Ajali ya Gari kwenye Service Bay

Ajali ya Gari kwenye Service Bay

Huwa hakuna kuji-race. Huwa kuna uzembe wa aina fulani. Wakati najifunza kuendesha, nilikosakosa ajali ya aina hiyo. Nilikosea. Badala ya kukanyaga brake, nikakanyaga kwenye moto. Karibu ningonge geti la TCU.
Ni kweli wakati wakujifunza gari..wengi badala ya kukanya breki wanakanyaga mafuta..
Hii niliona live ndugu yangu mmoja alijichanganya akakanyaga mafuta badala ya breki..gari lilipanda matuta kadhaa ya viazi..
 
Habari zenu wakuu
Jana jioni katika viunga vya Jiji la Arusha , Nilikuwa na jamaa yangu ametoka Dar , sasa kafanya mizunguko yake ya shughuli za kiserikali zilizomleta Arusha , kamaliza jioni nikaamua Nimepeleke pale kituo cha mafuta PANONE -NGARENARO ili amwage oil

Sasa jamaa wa pale Panone akawa anaumelekeza jamaa kuingia sehemu ya Service , ghafla tukasikia puuuuh

1. Gari ilipiga resi ya ajabu na ikagonga ukuta wa service bay

2. Airbag zikafumuka

3. Rejeta ikaaanza kuvuja

4. Bampa la mbele likapasuka
5. Kioo cha Mbele kikapata mpasuko (alama)

7. Engine, Gear box , Taa, Sight mirror hajizulika

Msaada na Maoni

1. Je airbag zinaweza kurudishiwa ?

2. Tatizo ni nini Gari kujipiga resi vile kama amekanyaga mafuta kwa nguvu

Maoni yenu wakuu
Gari gani ilikuwa hio
 
Baro baro,
Poleni kwa majanga.

Je ni airbag zote zimefumuka?

Kama ndio nimechungulia ebay kila moja ina bei yake na ukijumlisha unaweza pata kama dola 1200 kwa zote hapo bado transport na kodi....

Kama ina bima kubwa suit claim tu.
 
Kuna jamaa fundi alipewa gari abadilishe tairi then airudishe kwa mmiliki.

Kilichotokea fundi alivyoanza kuendesha gari ikajirace, gari ikaenda kugonga premio new model mpaka ile premio ikatumbukia kwenye mtaro.

Gari baada ya kugonga premio ikaenda kugonga bodaboda na abiria wake mama, yule mama akavunjika mguu.

Gari ikaenda kugonga escudo ikatoka hapo ikagonga geti la apartments za bank kuu.

Yule fundi akashuka akakimbia. Katika uchuguzi pale tukagundua kapeti ya dereva kukanyagia miguu ni la manyoya lilijikusanya likaisukuma accelerator pedal ndio chanzo cha hiyo race
Ndio shida ya automatic gearbox
 
ndomaana mm huwa nagombana sana na wanaopenda kusimama mbele ya gari kumwelekeza mtu apaki gari kwa mbele. haya mambo mm mwenyew nilishatakaga kuuwa mlinzi wa gereji. nilijichanganya badala ya kuweka breki nikaongeza wese weee! uzuri yule masai aligundua mapema aliskia ule mvumo akala kona fasta ndo ikawa pona yake ila nilifumua ule ukuta wa mbele yangu wote.
 
Hapana ndo nipo comfortable maana toka najifunza automatically ilitokea nikawa natumia miguu miwili, mmoja siwezi kutumia kabisa

Kwenye mazingira ambayo unahitajika kufanya maamuzi ya haraka sana, inaweza kukusababishia ajali.
 
Kuna jamaa fundi alipewa gari abadilishe tairi then airudishe kwa mmiliki.

Kilichotokea fundi alivyoanza kuendesha gari ikajirace, gari ikaenda kugonga premio new model mpaka ile premio ikatumbukia kwenye mtaro.

Gari baada ya kugonga premio ikaenda kugonga bodaboda na abiria wake mama, yule mama akavunjika mguu.

Gari ikaenda kugonga escudo ikatoka hapo ikagonga geti la apartments za bank kuu.

Yule fundi akashuka akakimbia. Katika uchuguzi pale tukagundua kapeti ya dereva kukanyagia miguu ni la manyoya lilijikusanya likaisukuma accelerator pedal ndio chanzo cha hiyo race
It means gari ilijiresi sana na breki zikagoma?

Au ndo jamaa alipaniki akakosa cha kufanya?
 
Back
Top Bottom