Ajali ya Dr. Mwakyembe na yatokanayo

Ajali ya Dr. Mwakyembe na yatokanayo

Kazi kweli kweli, sasa mambo kama haya yanafanya watu wafikirie mbali bila sababu, huyu Kombe anatakiwa ajiuzuru kulinusuru jeshi la Polisi na kurudisha heshima na imani kwa serikali. Kama hajiuzuru basi astaafishwe kwa manufaa ya uma. Vinginevyo makubwa na maajabu yatatokea mwakani, na mauaji ya ajabu yatatokea pasipo sababu muhimu.

Balibona ninkenyuka.....nani amstaafishe Kombe? IGP Mwema?... ameibiwa laptop 'akakaa kimya', woga! Weak state under the cage! habari ndiyo hiyo.
 
Mwakyembe,

Mimi sishangai kabisa kwa kitendo hiki cha polisi.

Kwa upande wa ajali polisi ni wazembe kweli kweli.

Ninajua kisa cha hivi karibuni tu cha mtu mmoja ambaye alikuwa akiendesha pikipiki yake na akakutana kwenye kona na gari aina ya defender ikiwa imemimina mbio tena ikiwa imeegemea upande wake wa kushoto alikokuwa.

Alipoona dreva aonekani kurudi upande wake wa kulia na yuko mbio, alijaribu kumkwepa na wakagongana uso kwa uso.

Baada ya ajali yule mwendesha pikipiki alibahatika kutopoteza maisha lakini alivunjika mguu sambamba na abiria aliyekuwa katika ile gari ambaye alikuwa ni utingo ambaye naye alivunjika mguu.

Huyu mwendesha pikipiki pamoja na yule abiria katika lile gari walikimbizwa hospitali na kulazwa kwa ajili ya matibabu, na maaskari wa usalama wa barabarani walikimbia kwenda kupima ajali na kuondoka na ile pikipiki na kuipeleka kituoni. Walimuhoji yule mwendesha pikipiki na akatoa maelezo yake huku akiwa hospitalini na kuondoka, pia walimuoji na yule tingo wa gari. Lakini kwa mujibu wa tingo wa gari ile, ni kwamba gari haikuwa hata na breki.

Ajabu ni kwamba ile gari haikuwahi kukanyaga katika kituo cha polisi na hata kukaguliwa. Lakini yule dreva wa gari alitoa maelezo yake kuwa alimgonga mwendesha pikipiki kwa sababu yule mwendesha pikipiki alikuwa anaendesha pikipiki huku akizungumza na simu na wao polisi wakakubaliana naye kirahisi hivyo tu. Game likaishia hapo. Na hakukanyaga polisi kituoni.

Alipokwenda yule mwendesha piki piki kuulizia pikipiki yake alitakiwa kulipia faini ili achukue pikipiki yake iliyoumia kwa maelezo kuwa ilikuwa na makosa na yeye ndiye alisababisha ajali. Alipouliza kuhusu gari lililomgonga, aliambiwa yule wa gari alilipa faini yake na game liliishia pale alipolipa faini, hivyo naye alipe faini game liishe.

Huu ndio utendaji kazi wa polisi wetu. Ni vigumu kuamini kama wanafanya vitu kitaaluma kama wanavyojisifia katika kesi ya Mwakyembe. Kwa ushahidi niliosimulia hapo juu siamini kama hata ya Mwakyembe wanayasema kwa nia njema. Ni wababaishaji tu huku wakijiingiza kisiasa kutokea kona nyingine.

Ole wao.
 
Polisi si wamesema wanamshitaki dereva? Basi huko ndiko Dr. atakuwa na nafasi kubwa ya kuthibitisha haya aliyoyatoa leo. Kama polisi wamemtungia jambo basi huko pia ataweza kuwabana vizuri.

Ila tu kusema lile gari liligongwa na lori kwa nyuma kwenye speed ya around 140k/h, basi mungu wa Mwakyembe anamlinda kweli, maana sio tu alimlinda yeye lakini pia alililinda na gari lake.

Penye ukweli uwongo hujitenga.
 
Hata kama kosa lilifanyika na kamati ya Bunge, Kosa Moja hali halalishi kosa jingine

Hivi Wabongo tumerogwa? Tunafikiri nini sisi watu?

Yani unakubali kwamba Mwakyembe alichemsha kutokumpa mwenzake hiyo ``natural justice`` halafu akaja baadae kuwa na moral authority ya kufundisha mapolisi kuhusu ``natural justice`` wewe unaona ni sawa?

Ni ushabiki shabiki wa kufuata upepo au ni kwamba wananchi hatuna a smidge of civic education na uelewa?

LeoKweli, are you serious?
 
Mwakyembe leo alalamikia ``natural justice``? Mwakyembe? Huyu mwalimu wa wanafiki alimhoji Lowassa?
Dilunga,
Achana na Lowassa. He conveniently disappeared alipopewa taarifa ya kuhojiwa na leo anajidai kuwa victim. Hapana. Kama ni victim, mbona alijiuzulu? Angetumia muda wake bungeni kujibu shutuma lakini alikacha? Achana naye!
 
- DK, hana sababu yoyote ya kuanza kwenda kwenye mahakama hizi uchwara uchwara, amepona akishakua back infour kwa 100% aende kanisani na kumshukuru Mungu wake, arudi kwenye the agenda yaani masilahi ya taifa akienda kwenye mahakama basi ataendelea kuwapa mafisadi ushindi wa bure na ndicho wanachokisubiri kusudi wakamuumbue kule kwa kuanza kumuhoji maswali ya conflit of interest, DK achana nao hao, tunapowambieni hapa kwamba mafisadi wamekutana kwa siri na wamepanga one, two three huwa hatutanii recently mfadhili wao mkuu Karamagi, amekua mkali sana akidai results ya mamillioni ya hela zake anazowapa kwa ajili ya operations mbali mbali ndio maana sasa hivi wapo alll over wanahaha,

- Mengine ni simple common sense, kama mafisadi wanaweza kumtisha mtuzima kama Pinda akaishia kigugumizi, eti Meremeta ni ya jeshi hakuguswi huko kisheria, sasa itakuwa huyo hakimu mkazi wa kuamua hii kesi ya ajali? Tena inayomusu DK? Ohh please aachane nao hao, amepona akirudi infour asonge mbele tu!

Respect.

FMES!

Mtanzania: Check PM.
 
"Polisi si wamesema wanamshitaki dereva? Basi huko ndiko Dr. atakuwa na nafasi kubwa ya kuthibitisha haya aliyoyatoa leo. Kama polisi wamemtungia jambo basi huko pia ataweza kuwabana vizuri."

________________________

Mtanzania:
Una hakika gani kwamba hawa mapolisi wa Masha watamwita Dr mahakamani? Watamwitaje bila kumhoji kwanza -- akienda kuwaumbua? Script ya mapolisi haikuwa na agizo la kumhoji Dr, basi. Umesahau 1996 mke wa Amrani Kombe, aliyeshuhudia kwa macho kuawa kwa mme wake hakuwa ameitwa mahakamani pale awali?

Kesi ya Mallya; kuna mashuhuda muhimu, -- wale waliofika mwanzo kabisa baada ya ile "ajali" ya Wangwe hawakuitwa mahakamani.
 
Tatu, kama suala hapa ni uelewa wa sheria husika, mwenendo wa upelelezi na wa mashitaka, ni nani katika Kamati hiyo ya Kombe anayeweza akadai kuwa na uelewa mpana na wa kina kunipita?

Inanikumbusha mambo ya waziri mkuu majivuno wa Kusadikika "Weusi wa nyweli za mshitakiwa waonyesha kwa kiasi gani hana busara"
 
Tahadhari kwa wote wanaopiga vita ufisadi, ni wakati wa mafisadi kujua kuwa wataua karibu watanzania wote lakini mwisho haki itasimama. hongera mh Mwakyembe.

Hekima
 
Jeshi la polisi, halina huduma hili kwa jamii na kukubalika kwake na watu nadhani ni chini ya 50%. It commands bad image.
 
Tatu, kama suala hapa ni uelewa wa sheria husika, mwenendo wa upelelezi na wa mashitaka, ni nani katika Kamati hiyo ya Kombe anayeweza akadai kuwa na uelewa mpana na wa kina kunipita?
Inanikumbusha mambo ya waziri mkuu majivuno wa Kusadikika

E bwana Mtanzania, kumbe umemwona huyu Mbunge anavyoongelesha viongozi wenzake hivyo? Kwa nini anapeta lakini? Watanzania nilidhani culturally hatupendi watu wenye majivuno na dharau. Yana mwisho...

Dilunga,
Achana na Lowassa. He conveniently disappeared alipopewa taarifa ya kuhojiwa ...

Jasusi, tuwe wakweli. Lowassa hakuwahi kuitwa na kamati. Leo Mwakyembe analilia "natural justice." Duuu...
 
Inanikumbusha mambo ya waziri mkuu majivuno wa Kusadikika "Weusi wa nyweli za mshitakiwa waonyesha kwa kiasi gani hana busara"


Hilo tu ndilo uliloliona? Nani amekukataza kujiamini? Sisi wanyaki ndivyo tulivyo kama umepona mshukuru Mungu
 
Tatu, kama suala hapa ni uelewa wa sheria husika, mwenendo wa upelelezi na wa mashitaka, ni nani katika Kamati hiyo ya Kombe anayeweza akadai kuwa na uelewa mpana na wa kina kunipita?

- Katika dunia ya kibepari kama tuliyonayo Tanzania sasa hivi, haya maneno ni ya kawaida sana na ni vyema sisi wananchi tukaji-tune na kuyakubali ili tuondokane na zile attitude za kijamaa jamaa, za kutambea na kandambili huku ni millionea kwa sababu ya kuogopa kuonekana unaringa na jamii,

- Yale mambo ya darasa la saba Mwenyekiti wa tawi la CCM kiwandani, kushindana na PhD yaani Director wa kiwanda na kuishia kuwa taifa la kwanza duniani kuwa na viwanda vya Sigara na Bia visivyoleta faida kwa taifa, sasa yameisha kama wewe ni bingwa wa fani yoyote ile, ubepari inataka useme tena sana au wazi bila kuficha kwa sababu under siasa ya ubepari tuliyonayo sasa hivi, huwezi jua opportunity ita-strike wapi na wakati gani,

- Bila majivuno ubepari hauwezi kushamiri, hakutakuwepo na competition katika biashara, hakutakua na competition katika siasa, tutaishia kurudi kule kule tulikotoka, kama ni majivuno basi hata mashindano ya uzuri wa kinadada zetu ni dhambi na majivuno kwani wanaoshindwa maana yake ni nini kama sio ugly? Je wewe uliowatoa kwenye mashindano unaweza kuwaumba ndio hizo mentality za kudai ukweli ni majivuno, hazina nafasi tena katika taifa letu,

Mwakyembe either ni bingwa sheria au sio, lakini ndio anayo haki zote kujitangaza kwa public na dunia, ndio ubepari tunaoutaka unavyotaka ndio maana unaona watu kama Michuzi sasa wanapeta maana anachikifanya kule Michuzi blog ndio hasa maana ya ubepari, indivualism kwanza!

Ahsante Wakuu.

William.
 
Last edited:
Hivi Mwakyembea mbona muongo hivi huyu Mbunge? Leo anadai alisema toka awali hii ni ajali, na hiki nini:

Mkuu unatafuta dosari au unafuatilia hoja? Uongo upi kausema Mwakyembe? Tatizo ni wewe unayemnukuu kutokana na gazeti ulilosoma, si ajabu Nyundo au TAZAMA, magazeti ya Rostam na Karamagi! Mimi hapa nina Majira ya Jumamosi Mei 23 inasema ukurasa wa mbele: "DKT. MWAKYEMBE: HAKUNA HUJUMA". Vilevile ukurasa wa nne wa gazeti hili, mwandishi anaripoti kuwa: "Bw. Mwakyembe alipotakiwa kueleza kama kuna hujuma kwenye ajali hiyo, alisema ni ajali ya kawaida na kwamba anamwachia Mungu".

Kama Kiingereza kinapanda, basi hata gazeti la The Citizen la siku hiyohiyo linamnukuu Mwakyembe akisema: "I believe this was a normal traffic accident. If it was God's wish I pray that he helps me to heal but if it was man-made, I also leave it to God".

Sasa Mkuu utamwitaje Mwakyembe muongo anaporudia maneno hayo leo? Dilunga acha fitina. Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni! Mwakyembe ni kichwa brother, utake usitake!
Fataki
 
Hilo tu ndilo uliloliona? Nani amekukataza kujiamini? Sisi wanyaki ndivyo tulivyo kama umepona mshukuru Mungu

Kwi kwi kwi!! Sikujua Wanyaki mna majivuno hivyo! Toka lini majivuno na kujiamini vikawa na maana moja? Hivi uelewa mpana na wa kina unapimwa vipi?

Kazi kweli kweli TZ!
 
It is unfortunately that we are losing our country in this manner;
  1. The Presidency - SOLD in 2000
  2. The Government - SOLD in 2000
  3. The Law Enforcement Units - SOLD in 2009 or earlier
  4. The Judicial System - Bids awaiting, but mingling the good and the ugly already in progress
  5. Legislative - Majority SOLD
  6. The Fourth Estate (Media) - SOLD or Strangled Absolutely
  7. The Army - SOLD to the politicians (Chief of Staff is a multmilionair fundraiser nowdays)
Were is Tanzania Going? Cry My Country, Cry.
 
Dilunga; Jasusi said:
Dilunga,
Hata kama hakuitwa kwenye kamati (for whatever reasons) lakini alikuwa na muda tosha kujitetea bungeni. Ila kilichotokea ni kwamba zile karatasi watu wake wa UWT walizoiba ofisini kwa Spika zilikuwa fake na kwa hiyo hakupata muda wa kujitetea wakati Mwakyembe aliposoma ripoti halisi. Hakuweza kujitetea kwa sababu alijua alichokifanya. Akajiuzulu na rafiki yake akamridhia.
 
- Shujaa wangu Mwakyembe, achana na haya malumbano lumbano yasiyo na faida,rudi kwenye ku-focus na ishu muhimu za taifa kama zamani ulivyokuwa,

- Hivi nyinyi mlio karibu naye mmegundua kuwa ni muda mrefu sana sasa mafisadi wamemuondoa kwenye focus ya taifa na kumuweka kwenye ulingo wa kuji-defend defend tu all the time kwa muda mrefu sasa, please Mwakyembe next press release au Conf. iwe ya kumkoma nyani waambie likizo imeisha,

- Ninakuombea kwa Mungu upone haraka, lakini please usijibishane tena na mafisadi maana katika miezi sita iliyopita umeruhusu mafisadi kukupangia agenda za kujitetea tetea bila ya ishu muhimu kwa taifa, please wake up DK yanayokutoea sio bahati mbaya wala amri ya Mungu, ni amri ya mafisadi huwa hatupendi ksuema sana, sasa it is about time ukawatandika where it hurts the most kama ulivyofanya bungeni siku ile na kuwakimbiza mafisadi watatu kwa mpigo, that was wasup! Sio hizi blah! blah! na yada! yada!

- Hit them back na ufisadi wao, si kuna mengine hukusema bungeni yamwage sasa unaona faida ya kuwaonea huruma wao hawana huruma hao mafisadi! na sasa hivi you are where they want you to be! yaani on defensive! Wangu ni ushauri wa bure tu!

Mungu Aibariki Tanzania na Akubariki Upone Sasa.

FMES!

Mkuu FMES, you are more than right! Lakini tatizo hapa si Dk. Mwakyembe: ni mimi, wewe na wao. Tunakaa kimya as spectators tukiacha watu wazuri wakipigwa below the belt. Hatusimami kutetea haki. What do we expect from our ill-informed public? Tunaponyamaza wananchi wanaamini udaku unaosambazwa na hawa mafisadi! Hivyo akina Mwakyembe wanalazimika from time to time to stand up and fend for themselves! Hii Bongo bwana, bla bla bla za solidarity nyingi, lakini vitendo sifuri!
 
Back
Top Bottom