Ajali ya bodaboda jijini Mwanza

Watanzania wengi hupuuza "Left keeping rule" siyo tu wenye vyombo hata watembea kwa mguu, mimi huwa napiga makofi ninao wamudu.

Matokeo ya haraka, mazoea na kupuuza sheria ndo haya. Barabara nyeupe kabisa watu wanagonganaje uso kwa uso wakati ilipaswa wawe side tofauti kabisa.

Shida ya bodaboda akiwa mzima wanafujo sana wenye haraka muda wote dharau na ujuaji ila wakipata ajari sisi waungwana huruma inatuingia na tunaumia vile vile.

Sasa ona wanaacha familia wake na watoto wadogo katika maisha magumu.

Mwenyezi Mungu tupunguzie Vifo utuongezee Vipato.
 
Ina huzunisha na kusikitisha yaan mabasi na MAGARI yanapita...

Tukiwa wadogo Mimi na my young brother huko mwanza tulikua na ng'ombe wa kisasa Kuna wakati wakata nyasi wakiondoka au kuacha kazi na sisi kuchukua baiskeli na kotama (mundu)na kwenda kukatia nyasi

Siku moja nikiwa na mdogo angu tukakata majani kila mtu na baiskeli yake tukapakiza magunia ya majani kila mtu na yake Mimi nikaongoza njia mbele

Mbele kidogo mdogo angu akaelemewa na baiskeli yake akaanguka Kuna kijana walikua wanapita njiani akaomba wamsaidie kunyanyua

Wakamjibu
""WATOA MSAADA SIKU ZOTE NDIO WANAO UMIAGA""

majamaa yakakataa kusaidia yakaendelea na mambo yao.. Nikaweka baiskeli yangu nikaenda kumsaidia dogo...

Hope hao jamaa wa magar wali apply hio falsafa
 
Hivi mtembea kwa miguu barabarani anatumia upande wake wa kulia au kushoto?? Upande upi ni wa hatari kwake kulingana na sheria za barabarani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…