Ajali ya Dr. Mwakyembe na yatokanayo

Ajali ya Dr. Mwakyembe na yatokanayo

Mkuu kwa upande fulani unachosema ni kweli. Hata waingereza wanasema kama huna facts huna haki ya kuongea. Kuna ukweli fulani ndani yake. Ndio maana hata wabunge wetu ambao walikimbia umande bungeni wanakaa kimya tu. La mmuhimu ni kuwa na facts zaidi ili tuweze kuwa na haki ya kuongea.

Mkuu mie nafikiri hili ndilo tatizo letu watz ,ndio maana unaona hata viongozi wetu wanamtazamo kama wakina mwakyembe kwamba sisi /ama baba yangu ndiye aliyepigania uhuru kwa hivyo mimi ndiye ninahaki ya kufanya vile ama hivi.

Kingine kwenye ajali bwana ni vigumu kukumbuka eti ilitokea hivi na vile,chukulia mfano ukipoteza kitu tena mbali lakini kwa ajili ya ubanadamu utakuwa unahisi kabisa ulikiweka mahala fulani kumbe wapi bwana?

Mfano.Mie pia nakumbuka hawa majambazi waliwahi kuvamia ka kioski ka nyumbani na wakapiga risasi moja tu ,lakini nilipotoka hapo mimi nilibisha sana na kusema jamaa walimimina risasi nyingi.

Harafu tukirudi kwenye De facto hivi hilo lori lilikuwa ktk speed gani hadi kuligonga gari kwa nyuma lenye speed 140km/h.chochode huyo aliyegonga alikuwa na ishuarensi gani ktk speed over 150km/h atasalimika baada ya kugonga? Mhhhhhhhhh nafikiri bongo bado hatujafikia mahala pa kuanza kujitoa mhanga namna hiyo.
 
ndugu yangu hata mimi mwanzoni nilifikiria ni suala la kutokuelewa, lakini baada ya kujaribu sana kuelewesha nikagundua kuwa mtu ambaye hajui kuwa haelewi na hataki kujua kuelewa utamuelewesha vipi? Ila tutafika tu.

Shukrani lakini pasipo mwenyewe kujua impact yake, nadhani ni makala iliyonitengenezea maadui wengi zaidi kuliko yoyote ile na wakati huo huo labda kusema kitu ambacho wengine walikuwa wanakifikiria kwa muda mrefu na hawakupata nafasi au mahali pa kukisemea. Thanks.

Mkuu MMM na mimi nietoke nje kidogo ya mjdadala nikupe mkono wa pongezi, japo mtupu, manake mi nimesona hard copy kabisa ya hilo gazeti, picha iliyonijia ni ile ya malumbano ya Kasungura na ndege ya uchumi, nikasema hivi mkuu wangu Mwanakijiji 'hawajamalizana' na Lowassa tu? Lakini ulichoandika, kwa mwelewa, ni kweli tupu...I hope iko somewhere huku JF na wengine waisome, ili wanapofananisha ajali ya Mwakyembe na suala la Lowassa kujiuzulu, wajue tumetoka wapi...ni sawa na kufananisha wingu na moshi
 
Kama kila ajali inahitaji kuundiwa kamati, tutaunda kamati ngapi?
 
Hivi wakuu zangu nambieni..
Pamoja na Mwakyembe kukatazwa kutoa taarifa yoyote kuhusiana na ajali hii, hayo maelezo yake hapo juu yanatueleza kitu gani.. Cha msingi nadhani tupime maelezo yake haya baada ya kukatazwa kuingilia uchunguzi ambao umetupa taarifa tofauti tofauti...Tuyapime na yale yaliyotangulia tupate kuona ukweli umesimama wapi (chukulieni nyie ni - Member of the jury) ingawaje tupo hapa kijiweni..ndio raha ya mjadala au sio? - Kukubali Kutokubaliana.

Kisha sii kweli ati Mwakyembe alisema gari lake lilipindika kutokana na shimo, au amekuwa akibadilisha maneno, maelezo hayo hapo juu yanajieleza wazi kuwa mengi yaliyozungumzwa hayakutoka mdomoni mwake na ndio maana kajibu tuhuma nyingi zilizokuwa zimesambaa..mnaopinga kujieleza kwake mlitaka afanye kipi ili wananchi muamini kwamba makosa sii ya dereva wake. He is the prime witness pekee ambaye anajua kuliko sisi sote..ni victim wa ajali hii iwe makosa ya mtu yeyote - Hakuwa dereva wala hakuwa aliyesababisha ajali meaning mwenye lori.. Tuache ushabiki wakuu zangu tuache. Mwakyembe kama abiria ati alilala usingizi hivyo kusababisha ajali na blaa blaaa blaaa....hii kweli ni haki jamani?.inestigation yote inamtazama mwakyembe alikuwa ktk hali gani wakati hakuwa chonzo wala sababu ya ajali.. what a F.....

Now, kama kuna swali kuhusiana na maelezo yake haya mapya nadhani itakuwa vizuri tuyazungumze kuliko kuvuta kila hoja ya Mwakeymbe kwa sababu mengi amekuwa akijibu ama kusema baada ya uvumi kutokea..
Mwanzo ilikuwa ni ajali, tukataka kujua sababu sasa hivi imekuwa ni swala la siasa....Wengi wanajaribu kumhukumu Mwakyembe kwa sababu yake binafsi.. jamani hata Jambazio aliyekamatwa akipata ajali, hiyoajali huchunguzwa na haiwezi kuhukumiwa kutokana na mtu aliyepata ajali..Mwakyembe ana makosa tufahamisheni lakini zingatieni alichosema yeye kama statement yake...Hana historia ya kudanganya au kubadilisha maneno kisi kwamba watu waanze kutumia hoja za kuto amini statement yake kwa sababu tu hupendi Mwakyembe anavyojigamba akiwa Mbunge..
 
............Harafu huyu Mwakyembe kwa kweli mimi haziivi kabisa naye hasa alivyo nazarau kwa sisi ambao umande ulikuwa kikwazo kwetu. Maana ukijaribu kuitafsiri senteso yake unapata picha ya kwamba mtu yeyote ambaye elimu yake ipo chini ya Mwakyembe hatakiwi ku argue naye...........

Ideally Mwakyembe yuko sahihi..........lakini jambo moja anasahu society iliyomzunguka ikoje.........na hiyo society ndio inabidi impe feedback........sasa whether they make sense or not......as a Teacher Dr. anatakiwa ku-guide accordingly (na huko ndio kuonyesha kuwa elimu ina faida kwako na kwa wote).......na sio kuleta dharau nk.........
 
Hivi wakuu zangu nambieni..
Pamoja na Mwakyembe kukatazwa kutoa taarifa yoyote kuhusiana na ajali hii, hayo maelezo yake hapo juu yanatueleza kitu gani.. Cha msingi nadhani tupime maelezo yake haya baada ya kukatazwa kuingilia uchunguzi ambao umetupa taarifa tofauti tofauti...Tuyapime na yale yaliyotangulia tupate kuona ukweli umesimama wapi (chukulieni nyie ni - Member of the jury) ingawaje tupo hapa kijiweni..ndio raha ya mjadala au sio? - Kukubali Kutokubaliana.

Kisha sii kweli ati Mwakyembe alisema gari lake lilipindika kutokana na shimo, au amekuwa akibadilisha maneno, maelezo hayo hapo juu yanajieleza wazi kuwa mengi yaliyozungumzwa hayakutoka mdomoni mwake na ndio maana kajibu tuhuma nyingi zilizokuwa zimesambaa..mnaopinga kujieleza kwake mlitaka afanye kipi ili wananchi muamini kwamba makosa sii ya dereva wake. He is the prime witness pekee ambaye anajua kuliko sisi sote..ni victim wa ajali hii iwe makosa ya mtu yeyote - Hakuwa dereva wala hakuwa aliyesababisha ajali meaning mwenye lori.. Tuache ushabiki wakuu zangu tuache. Mwakyembe kama abiria ati alilala usingizi hivyo kusababisha ajali na blaa blaaa blaaa....hii kweli ni haki jamani?.inestigation yote inamtazama mwakyembe alikuwa ktk hali gani wakati hakuwa chonzo wala sababu ya ajali.. what a F.....

Now, kama kuna swali kuhusiana na maelezo yake haya mapya nadhani itakuwa vizuri tuyazungumze kuliko kuvuta kila hoja ya Mwakeymbe kwa sababu mengi amekuwa akijibu ama kusema baada ya uvumi kutokea..
Mwanzo ilikuwa ni ajali, tukataka kujua sababu sasa hivi imekuwa ni swala la siasa....Wengi wanajaribu kumhukumu Mwakyembe kwa sababu yake binafsi.. jamani hata Jambazio aliyekamatwa akipata ajali, hiyoajali huchunguzwa na haiwezi kuhukumiwa kutokana na mtu aliyepata ajali..Mwakyembe ana makosa tufahamisheni lakini zingatieni alichosema yeye kama statement yake...Hana historia ya kudanganya au kubadilisha maneno kisi kwamba watu waanze kutumia hoja za kuto amini statement yake kwa sababu tu hupendi Mwakyembe anavyojigamba akiwa Mbunge..

Sasa hiyo sentenso yake ipo sahihi kuhoji nani anayeijuwa sheria kati ya kamati na yeye? duuu kweli kazi ipo.
 
Nakupata sana mkuu ila nachojaribu kufanya ni kuwarudisha watu ktk mjadala..
Mimi nimesikia mengi sana kuhusiana na huyu jamaa na inaonyesha wazi ni ignorant fulani..Inachukiza sana na wala haipendezi lakini wapo wabunge wengi sana.. wengine wanakuchekea tu ukiwa nao ktk mazungumzo au mgeni wao.. wazuri sana wanapokuwa na shida, lakini ukianza kuuliza tu au kutaka msaada watakutolea nje vibaya sana...

Sisi UK mkuu wangu tulikuwa na mbunge mmoja tu ambaye tunamkumbuka sote alikuwa akiitwa Msonge.. Sii mama Mongela wala mzee Msekwa walikuwa watu wasiokuwa na mapungufu kama Wabunge..Lakini hainipi sababu kabisa ya kuwadharau kama binadamu..

Mimi nasema hivi Mwakyembe kama mbunge inabidi watu mfanye kazi ya ziada, siasa za Bongo ni lazima ujiweke sawasawa ktk mashambulizi na guards zako ziwe imara.. Mwakyembe hafanyi kitu chochote tofauti na Wabunge wengine..kwamba mgombea yoyote anayekupinga aua kuwa against ni ADUI..hivyo una m-treat kama adui na hii haiwezi kubadilika leo wala kesho. Waulize wabunge wote watakwambia kwamba kugombea Ubunge unajiweka ktk suluba..ni lazima ukabiriane na mengi personal, Fedha, uchawi, na mengineyo mengi ambayo ni lazima ujiunge na mtandao (syndicate) fulani.. Huna refa wala mganga watakumaliza iwe ajali au homicide yote haya ni Matakwa ya Mungu kwa tafsiri ya Mdanganyika.
Ndio maana wengine tunakaa nje kabisa bora box linaloweka mkate mezani!..
 
Wewe unaogopa nini kule Nansio maisha bomba kwani umekuja kudumu hapa duniani kufa leo ama kesho zote ni suluhu tu hakuna mshindi ,siku hizi hakuna mamba kumwalo.

Harafu nasikia siku hizi ulaya hakuna sehemu ya kuzikia ,ukifa wanakutia kiberiti wanazika tumajivu tuchache ili kakaburi kasichukue nafasi.Usiogope walozi wa uk siku hizi walishapotea rudi tukaijenge uk si bora mamba apite na wewe kuliko kutiwa kiberiti ama wewe unasema je?

Na ni heri kifo kikukute vitani kuliko kukuta kitandani ama unasema je mwanawasu?
 
...Wakati tukiendelea kubishana juu ya kama ni ajali ya kupangwa ama la naomba kusema neno moja ambalo halimlengi Mwakyembe as such bali bali namtumia kama alama tu ya ubinafsi wa wabunge wetu. Hivi mtu unatokaje Mbeya ama Makambako mko wa wawili tu kwenye gari la VX lenye uwezo wa kuchukua watu wengine watatu waliokaa comfortably? Hivi kweli hakukuna na wananchi wa kwenda Dar kutoka Mbeya ambao Mbunge ama dereva angejisumbua kidogo tu angeweza kuwapata na hivyo kuwapunguzi gharama za usafiri????? Narudia tena, Simlengi Mwakyembe bali namtumia tu kama ushahidi wa Ubinafsi wa Wabunge wetu. Msitupe Ngumi.
 
Baba Desi,,

Hilo unalosema hata kama ni la wabunge wote bado si HAKI kwa sababu hakuna mtanzania mwenye gari yake binafsi anayewachukua watu ovyo ovyo kisa kuwapunguzia gharama za usafiri

Anzia na DSM watu wangapi wanaenda makazini, anampita jirani yake ambaye anajua anaenda huko huko? Kwa nini hili liwe ajabu kwa Wabunge?

Hivi Rais na msafara wake wanachukua watu? Mimi nadhani asingeweza kufanya hivyo kwa sababu za kiusalama zaidi hata kama utashi ungekuwepo, hasa ukizingatia hali ya kisiasa inayomwandama yeye binafsi na wabunge wengine wenye misimamo kama yake ya kupinga ufisadi; pili, kwa sababu za kibima, kama abiria wakipata ajali kwenye gari lake nani angewalipa?

Lakini la muhimu, ebu mniambia kwa mlioa ulaya na marekani huwa watu wanapeana lifti?
 
MkamaP,
Mkuu sikuja kudumu hapa dunaini isipokuwa nazungumzia maswala mabyao sina haja ya kujipendekeza hata kama...Mojawapo ni siasa na pili kupigana vita..

Nawapongeza sana wenye nguvu na moyo wa kujenga inapofikia last solution ya maisha yao kuwa ktk mafungu haya hasa kwa nchi kama Tanzania.. Our Heroes leo hii ni waliopanda mlima Kilimanjaro au waliokimbiza mwenge wa Uhuru, Unakufa sii shujaa bali mshenzi fulani tu..mifano ni kwa wale waliotangulia.. Watu kama Mkwawa, Sokoine, Abraham Babu kwa Zanzibar walitakiwa kukumbukwa hata kwa siku moja lakini sio Tanzania yetu..

Nansio Poa toka Mkoloni mkuu wangu kama ulikuwa hujui. (nahisi wewe wa home) Nansio ulikuwa mji toka mkoloni na wilaya chache sana hapa Tanzania naweza kuzilinganisha nayo kwa mambo yote yanayohusiana na mji, isipokuwa tumerudi nyuma toka wabunge hawa waingie...Leo hii Ukerewe na umaarufu wake ktk Mpunga, matunda na samaki ni hadithi ambayo huwezi kuiwekea ushahidi..

Pamoja na yote haya siwezi kusimama hapa na kuanza kumchambua Mzee wangu Msekwa au mama Mongella kwa hoja ambazo hazihusiani na kilichotokea ati kwa sababu tu sikupenda uwakilishi wao.

Kuna jamaa mwingine Kamando kama umewahi msikia FMES akimsema sana, huyu tunafahamiana hadi familia zetu..Licha ya yote nani asiyeijua familia ya Mkandara pale Nansio, Ukerewe.....

Lakini nilipokutana naye nilijitambulisha, akasema hanikumbuki na hata baada ya kumfahamisha bado alinambia hanijui na he just walk away!..kama vile mimi nilikuwa nalazimisha kufahamiana naye..(baada ya kupata cheo Foreign, Ubalozi wa France).. Yet, akipata Ajali nitamtazama kama binadamu na kilichotokea kiwe sababu ya mtazamo wangu sii kuweka beef...

Kinachofanyika hapa ni beef tu na huyu jamaa...kibaya zaidi ni kwamba beef lenu linapongezwa sana na mtandao ambao wanataka pia kuona mwisho wake kwa sababu tofauti kabisa na zenu. Hivyo isije kuwa tunampoteza kiongozi wa Taifa zima kwa sababu ya matatizo ya Kyela ambayo huyo kijana wa UK anaweza kabisa kuyamaliza lakini asiweze kabisa kupambana na Mafisadi....
 
Mzee,
Hapa kula 5 kabisa kutoka kwangu. Hivi umesomea mambo ya Economic in Transport au mambo ya Ecology? Unafahamu kuwa kuna baadhi ya nchi wanatenga barabara kwa ajili ya mabasi na taxi na pia wanaongeza gari lolote lenye abiria zaidi ya 4? Unakuta hiyo lane nyeupe wakati nyingine zimebanana magari hadi unapata hamu ya kutafuta abiria kwa nguvu ili ufike haraka uendako. Hivyo, watu hutafuta kwa nguvu sehemu wanazoishi abiria (hasa wanafunzi) ambao kila siku asubuhi wanawabeba na kuwashusha mjini. Hiyo huwasaidia wao na kusaida wengie na wakati huohuo, wanapunguza msongamano wa magari na kupunguza kuchoma mafuta na makelele.

Miaka ya 90 nilikuja kujua kuwa German walikuwa na utaratibu wa kwenda kujiandikisha kama unataka kwenda nchi fulani. Badala ya kusimama na kibao barabarani na kuonyesha kidole na mwiso unabebwa/unabeba jamaa hulifahamu na kuishia kudhurika, wao wana-organise hizo safari. Wanakutafutia abiria na siku unaondoa mnakutana na kuanza safari pamoja. Hii inafanya usisafiri peke yako na ni safe kwani wote mnaacha data zenu na pia kupunguza gharama kwa kuchangia mafuta.

Sijui kwa Tanzania huu utaratibu unawezekanaje. Ila kama ofisi ya mbunge wilayani ikiwa ina organise, nafikiri inawezekana kwani itakuwa inajulikana mapema, abiria zake wako wapi.

Babadesi/Mods, naomba ikibidi hii muifungulie thread yake peke yake ili ikiwezekana, huu utaratibu uanze walau kwa mkoa wa Dar, watu wawe wanabeba vitoto vya shule. Unakuta mtu anaenda Posta, ndani ya shangingi, PEKEEE YAKE!!! Too Sad.
 
Kidogo ukisoma maelezo yangu hapo juu, ninapisha na wewe. Hiki kitu kinawezekana kabisa na usalama ukawepo. Kwani wakati anaenda kuwaomba kura, hao RAIA WAOVU wanaoweza kumdhuru kipindi hicho huwa wameenda likizo? Akishinda ubunge tu, basi jamaa wanaanza kazi ya kumsaka wamdhuru.
Pia Babadesi anazungumzia IN-GENERAL. Nchi nyingine wanafanya hili kwa mafanikio makubwa. Amini usiamini, kama wangelijenga barabara pale Dar na kutenga lane moja kwa ajili ya mabasi, taxi na magari yenye abiria zaidi ya 4, shangingi zote zingelijaa hadi ukashangaa. Ningelikuwa na uwezo, ningelifanya hili kwa kutumia mifano live.
 
Hee imekuwa tena swala la kuchukua abiria wengine.. jamani.. mwee hawa abiria wangekufa ktk ajali hiyo si mngetaka Mwakyembe ajiuzuru...kasababisha, uzembe na matumizi mabaya ya mali ya Umma,....Kwa nini kachukua abiria!..yaani hamkosi jambo.. Wallahi, nimechoka na Wabongo!
 
MkamaP,
Mkuu sikuja kudumu hapa dunaini isipokuwa nazungumzia maswala mabyao sina haja ya kujipendekeza hata kama...Mojawapo ni siasa na pili kupigana vita..

Nawapongeza sana wenye nguvu na moyo wa kujenga inapofikia last solution ya maisha yao kuwa ktk mafungu haya hasa kwa nchi kama Tanzania.. Our Heroes leo hii ni waliopanda mlima Kilimanjaro au waliokimbiza mwenge wa Uhuru, Unakufa sii shujaa bali mshenzi fulani tu..mifano ni kwa wale waliotangulia.. Watu kama Mkwawa, Sokoine, Abraham Babu kwa Zanzibar walitakiwa kukumbukwa hata kwa siku moja lakini sio Tanzania yetu..

Nansio Poa toka Mkoloni mkuu wangu kama ulikuwa hujui. (nahisi wewe wa home) Nansio ulikuwa mji toka mkoloni na wilaya chache sana hapa Tanzania naweza kuzilinganisha nayo kwa mambo yote yanayohusiana na mji, isipokuwa tumerudi nyuma toka wabunge hawa waingie...Leo hii Ukerewe na umaarufu wake ktk Mpunga, matunda na samaki ni hadithi ambayo huwezi kuiwekea ushahidi..

Pamoja na yote haya siwezi kusimama hapa na kuanza kumchambua Mzee wangu Msekwa au mama Mongella kwa hoja ambazo hazihusiani na kilichotokea ati kwa sababu tu sikupenda uwakilishi wao.
Kuna jamaa mwingine Kamando kama umewahi msikia FMES akimsema sana, huyu tunafahamiana hadi familia zetu..Licha ya yote nani asiyeijua familia ya Mkandara pale Nansio, Ukerewe.....
Lakini nilipokutana naye nilijitambulisha, akasema hanikumbuki na hata baada ya kumfahamisha bado alinambia hanijui na he just walk away!..kama vile mimi nilikuwa nalazimisha kufahamiana naye..(baada ya kupata cheo Foreign, Ubalozi wa France).. Yet, akipata Ajali nitamtazama kama binadamu na kilichotokea kiwe sababu ya mtazamo wangu sii kuweka beef...
Kinachofanyika hapa ni beef tu na huyu jamaa...kibaya zaidi ni kwamba beef lenu linapongezwa sana na mtandao ambao wanataka pia kuona mwisho wake kwa sababu tofauti kabisa na zenu. Hivyo isije kuwa tunampoteza kiongozi wa Taifa zima kwa sababu ya matatizo ya Kyela ambayo huyo kijana wa UK anaweza kabisa kuyamaliza lakini asiweze kabisa kupambana na Mafisadi....

Huyu kamando ni arrogant sana hata mie na beef naye ,Lakini Mwakyembe ni arrogant mwingine ambaye naye mimi binafsi simpeperushii kabisa kibendera.Maana si mara ya kwanza kuhoji watu na usomi wake.

Kwani wewe ukiwa prof na mimi wa kidato cha nne utaweza niuliza kweli kati yako na mimi ni nani anayejuwa vyema 1 + 1 = ? Hapa na maana ya kuwa kunakiwango cha uelewa/mazingira ambacho hakitegemei tena elimu ya mtu bali kinategemea CORE ya watu wale kama wanacho.

Hakuna BEEF lolote na Mwakyembe ,wenye beef na Mwakyembe ni akina Lowasa na RA,mimi na yule kama watanzania tuna uhuru wetu wa kuongea ,kukosoa bila kuvunja katiba ya nchi na mimi siku zote nayaamini mawazo yangu mpaka yatakapo proof failure ndipo natambuwa hayakuwa sahihi,huwa sina tabia ya kufuata upepo.

Na kwa mlengo huohuo bado naamini Mwakyembe sio kiongozi atakayeleta mabadiliko ya akina kyela awapishe wengine ,Hizo arrogant zake aende kuwatishia students darasani ili students wapate munkali wakutishwatishwa na wao wakandamize kitabu kama yeye ili waepuke vitisho .Nemekosea homeboy?
 
Huyu kamando ni arrogant sana hata mie na beef naye ,Lakini Mwakyembe ni arrogant mwingine ambaye naye mimi binafsi simpeperushii kabisa kibendera.Maana si mara ya kwanza kuhoji watu na usomi wake.

Kwani wewe ukiwa prof na mimi wa kidato cha nne utaweza niuliza kweli kati yako na mimi ni nani anayejuwa vyema 1 + 1 = ? Hapa na maana ya kuwa kunakiwango cha uelewa/mazingira ambacho hakitegemei tena elimu ya mtu bali kinategemea CORE ya watu wale kama wanacho.

- Mkuu I beg to differ mkuu, Mwakyembe ni PhD wa sheria, sasa inapokuja masuala ya sheria yes anayo authority tena kubwa sana ya kumuuliza form four leaver yaani mkuu wa Traffic wa mkoa kama kweli ana uwezo mkubwa kuelewa sheria kuliko yeye, hii ni fact sio matusi wala kejeli,

- Na uliyoyasema kuhusu Komando, kwa kweli hayana uhusiano wowote na utendaji wake wa kazi kwa taifa, huyu amekua ni baadhi ya wananchi wachache sana wachapakazi kwa taifa letu, wasiokuwa wezi na waaminifu.

Respect.

FMEs!
 
MkamaP,
Na kwa mlengo huohuo bado naamini Mwakyembe sio kiongozi atakayeleta mabadiliko ya akina kyela awapishe wengine ,Hizo arrogant zake aende kuwatishia students darasani ili students wapate munkali wakutishwatishwa na wao wakandamize kitabu kama yeye ili waepuke vitisho .Nemekosea homeboy?
Homeboy - Yes, sasa nakukubali at last..
Mkuu shukran sana lakini hapa sii mahala pake mkuu nielewe..Anzisha mada au turudi kule kwenye siasa za Kyela.. Hii ajali mnapoiunganisha na uongozi wake mnatuvuruga kabisa..
Ni sawa na majambazi wameingia Ikulu na kumuua/kumjeruhi rais wetu na familia yake kisha watu waseme well, size yake hakuwa kiongozi mzuri!.. swala la Majambazi kuingia Ikulu na safety ya Taifa letu inatupiliwa mbali..
 
Mzee,
Hapa kula 5 kabisa kutoka kwangu. Hivi umesomea mambo ya Economic in Transport au mambo ya Ecology? Unafahamu kuwa kuna baadhi ya nchi wanatenga barabara kwa ajili ya mabasi na taxi na pia wanaongeza gari lolote lenye abiria zaidi ya 4? Unakuta hiyo lane nyeupe wakati nyingine zimebanana magari hadi unapata hamu ya kutafuta abiria kwa nguvu ili ufike haraka uendako. Hivyo, watu hutafuta kwa nguvu sehemu wanazoishi abiria (hasa wanafunzi) ambao kila siku asubuhi wanawabeba na kuwashusha mjini. Hiyo huwasaidia wao na kusaida wengie na wakati huohuo, wanapunguza msongamano wa magari na kupunguza kuchoma mafuta na makelele.

Miaka ya 90 nilikuja kujua kuwa German walikuwa na utaratibu wa kwenda kujiandikisha kama unataka kwenda nchi fulani. Badala ya kusimama na kibao barabarani na kuonyesha kidole na mwiso unabebwa/unabeba jamaa hulifahamu na kuishia kudhurika, wao wana-organise hizo safari. Wanakutafutia abiria na siku unaondoa mnakutana na kuanza safari pamoja. Hii inafanya usisafiri peke yako na ni safe kwani wote mnaacha data zenu na pia kupunguza gharama kwa kuchangia mafuta.

Sijui kwa Tanzania huu utaratibu unawezekanaje. Ila kama ofisi ya mbunge wilayani ikiwa ina organise, nafikiri inawezekana kwani itakuwa inajulikana mapema, abiria zake wako wapi.

Babadesi/Mods, naomba ikibidi hii muifungulie thread yake peke yake ili ikiwezekana, huu utaratibu uanze walau kwa mkoa wa Dar, watu wawe wanabeba vitoto vya shule. Unakuta mtu anaenda Posta, ndani ya shangingi, PEKEEE YAKE!!! Too Sad.

Mkuu kwa hili? sidhani..wenyewe wana matangazo yao, kuna bwana mmoja anaitwa FATAKI, na wamemhusisha na wakina baba wanaobeba vibinti vya shule na kisha kuwafanyia mchezo mbaya...maana yake ni kwamba itaendelea kuwa vigumu kwa wenye magari binafsi kubeba wanafunzi kwa kuhofia kuitwa mafataki!
 
Back
Top Bottom