Ajali ya Dr. Mwakyembe na yatokanayo

Ajali ya Dr. Mwakyembe na yatokanayo

ni kweli lakini tusubiri taarifa zaidi kutoka serikalini kuhusiana na majaaliwa yake,kwani anahamishiwa kwa wataalamu zaidi wa tiba.
 
gurudumu likachomoka? really? isijekuwa kuna mtu alilegeza nati za gurudumu kabla ya safari!!!!!

La msingi hapa ni kumshukuru Mungu kwa kumjaalia kupona na tumuombee ampe subira na apate nafuu ya kupona haraka kwa baraka zake maana huu ulikuwa mtihani mgumu kwakwe. Tukianza kutia dhana na ushirikina tutakuwa tunaenda kinyume na mafundisho ya dini. Ajali ni ajali inaweza kutokea kwa mtu yeyote wakati wowote. Kama Mungu hakupenda hata ukilegeza nati haisaidii kitu.
 
Inasemekana kuwa dereva wake alikuwa akiovateki (akilipita) lori, lakini kwa bahati mbaya akagonga kwenye shimo lililoko barabarani na kulifanya gari lipinduke mara kadhaa!
Naamini Mungu atamponya! AMEEEEEEEEEN!!!!!

...na bado 'doubters' watasema 'nanihii' ndio aliolichimba hilo shimo! kaazi kweli kweli...
 
Pole sana Mpiganaji wetu Mungu anakupenda tunakuombea upone mapema.Mafisadi washindwe na walegee kwa jina la Yesu.Tukigundua sababu ni wao tutajua la kufanya.
 
Inasemekana kuwa dereva wake alikuwa akiovateki (akilipita) lori, lakini kwa bahati mbaya akagonga kwenye shimo lililoko barabarani na kulifanya gari lipinduke mara kadhaa!
Naamini Mungu atamponya! AMEEEEEEEEEN!!!!!

Driver wa lorry aliwaruhusu ku overtake akini walipofika katikati akwabana walibidi waingie kwenye shimo na ku overturn. Was it intentional au bahati mbaya???????????????????
 
Pole sana Mpiganaji wetu Mungu anakupenda tunakuombea upone mapema.Mafisadi washindwe na walegee kwa jina la Yesu.Tukigundua sababu ni wao tutajua la kufanya.

...I hope una maana; wakandarasi 'mafisadi' wanaofanya matengenezo kwenye hiyo barabara bila kuweka alama "punguza mwendo, kuna mashimo ya hapa na pale!"...

...Barabara ile unaijua au unaisikia? kwanza nyembamba...pili kuna mashimo makubwa na madogo ya kushtukiza, tatu sehemu nyingi zimetitia hivyo ni kunesa utadhani uko kwenye bembea.

Miezi michache iliyopita nilipita barabara hiyo. Kwa kweli kipande cha Mafinga-Iringa kilikuwa kibaya na matengenezo yalikuwa yanafanyika sehemu kadhaa.

Pole Dr. Mwakyembe.
 
Driver wa lorry aliwaruhusu ku overtake akini walipofika katikati akwabana walibidi waingie kwenye shimo na ku overturn. Was it intentional au bahati mbaya???????????????????

...acha ku- spin habari bana!
 
Pole sana mpiganaji wetu,tunakuombea kwa Mungu upate nafuu haraka.
 
Duuhh hii kali.....hawa ma-Guest vipi jamani...hebu wachekini

Currently Active Users Viewing This Thread: 254 (66 members and 188 guests)

Ogah,

Wapo kazini... Wangejua kuna mambo wanakosa wakiwa guests...!
 
Naona idadi ya guests inazidi kuongozeka kha!
Jamani si mjiunge tu karibuni.
 
Amebebwa na gari la Polisi PT 0213 na amekuja na Ndege TanzAir 5H-TZT.

Waliofika ni pamoja na (wabunge) Shelukindo, Mpendazoe, Kimaro, Katibu wa Bunge na maafisa wa Bunge pamoja na Katibu wa kamati ya Miundo mbinu na Michael Nyaruma pamoja mzee Mengi wapo pia.

Anaendelea vizuri (kwa maelezo ya wauguzi) lakini amebebwa kwenye kitanda cha kubebea wagonjwa na aliweza kunyanyua mkono kuwasalimia waliofika kumpokea.

Anapelekwa Muhimbili inaelekea
 
Taarifa ya habari TBC saa 10 jioni. Dk MWakyembe hajaumia sna ila ana michubuko na anaongea. Daktari anayemtibu (alizungumza live) anasema kuwa amevimba usoni inaonekana alijigonga sana wakati wa ajali ila hajavunjika sehemu yoyote.
 
Mwenyezi mungu ni mwingi rehema na ukarimu, tunamuomba amponye mzamivu mwakyembe na arejee ktk hali njema.

Pole sana mzamivu harrison george mwakyembe.
 
Ndo wamevuka mataa ya Chang'ombe wanaelekea Muhimbili.

Picha ni hizi

i388_2.JPG

Dr Mwakyembe akifikishwa hospitali ya mkoa wa Iringa leo baada ya ajali

i389_Gari.JPG

Gari la Dr Mwakyembe likiwa limeharibika vibaya baada ya ajali

i390_Shimo.JPG

Shimo lililosababisha ajari ya Dr Mwakyembe
 
ndo wamevuka mataa ya chang'ombe wanaelekea muhimbili.

Picha ni hizi

2.jpg


dr mwakyembe akifikishwa hospitali ya mkoa wa iringa leo baada ya ajali

gari.jpg


gari la dr mwakyembe likiwa limeharibika vibaya baada ya ajali

shimo.jpg

shimo lililosababisha ajari ya dr mwakyembe
mkuu invisible,wengine tu computer twetu ni twa internrt za uchochoroni kariakoo hazina uwezo wa kufungua hizo picha.zitundike moja kwa moja mkuu!
 
Francis ametoa picha lakini hakutenda haki kuweka picha ya waziri mkuu wa kwanza wa awamu ya nne ktk taarifa yake na hata ambatanisho la ripoti yake Mwakyembe. Ktk hali ya mtu kupigania maisha yake tujitahidi kuwa waungwana. I hate gossiping at sad moment.
Nawasilisha
 
Wamefika Muhimbili, naambiwa hata Masilingi naye kaungana na waliomsindikiza Dr. Mwakyembe hospitalini hapo.
 
Madaktari wanafanya kazi yao, washamchukua mgonjwa na kumpeleka wodini. Wengine wamebaki nje wanasubiri kupewa taarifa ya nini kinaendelea.
 
Back
Top Bottom