William J. Malecela
R I P
- Apr 27, 2006
- 26,584
- 10,400
halafu wanajiita wanakoma nyani...
WEKA vitu mwana, kila jiwe litageuzwa pande zote usawa huu.
Ogah,
Mkuu wangu nadhani hapa kidogo hatukuelewana. Unapofikia Ku diesign kitu ina maana tayari una matumizi yake.. Hiyo safety ni kati ya vitu vinavyoambatana na muundo wa kitu hicho iwe hata gari au shati la kuvaa. sababu kubwa ya kutengeneza gari ni kurahisisha Usafiri, na katika kurahisisha usafiri huo unatazama kwanza faida zake kiuchumi na maendeleo ya jamii..
Hivyo fikra ya kwanza ktk maendeleo ya nchi au hata mtu binafsi ni Umuhimu wa kuendelea, kujijenga kiuchumi na kuweka mapango madhubuti wa vyanzo vya kukuwezesha kufanikiwa..Na mara zote vyanzo hivi (miundombinu) ni long term strategy inayotazama kukuza uchumi wa nchi na ndicho nachozungumzia..
Barabara ya Kwenda Iringa, Mwanza, au hata Arusha ni barabara zinazojengwa/kukarabatiwa kwa sababu wananchi wanalalamika au matokeo ya vifo na kadhalika ndizo sababu zinazowasukuma serikali kuweka safety badala ya kutazama malengo ya barabara hizo kwanza..
Ukitazama barabara zote hizi vimejengwa bila plan ya miaka mingi na hasa tukilenga kukuza uchumi wetu kwani mara zote barabara zetu zina mapungufu ya safety kwa sababu tunatazama karibu matumizi tofauti ya barabara hizo.. Kila Highway nchini ina lane moja au mbili at the maximum na zote zinapita katikati ya vijiji au kando ya mji mkuu..meaning kila Freeway inapokaribia mjini hugeuka na kuwa barabara ndogo yenye traffic lights..Na ndio maana sikuona ajabu Mtanzania aliposema kuna mtu akiendesha baiskeli alikatiza..
Hivyo hata kama barabara hizi zimejengwa kwa alama za kutosha, lami, sheria na kila pambo linaloweza kupendeza, hiyo safety haiwezi kuwepo kwa sababu tunajenga mabarabara haya pasipo sababu ya maana kiuchumi. Hivyo sii tu tunaongeza ajali bali pia hatujengi miundombinu imara kwa malengo marefu ya matumizi yake kulingana na ukuaji wa uchumi tunaotegemea..
Trust me mkuu wangu hata hao watengeneza magari hutazama mahitaji ya gari ktk Usafiri unaokusudia kujenga Uchumi wa shirika husika mbele ya Quality (safety, mahitaji ya nguvu ya gari hilo, matumizi ya mafuta, na kadhalika) na ndio maana kila shirika la kutengeneza magari huwa na viwango tofauti na shirika jingine..Kitu muhimu ni kuhakikisha vina pass viwango vya standard vilivyowekwa.. Sasa kama watu tungekuwa tunapanda magari au kutengeneza magari kwa sababu ya safety, trust me by now labda magari yote yangekuwa kind of robotic engineered...
Sasa nachojaribu kusema hapa ni kwamba inatakiwa sana sisi tufikirie umuhimu wa barabara kiuchumi.. Kumwezesha wasafri, mizigo, na mazao wafike haraka, salama na katika wakati unaohitajika bila kusababisha machafuzi ktk mazingira.Barabara kuu za Mbeya, Songea, Moshi, Tanga na Kigoma, Mwanza na pengine mikoa yote zinatakiwa zijengwe na plan ya miaka kama 50 ijayo kulingana na shria za ujenzi wa Highway. Na sababu kubwa inayotanguliza ni kuunganisha sehemu hizi ili kuweza chumi za sehemu hizi kukua kiharaka... safety itakuwepo tu kwani hii ni sheria ambayo hutungwa bila gharama kubwa lakini sii ujenzi wa barabara..
Leo hii ukitaka kupanua barabara kuu yoyote ile unalazimika kuhamisha watu waliojenga kando ya barabara hizi lakini badala ya kufanya hivyo serikali yetu ikiwa ni pamoja na halmashauri za miji huweka bumps barabarani, traffic lights na kadhalika wakati hii barabara inatakiwa kuwa Freeway..haisaidii kitu kwani ajali bado zinatokea kwa wenda miguu!
Hizo barabara za Mbeya, Mwanza na hata Moshi zingejengwa kama Highway zinavyotakiwa kuwa kwa jina la Freeway..safety ingekuwepo kwani mara zote ujenzi wa Highway una viwango vyake ambavyo vinaleta hizo safety tofauti na barabara ndogo za mtaani..
FMES,
Huku Kyela wakati wa matatizo wananchi wote wanaungana kwa pamoja na hata sasa kila mtu amefurahi kusikia mbunge wao yu salama. Kwa kifupi wanamtakia heri mwanao apate nafuu.
Ila kuna jambo ambalo linaongelewa mara nyingi ambalo ni la Mwakyembe kupenda kutembea usiku. Kila mtu anasema hivyo hivyo, ashauriwe aache kusafiri usiku. Mimi sikujua hili lakini ndilo linaongelewa zaidi.
Kitu ambacho labda waandishi wetu pamoja na polisi wameshindwa kufanya uchunguzi, ni je ni kweli Mwakyembe alilala Makambako? Kama alilala makambako waliondoka hapo saa ngapi? Kutoka Makambako mpaka Ifunda kisheria ni masaa sio chini ya matatu, kama walifika Ifunda kwenye saa moja, kuna mawili, waliondoka mapema sana au walikuwa wanakimbia sana.
Pia inasemekana waliondoka Kyela saa mbili usiku; kutoka Kyela mpaka Makambako ni kama masaa matano kama unafuata sheria za barabarani. Sasa kama ni kweli ina maana walifika Makambako masaa ya saa saba, watafute guest na kulala na kuondoka kama saa kumi asubuhi, je ina make sense?
Kitu kingine ambacho inatakiwa kujua mnapochangia hili jambo ni kwamba Mwakyembe anamwamini sana huyo dereva wake. Kwenye mikutano yake mingi hudiriki hata kusema kuna watu wamejaribu kumpa mamilioni huyo dereva ili amwue lakini dereva siku zote anakataa. Huwa najiuliza kama kuna hayo mambo kwanini hawaendi polisi? Labda ni maneno ya kisiasa zaidi kuliko ukweli. Kilicho ukweli ni kwamba Mwakyembe anamwamini sana huyo dereva wake na ningetegemea kabisa afanye lolote lile kujaribu kumwokoa asiingie matatizoni.
Jambo lingine ambalo sio muhimu sana lakini wote tunajua mzee akiwa na pressure, familia yote mpaka wafanyakazi wote wanakuwa na pressure kubwa. Wiki mbili zilizopita mheshimiwa alipata pressure kubwa sana baada ya kuona ghafla upepo umebadilika Kyela. Mwakyembe ni msomi na anajua kusoma alama za wakati, kwa kweli kilichotokea kwenye hicho kikao cha halmashauri ya CCM na yaliyofuatia baada ya hapo yalimchanganya sana. Kwa kifupi ni kwamba ali panic kuona watu wamepata courage ya kusema mambo ambayo miezi michache huko nyuma wasingediriki kusema. Kwahiyo mpaka Mwakyembe anaondoka Kyela juzi, alikuwa ni mtu mwenye pressure hata kwa kumwangalia tu. Alifanya mikutano kadhaa na kutembelea baadhi ya kata kama njia ya kukabiliana na mashambulizi lakini alionekana kuwa na wasiwasi na kutumia muda mwingi kuongelewa kuandaliwa kwa milioni 400 za kummaliza yeye kisiasa. Lakini wilaya ya Kyela ni ndogo sana, mtu akimwaga hata milioni 10 itaonekana tu.
Pia sikujua kumbe Mwakyembe na dereva wake wote huwa wanatembea na pistol muda wote, kwanini? labda ndio kulinda usalama wake. Kutembea na silaha ni hatari sana, afadhali hata waheshimiwa waajiri walinzi kama wanaona maisha yao yako hatarini, vinginevyo tusije tukashangaa tukisikia yale ya Dotto. Kyela watu wengi kumbe wanajua hilo la kutembea na silaha muda wote.
Muhimu kwasasa ni kumwombea mwakyembe apone kabisa na tuendelee na mambo ya kujenga nchi yetu kuelekea uchaguzi 2010. Nimjuavyo Mwakyembe sitashangaa kusikia kwenye mikutano yake ya Kyela hasa huko vijijini akisema kulikuwa na mkono wa mafisadi na walitaka kumwua.
Kikwete na ujumbe wake wamekuja mara nyingi Marekani na ulaya na sehemu nyingine ambapo miundo mbinu ya barabara ni ya kisasa. Kwa miaka 10 amekuwa waziri wa mambo ya nje, wasaidizi wake wengine walikuwa huku huku kijijini; wapo watu pale Mambo ya Nje ambao wanajua kabisa kinachoendelea.
Malengo ya barabara yanajulikana tangu enzi za mababu; tatizo siyo kutokujua malengo au kutokujua umuhiimu wa barabara au suala zima la usalama. Tatizo ni kubwa zaidi kuliko tunavyofikiria; na halihusianni na kutokujua. Mapendekezo yanayotolewa yamekuwa yakitolewa kwenye "wiki ya nenda kwa usalama" tangu nikiwa mtoto mdogo na yamekuwa yakitolewa na kuibuliwa Bungeni kila kikao cha bajeti! Kwamba barabara kutokana na ufinyu wake zimechangia ajalii linajulikana.
so.. kwanini tunafikiria tukiumba wimbo ule ule ila tukibalisha mpangilio wa beti, basi mbuzi atacheza?
Kama mbuzi hachezi mnafikiri tatizo ni muziki au track ya CD yenyewe..
Mtanzania,
Utachokaje kumsihi dereva wako awe mwangalifu? Maisha yako unayaacha mikononi mwa reckless driver umechoka? Kumbe ndio maana wenzetu walishaona kila mtu ajiendeshe mwenyewe, unless u're vice president.
Kikwete na ujumbe wake wamekuja mara nyingi Marekani na ulaya na sehemu nyingine ambapo miundo mbinu ya barabara ni ya kisasa. Kwa miaka 10 amekuwa waziri wa mambo ya nje, wasaidizi wake wengine walikuwa huku huku kijijini; wapo watu pale Mambo ya Nje ambao wanajua kabisa kinachoendelea.
Malengo ya barabara yanajulikana tangu enzi za mababu; tatizo siyo kutokujua malengo au kutokujua umuhiimu wa barabara au suala zima la usalama. Tatizo ni kubwa zaidi kuliko tunavyofikiria; na halihusianni na kutokujua. Mapendekezo yanayotolewa yamekuwa yakitolewa kwenye "wiki ya nenda kwa usalama" tangu nikiwa mtoto mdogo na yamekuwa yakitolewa na kuibuliwa Bungeni kila kikao cha bajeti! Kwamba barabara kutokana na ufinyu wake zimechangia ajalii linajulikana.
so.. kwanini tunafikiria tukiumba wimbo ule ule ila tukibalisha mpangilio wa beti, basi mbuzi atacheza?
Kama mbuzi hachezi mnafikiri tatizo ni muziki au track ya CD yenyewe..
"I will not in under any circumstances backslide in my crusade against corruption," he said, replying to a question from a journalist.
"As a member of the family, I see no need for investigations. And I believe this is the whole family's position," he said, adding the reports on his brother's accident had been exaggerated. Mr Mwakyembe called for calm as his brother recovers in hospital.
Dr Mwakyembe said the speeding truck driver looked into his side mirror as his vehicle was about to pass by it.Upon realising what lorry driver was doing, Dr Mwakyembe said he advised his driver to speed, driving at more than 140 km/hour in order to overtake it.
Overspeeding, dereva aka-loose control
The truck then smashed into the MP's vehicle, pushing it off the road as the driver smashed into a pothole and lost control. Dr Mwakyembe said his vehicle rolled three times, as its tyre burst before it smashed into a tree.
Hii kwa upande wangu naona kama sio kweli, Dereva wa Gari alilokuwa Mwakyembe lazima atakuwa aliomba ku-overtake na aliruhusiwa sasa swala la kugongwa na lori sijui lina kujaje hapa!!?
Police said on Thursday that preliminary investigations established that was purely a road accident. "There is no evidence to prove that it was a plot to kill the MP. We have established the cause of the accident was hitting the pothole,"
Kwa nini watanzania kila linalotokea kwa kiongozi huwa tunafikiria kuwa ilikuwa planned?
...haya sasa, mheshimiwa mzima anaanza kutuletea paukwa pakawa! akisema hivyo kina Mudhihir Mudhihir na Kapuya nao waliopata ajali watasemaje?
...alijuaje kwenye taa ya nyuma iwapo alipoteza fahamu kwa mshituko? ...kahadithiwa?
...Kwenye picha, taa ya kulia inaonekana nzima. Ndio kusema kama lori lilikuwa linawafuata kwa kasi na kuwagonga lingewagonga taa ya kulia, sio kushoto.
Aseme tu baada ya ku overtake dereva wake alipunguza mwendo ghafla kuogopea hako kashimo lndio maana wakagongwa kushoto!...
Simlaumu dereva, anatetea unga wake.
...kama limechomoka ajabu ni nini kwenye impact kama hiyo?
Upon realising what lorry driver was doing, Dr Mwakyembe said he advised his driver to speed, driving at more than 140 km/hour in order to overtake it.
Kweli TZ hatuko makini kabisa, ile barabara ya Mbeya - Iringa unaweza kuendesha kwa speed ya zaidi ya 140km/h? Hizo ni karibu 90 miles/h kwa UK ambayo ni overspeeding ya 20miles zaidi ya maximum speed kwa motor ways za UK.
Huyu mungu tunamweka kwenye majaribio kweli kweli wakati uzembe ni wetu wenyewe. Kwa ile barabara hata speed ya 100kms/h bado haifai na ukigonga mnyama au binadamu gari litatupwa nje tu.
Ingelikuwa nchi za wenzetu, kwa huo mwendo ambao wamekiri walikuwa wanaenda, huyo dereva angenyang'anywa leseni hapona kufungiwa kuendesha kwa zaidi ya mwaka mmoja na faini juu. Lakini kwasisi Waafrika tutaishia kusema kuna mkono wa mtu.