁
 
Miundombinu haikidhi mahitaji mkuu, ni ngumu mno kwa idadi ya vyombo vya moto kupishana kwenye barabara moja na kwa anaekwenda na kurudi na Watembea kwa miguu kwa wakati mmoja, hasa kwa miji yenye pilika pilika nyingi.

Unakuta ni free way ila Watembea kwa miguu wanakatisha🤫
80% ya ajali zote ni wrong driving[makosa ya binadam],15% ni ajali zinazosababishwa na hali ya hewa mbaya eg mvua,ukungu barabarani,n.k, na 5% ndio zinasababishwa na miundo mbinu,hiyo ni kwa mujivu ya shule fupi ya driving niliyopitia
 
Elimu,watu wengi wamejua kuendesha gari au chombo chochote bila kupata elimu ya u driver hii inawafanya waone Kila kitu sawa TU
Lakini kingine ni ujinga nyuma ya usukani hii inaumiza wengi

Ni kweli.
Mfumo wa leseni haukuwa makini. ?!
Kugongesha na Hela Basi madhara ndio hayo .
 
Dereva anaesababisha ajali kwa uzembe hadi kifo ni Sawa na amemua kujiua mwenyewe.
Msiba wake wengi hawaombolezi kivile maana ni kama wa mtu alojinyonga mwenyewe .
Sasa mtu kaamua kijiua mwenyewe mnamlilia wa nini ?
Sema atawatia ndugu na majirani hekaheka na Hela za nauli na ulezi wa wategemezi wake alowaacha.
 
Miundombinu haikidhi mahitaji mkuu, ni ngumu mno kwa idadi ya vyombo vya moto kupishana kwenye barabara moja na kwa anaekwenda na kurudi na Watembea kwa miguu kwa wakati mmoja, hasa kwa miji yenye pilika pilika nyingi.

Unakuta ni free way ila Watembea kwa miguu wanakatisha🤫
Hii ni kweli
 
Kwa desturi za makabila mengi maziko ya mtu alojiua mwenyewe huwa siyo ya serous sana.
Wengine wanafukia tu hata matanga hawaweki.
Wengi hata misa hawasomi ya shukrani au kumbukumbu ili kuondoa ile roho na mkosi.
 
Leseni hazizingatii elimu ni hela unapata unaingia barabarani unaanza kufukuzana

Inasikitisha mno tena mno .
Kuna nchi ili upate leseni ya udereva ni hadi uwe umehakikiwa kweli kweli sana hatari haikuwa kwake yeye dereva mzembe bali anaweza kusababishia wengine kufa au ulemavu wa kudumu ambao wako innocent.
 
Nimeishuhudia hii ajali leo,nimekuta hata miili haijatolewa!!so sad
Rest in peace
Watu watatu wamefariki dunia papo hapo baada ya gari aina ya Toyota Rav4 waliokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na basi la abiria la Kampuni ya Ester Kuxury, mkoani Kilimanjaro leo Jumamosi Februari mosi, 2025.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji mkoani Kilimanjaro, Jeremiah Mkomagi amesema ajali hiyo imetokea eneo la Mdawi, Wilaya ya Moshi.

"Ajali imetokea leo asubuhi eneo la Mdawi, watu watatu waliokuwa kwenye gari dogo aina ya Toyota Rav4 wamefariki dunia baada ya gari hilo kugongana uso kwa uso na basi la kampuni ya Ester Luxury lililokuwa likitokea Moshi kwenda Dar es Salaam," amesema Mkomagi.

Amesema chanzo cha ajali ni baada ya dereva wa gari dogo kuyapita magari mengine bila kuchukua tahadhari na kwenda kugongana uso kwa uso na basi hilo.

Hata hivyo, Kamanda Mkomagi amesema hakuna majeruhi kwenye basi hilo, na miili ya marehemu waliokuwa kwenye gari dogo imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro, Mawenzi.

 
Sijui kwanini watu wanapenda ku overtake njia zinakopita mabasi na malori, kama huoni mbele kuko kweupe na eneo, ulilopo halina ushirikiano. Bora mwende huo mwendo wa sindikiza harusi, mtafika salama. Sasa walikuwa wakiwahi wapi? Walale Mahala pema.
 
Back
Top Bottom