Ajali ya basi la Ester, Rav4 yaua watatu Kilimanjaro

Malizia au andika ushauri kwa serikali yetu,,,
Wazipanue barabara za kuingilia manispaa mbalimbali , kutenga sehemu maalum kwa watembea kwa miguu hasa kwenye free way, alama za barabarani ziboreshwe .

Kuwe na Traffic lights kwenye kila makutano ya barabara.

Elimu za sheria za barabarani zitolewe kwa raia na madereva .

Vyombo vibovu vipingwe marufuku hata kunusa pua zao barabarani .

Madereva walevi watengenezewe sheria kali na faini za kutisha.

Boda boda wote wapate mafunzo maalumu ikibidi wapate na vyeti na watumia mihadarati wazibitiwe.

Rushwa zizibitiwe vikali kabisa na abiria watoe ushirikiano kuhusu kuzizibiti ...

Mwisho kabisa abiria wafundishe haki zao wanaponda usafiri wa umma , pia wawe macho kuzibiti uzembe na mwendo kasi wa madereva.
 
Hii familia naifahamu.
Mke aliztaafu na khpata mafao wakaamua wakanunue gari Dar.
wakati wa kurudi wakaamua kukodi dereva awarudishe Arusha, ndio hivyo tena
 
Sijui huwa ni shetani gani huwaingia Mtu anatamani ku overtake tu kwenye mazingira yoyote yale.Upo kwenye Basi wakati mwingine unashangaa Dereva analazimisha ku overtake kwenye mlima na alama za onyo zipo zinazokataza kufanya hivyo,Mtu yupo tayari kubahatisha kubaki hai au kufa.Ubinaadamu kazi.
 
sure
 
Mama mwalimu kapokea pension kamchukuwa kijana wake twende dar tukachukuwe gari
Kufika wakamlipa dereva awapeleke Arusha na chuma mpya, familia imempoteza kijana na mama yake mzazi na dereva waliyemkodi. Inasikitisha sana
Kuna mwenye miaka 65 na 61, yupi hapo ni mama na yupi hapo ni kijana wa huyo mama?

Mwenye miaka 25 alikuwa dereva dereva.
 
Ukiendesha njia kuu utaona hawa wapumbavu wengi sana. Mmoja akiovateki nao wanafuata nyuma kama nyumbu kumbe mwenzao kakadiria gap lake dogo matokeo yake ndio haya.
Wengi wako hivi. Basi akitoa na wao wanatoa. Basi linawaziba field of vision yao kabisa hawaoni mbele kuna nini, wanalifuata tu basi nyuma.
 
Wengi wako hivi. Basi akitoa na wao wanatoa. Basi linawaziba field of vision yao kabisa hawaoni mbele kuna nini, wanalifuata tu basi nyuma.
Upumbavu wanaoendekeza huko mitaani wanaingia nao njia kuu, wacha wanyooshwe tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…