Ajali ya coaster na Fuso maeneo ya Kintinku wilaya ya Manyoni Mkoa wa Singida

Ajali ya coaster na Fuso maeneo ya Kintinku wilaya ya Manyoni Mkoa wa Singida

Mjanja M1

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2018
Posts
4,058
Reaction score
14,382
IMG_20240411_110145.jpg

IMG_20240411_110142.jpg

Hii ajali imetokea asubuhi ya Leo maeneo ya Kintinku wilaya ya Manyoni Mkoa wa Singida,

Hilo Lori lilisimamishwa kwa ajili ya ukaguzi hiyo coaster ikaja kuvaa Lori kwa nyuma na kuna taarifa za kifo,

Poleni sana aisee na Mungu awatie nguvu wote waliofikwa na majanga haya.

Credit - Adventure_36
 
Kwamba kusimamishwa ilikuwa ghafla kiasi hicho au coaster ilikuwa mafuta sana!?
Bado hapo Kuna uzembe wa matumizi ya barabara
 
Kwamba kusimamishwa ilikuwa ghafla kiasi hicho au coaster ilikuwa mafuta sana!?
Bado hapo Kuna uzembe wa matumizi ya barabara

Nchi zingine panapo kizuizi mbele ishara huanzia mbali sana.

Barrier haiwezi kuwa kwenye highway.

Bila kusahau brake hufeli na hasa kwenye uhitaji wake wa ghafla.
 
Alaf wajomba hao ikitokeaga hivyo wanatoa barrier faster wanarudi kituoni 😂😂
Wajomba wana makosa ila madereva nao wana makosa, driver wa coaster angepunguza speed alipoona iyo semi mbele yake asingejibamiza ivo inamaana yeye hakujifunza kupunguza mwendo anapoona amekaribia gari lililo mbele yake kwenye uelekeo sawa? Alikuwa anawahi apite uvunguni
 
Usisahau brake huweza kufeli bila warning ndiyo maana:

Nchi zingine panapo kizuizi mbele ishara huanzia mbali sana.

Barrier haiwezi kuwa kwenye highway kama tahadhali ya msingi.
Angekuwa hayupo kibati dereva angeweza kuchochora hata pembeni kama breki ilifeli.
 
Tumshukuru muda kwani mda sasa hatujasikia ajali mbaya au mmedhibiti kiasi
Au ni askari barabarani ndio walikuwa nongwa?
Ila mnahitaji vibao vya tahadhari vingi na pia sehemu za maegesho kwa ajili ya ukaguzi wao
Maana huwa wanaamua tu popote
 
HAIRUHUSIWI kusimamisha gari zaidi ya moja kwa Askari mmoja kwa wakati mmoja kwenye kizuizi.

Maana kusimamisha gari kunatakiwa kuwe na sababu inayomlazimisha Askari kuisimamisha gari husika.

Maaskari wetu wanasimamisha magari hovyo hovyo mara nyingi bila za sababu ya Msingi.
 
Wajomba wana makosa ila madereva nao wana makosa, driver wa coaster angepunguza speed alipoona iyo semi mbele yake asingejibamiza ivo inamaana yeye hakujifunza kupunguza mwendo anapoona amekaribia gari lililo mbele yake kwenye uelekeo sawa? Alikuwa anawahi apite uvunguni
We ni dereva wa mara kwa mara!? Safari ndefu? Unaweza kutofautisha lori lililosimama na linalotembea esp kama halijawa na tadhari yoyote unayoona!?
 
We ni dereva wa mara kwa mara!? Safari ndefu? Unaweza kutofautisha lori lililosimama na linalotembea esp kama halijawa na tadhari yoyote unayoona!?
Ndiyo, najua tahadhari ni muhimu mnoo maana gari ikiwa mbele yako ukiikaribia si lazima utakuwa unapunguza speed ili muendane huku ukitafuta chance ya kuovertake au? Unataka kuniambia ukiwa safari ndefu hutakiwi kuwa na tahadhari ya speed kisa gari haijaonesha indicators zozote?
 
Nchi zingine panapo kizuizi mbele ishara huanzia mbali sana.

Barrier haiwezi kuwa kwenye highway.

Bila kusahau brake hufeli na hasa kwenye uhitaji wake wa ghafla.
Hayo yote ndio tunaita uzembe wa matumizi ya barabara kwa kifupi hapo Kuna mtu anapaswa kuwajibishwa ingawa najua hatakuwa dreva wa lorry maana sioni kosa lake
Hapo ni hao barrier na coaster
 
Back
Top Bottom