Ajali ya bodaboda jijini Mwanza

Ajali ya bodaboda jijini Mwanza

Yani watu baada ya kushirikiana kwenye mchanga wanalia lia kama mbuzi wanasubiri miujiza
 
Kuzaliwa tz ni michosho sana

Watu hawajui hata kukabiliana na emergency,mwanzo nilidhani ni vijijini huko, sasa hapo misungwi ajali imetokea barabarani magari yamejaa wanazima moto na mchanga na maji kweli?

Fire extinguisher kwenye magari ni kuajili ya kuonyesha traffic officers? Mbona magari yapo nilitegemea Kuona mtu anakuja na fire extinguisher
Nimeshangaa sana pia
 
Kuzaliwa tz ni michosho sana

Watu hawajui hata kukabiliana na emergency,mwanzo nilidhani ni vijijini huko, sasa hapo misungwi ajali imetokea barabarani magari yamejaa wanazima moto na mchanga na maji kweli?

Fire extinguisher kwenye magari ni kuajili ya kuonyesha traffic officers? Mbona magari yapo nilitegemea Kuona mtu anakuja na fire extinguisher
Zile huwa,zisha expire mda sana,na ajabu zaidi dereva wengi hawajui kuzitumia
 
Hao waliosimama na makoti yao ni wapumbavu hata kama ni maiti sio busara kuacha inaungua, fikiria mtu bado anahema wanashindwa hata kutumia nguo kuzima moto .

Hao vijana ni wapumbavu kabisa.
 
Hivi watz sisi aliyeturoga nani? Unapata wapi ujasiri wa kumrecord mwenzio akiwa katika hali hiyo pasina kutoa msaada wowote? Qqqwqmae zenu wote mliorekodi hiyo video.
Ni huzuni ila aliyerekodi kama ni mmoja asamehewe na tujikite kwenye tulichokiona watu wote wale wanaishia kulia lia na kushangaa?
 
Upendo umepoa sana. Mtu anawaka moto huku anaona na hapati msaada zaidi ya kurikodiwa ili apostiwe.
 
Tatizo la ajira limefanya Hadi graduate wawe boda boda!!

Kuna hazina ya ajira milion Moja nchini lakini hawataki kuajiri eti wanasema ajira hamna wakati uhitaji upo!!

Hasta limit ya kulipa mishahara iliyowekwa na shirika la kazi Duniani hatujaifikia bado!!

Hela wanagawana wenyewe wanasiasa wanatuacha vijana wakimaskini wakifa Kwa ajali ya boda boda!!
 
I mean baada ya kupelekwa hospitali, huoni amekaa muda mrefu na moto mwilini (Deep burn) achilia mbali majeraha aliyopata baada ya kudondoka na hiyo pikipiki? Ndiomana nimeuliza huko hospitali amepona?
Kuna mwamba hapo anakatiza mbele ya camera anasema"hawezi kupona". Na ndo ukweli, hawezi kutoboa kakaa sana kwenye moto, hapo umepenya hadi ndani (deep burn) na kuharibu kila kitu huko.

Wapuuzi walikuwa na nafasi ya kutosha kumwokoa wanamshangaa tu na kumrekodi.

Ajabu hata walipomzima na kumsogeza kidogo bado wakamwacha hapo na kuuvuta tena moto ukamkuta, ndo kujiongeza kumweka pembeni ikiwa too late. Bongo za waswahili zinaload kwa speed ya 1G, ndo maana maamuzi yanakuwa ya kulegalega sana.

Bongo zetu ni special kwa kazi moja tu ya kuipitisha ccm kila baada ya 5yrs iendelee kutawala.
 
Ila watanzania ni watu wa hovyo sana. Yani limtu limekomaa ku record tu badala ya kutoa msaada linaropoka ropoka tu.
Boss mbona unawaita waTz wenzako watu wa hovyo ilhali na ww ni mTz? halafu pia mtu unamwita limtu kana kwamba hafai au hatoshelezi viwango vya kuwa ni mtu kamili?
Sioni kama huyo aliyerocord tukio kama amekosea sana kwa sababu inaelekea bodaboda darasa lao ni moja -Shingo ngumu. Leo anapata ajali huyo, kesho anakufa yule n.k.n.k. lakini wap! hawajifunzi wala hawabadiliki - utadhani ni sifa kwao.
 
U

Uache ujinga, hayamkuti mamba haya, yanatusubiri watu wa barabarani mimi na wewe.. ajali nyingine unasababishiwa, nyingine hitilafu ya chombo, nyingine uzembe wako dereva, hujui kilichotokea unaropoka tu.
Mzee barabara pana kama hiyo boda 2 zinagongana sio kichochoro hicho

Mmoja alikuwa kulia mwingine kushoto

Jiulize walikutanaje mpaka wakagongana

Uzembe mkubwa sana
 
Back
Top Bottom