Dr hyperkid
JF-Expert Member
- Jun 7, 2019
- 12,679
- 25,646
mtandao wa km za mraba kwa kiwango cha lami tulizo nazo tukizimwaga pale rwanda hawapati hata eneo la tuta moja la mchichaNi kweli mkuu ila bado ni mwendo wa kinyoga , huku fedha nyingi zikienda kwenye mambo ambayo sio ya msingi kihivyo, karibu beer 🍺 mkuu😊
Sijakataa kuwa barabara ipo, je ina kiwango cha kukidhi mahitaji ya vyombo vya moto? Hapa naongelea mult line road haswa kwa mnispaa mbalimbali ili kupunguza misongamano , mbona kwa uchumi wetu tukijifunga mikanda anasa zikapunguzwa tunaweza?mtandao wa km za mraba kwa kiwango cha lami tulizo nazo tukizimwaga pale rwanda hawapati hata eneo la tuta moja la mchicha
tatizo kubwa hata ukimsikiliza kamanda ni udereva wa kutokujihami na kuwapa kipaumbele wengine
BIA INADUMAZA AKILI MEKU 😂
80% ya ajali zote ni wrong driving[makosa ya binadam],15% ni ajali zinazosababishwa na hali ya hewa mbaya eg mvua,ukungu barabarani,n.k, na 5% ndio zinasababishwa na miundo mbinu,hiyo ni kwa mujivu ya shule fupi ya driving niliyopitiaMiundombinu haikidhi mahitaji mkuu, ni ngumu mno kwa idadi ya vyombo vya moto kupishana kwenye barabara moja na kwa anaekwenda na kurudi na Watembea kwa miguu kwa wakati mmoja, hasa kwa miji yenye pilika pilika nyingi.
Unakuta ni free way ila Watembea kwa miguu wanakatisha🤫
Huko shule hauwezi funzwa vingine tofauti na serikali inavyotaka.80% ya ajali zote ni wrong driving[makosa ya binadam],15% ni ajali zinazosababishwa na hali ya hewa mbaya eg mvua,ukungu barabarani,n.k, na 5% ndio zinasababishwa na miundo mbinu,hiyo ni kwa mujivu ya shule fupi ya driving niliyopitia
Nyingine zinapigwa hata hazijasajiliwaEKU gari bado mpyaa
Poleni sana aisee
Elimu,watu wengi wamejua kuendesha gari au chombo chochote bila kupata elimu ya u driver hii inawafanya waone Kila kitu sawa TU
Lakini kingine ni ujinga nyuma ya usukani hii inaumiza wengi
Sijui Kwanini jeshi la polisi halisemi ??Waliokuwa kwenye Rav 4 ni akina nani na walutokea wapi?
Huko shule hauwezi funzwa vingine tofauti na serikali inavyotaka.
Hii ni kweliMiundombinu haikidhi mahitaji mkuu, ni ngumu mno kwa idadi ya vyombo vya moto kupishana kwenye barabara moja na kwa anaekwenda na kurudi na Watembea kwa miguu kwa wakati mmoja, hasa kwa miji yenye pilika pilika nyingi.
Unakuta ni free way ila Watembea kwa miguu wanakatisha🤫
Leseni hazizingatii elimu ni hela unapata unaingia barabarani unaanza kufukuzanaNi kweli.
Mfumo wa leseni haukuwa makini. ?!
Kugongesha na Hela Basi madhara ndio hayo .
Leseni hazizingatii elimu ni hela unapata unaingia barabarani unaanza kufukuzana
Watu watatu wamefariki dunia papo hapo baada ya gari aina ya Toyota Rav4 waliokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na basi la abiria la Kampuni ya Ester Kuxury, mkoani Kilimanjaro leo Jumamosi Februari mosi, 2025.
Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji mkoani Kilimanjaro, Jeremiah Mkomagi amesema ajali hiyo imetokea eneo la Mdawi, Wilaya ya Moshi.
"Ajali imetokea leo asubuhi eneo la Mdawi, watu watatu waliokuwa kwenye gari dogo aina ya Toyota Rav4 wamefariki dunia baada ya gari hilo kugongana uso kwa uso na basi la kampuni ya Ester Luxury lililokuwa likitokea Moshi kwenda Dar es Salaam," amesema Mkomagi.
Amesema chanzo cha ajali ni baada ya dereva wa gari dogo kuyapita magari mengine bila kuchukua tahadhari na kwenda kugongana uso kwa uso na basi hilo.
Hata hivyo, Kamanda Mkomagi amesema hakuna majeruhi kwenye basi hilo, na miili ya marehemu waliokuwa kwenye gari dogo imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro, Mawenzi.