Ogah,
Mkuu wangu nadhani hapa kidogo hatukuelewana. Unapofikia Ku diesign kitu ina maana tayari una matumizi yake.. Hiyo safety ni kati ya vitu vinavyoambatana na muundo wa kitu hicho iwe hata gari au shati la kuvaa. sababu kubwa ya kutengeneza gari ni kurahisisha Usafiri, na katika kurahisisha usafiri huo unatazama kwanza faida zake kiuchumi na maendeleo ya jamii..
Hivyo fikra ya kwanza ktk maendeleo ya nchi au hata mtu binafsi ni Umuhimu wa kuendelea, kujijenga kiuchumi na kuweka mapango madhubuti wa vyanzo vya kukuwezesha kufanikiwa..Na mara zote vyanzo hivi (miundombinu) ni long term strategy inayotazama kukuza uchumi wa nchi na ndicho nachozungumzia..
Barabara ya Kwenda Iringa, Mwanza, au hata Arusha ni barabara zinazojengwa/kukarabatiwa kwa sababu wananchi wanalalamika au matokeo ya vifo na kadhalika ndizo sababu zinazowasukuma serikali kuweka safety badala ya kutazama malengo ya barabara hizo kwanza..
Ukitazama barabara zote hizi vimejengwa bila plan ya miaka mingi na hasa tukilenga kukuza uchumi wetu kwani mara zote barabara zetu zina mapungufu ya safety kwa sababu tunatazama karibu matumizi tofauti ya barabara hizo.. Kila Highway nchini ina lane moja au mbili at the maximum na zote zinapita katikati ya vijiji au kando ya mji mkuu..meaning kila Freeway inapokaribia mjini hugeuka na kuwa barabara ndogo yenye traffic lights..Na ndio maana sikuona ajabu Mtanzania aliposema kuna mtu akiendesha baiskeli alikatiza..
Hivyo hata kama barabara hizi zimejengwa kwa alama za kutosha, lami, sheria na kila pambo linaloweza kupendeza, hiyo safety haiwezi kuwepo kwa sababu tunajenga mabarabara haya pasipo sababu ya maana kiuchumi. Hivyo sii tu tunaongeza ajali bali pia hatujengi miundombinu imara kwa malengo marefu ya matumizi yake kulingana na ukuaji wa uchumi tunaotegemea..
Trust me mkuu wangu hata hao watengeneza magari hutazama mahitaji ya gari ktk Usafiri unaokusudia kujenga Uchumi wa shirika husika mbele ya Quality (safety, mahitaji ya nguvu ya gari hilo, matumizi ya mafuta, na kadhalika) na ndio maana kila shirika la kutengeneza magari huwa na viwango tofauti na shirika jingine..Kitu muhimu ni kuhakikisha vina pass viwango vya standard vilivyowekwa.. Sasa kama watu tungekuwa tunapanda magari au kutengeneza magari kwa sababu ya safety, trust me by now labda magari yote yangekuwa kind of robotic engineered...
Sasa nachojaribu kusema hapa ni kwamba inatakiwa sana sisi tufikirie umuhimu wa barabara kiuchumi.. Kumwezesha wasafri, mizigo, na mazao wafike haraka, salama na katika wakati unaohitajika bila kusababisha machafuzi ktk mazingira.Barabara kuu za Mbeya, Songea, Moshi, Tanga na Kigoma, Mwanza na pengine mikoa yote zinatakiwa zijengwe na plan ya miaka kama 50 ijayo kulingana na shria za ujenzi wa Highway. Na sababu kubwa inayotanguliza ni kuunganisha sehemu hizi ili kuweza chumi za sehemu hizi kukua kiharaka... safety itakuwepo tu kwani hii ni sheria ambayo hutungwa bila gharama kubwa lakini sii ujenzi wa barabara..
Leo hii ukitaka kupanua barabara kuu yoyote ile unalazimika kuhamisha watu waliojenga kando ya barabara hizi lakini badala ya kufanya hivyo serikali yetu ikiwa ni pamoja na halmashauri za miji huweka bumps barabarani, traffic lights na kadhalika wakati hii barabara inatakiwa kuwa Freeway..haisaidii kitu kwani ajali bado zinatokea kwa wenda miguu!
Hizo barabara za Mbeya, Mwanza na hata Moshi zingejengwa kama Highway zinavyotakiwa kuwa kwa jina la Freeway..safety ingekuwepo kwani mara zote ujenzi wa Highway una viwango vyake ambavyo vinaleta hizo safety tofauti na barabara ndogo za mtaani..