Mkuu kwa upande fulani unachosema ni kweli. Hata waingereza wanasema kama huna facts huna haki ya kuongea. Kuna ukweli fulani ndani yake. Ndio maana hata wabunge wetu ambao walikimbia umande bungeni wanakaa kimya tu. La mmuhimu ni kuwa na facts zaidi ili tuweze kuwa na haki ya kuongea.
Mkuu mie nafikiri hili ndilo tatizo letu watz ,ndio maana unaona hata viongozi wetu wanamtazamo kama wakina mwakyembe kwamba sisi /ama baba yangu ndiye aliyepigania uhuru kwa hivyo mimi ndiye ninahaki ya kufanya vile ama hivi.
Kingine kwenye ajali bwana ni vigumu kukumbuka eti ilitokea hivi na vile,chukulia mfano ukipoteza kitu tena mbali lakini kwa ajili ya ubanadamu utakuwa unahisi kabisa ulikiweka mahala fulani kumbe wapi bwana?
Mfano.Mie pia nakumbuka hawa majambazi waliwahi kuvamia ka kioski ka nyumbani na wakapiga risasi moja tu ,lakini nilipotoka hapo mimi nilibisha sana na kusema jamaa walimimina risasi nyingi.
Harafu tukirudi kwenye De facto hivi hilo lori lilikuwa ktk speed gani hadi kuligonga gari kwa nyuma lenye speed 140km/h.chochode huyo aliyegonga alikuwa na ishuarensi gani ktk speed over 150km/h atasalimika baada ya kugonga? Mhhhhhhhhh nafikiri bongo bado hatujafikia mahala pa kuanza kujitoa mhanga namna hiyo.