Ajali ya Kimara Stop Over kumbe kaka yangu naye alikuwepo!

Sister Abigail

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2020
Posts
2,886
Reaction score
9,088
Siku tatu hizi hajarudi anapoishi, wamemtafuta simu hapatikani, kazini kwake nao hawampati mwisho akakutwa mortuary hafai Aliopolewa akiwa tayari kaenda.

Unajua nilivyopata taarifa ya ile ajali mida ya asubuhi nilishinda siku yote najisikia hatia, mpaka nakajiuliza kwanini lakini sikupata jibu. Nikawa najisikia vibaya tu na uzito ndani yangu.

Tumekua wote, tumecheza wote, tumekula wote, moments nyingi tumeshea tukiwa karibu, tabasamu lake, ni mtu asiyejua kukasirika labda awe pissed off kwa sana, mizaha na utani wake. 30 good years tupo wote, now mwendo kaumaliza.

Mtu mnaongea mnacheka muda wote, anakwambia baadae basi kumbe ndio kwaheri. Hakujua nini kitatokea usiku ule, hakuna aliyejua ile barabara na kituo ndio njia ya uelekeo kazini. Akajikuta mmoja wa wahanga bila kutarajia. Sitamuona tena! Waliosema hakuna ajuae kesho yake hawakukosea!

Ushauri: Ishini kwa upendo sana guys, kuwa chanzo cha furaha na tabasamu kwa wote unaokutana nao. Usimdharau mtu yeyote, alienacho asie nacho wote wape heshima.

Usijivune.
Usipungukiwe upendo.
Usimsahau Mwenyezi Mungu.

Moyo wangu unauma.
 
Pole sana mkuu
Mungu akutie wepesi katika kipindi hiki kigumu
Apumzike kwa amani 🙏
 
Pole sana mkuu, Bwana awafariji kwa msiba huo

1 KOR. :15:26
Adui wa mwisho atakayebatilishwa ni mauti

Nasi tutakiuliza kifo maswali siku hiyo

1 KOR. :15:55
Ku wapi, Ewe mauti, kushinda kwako? U wapi, Ewe mauti, uchungu wako?
 
Pole sana Abigail
 
Poleni sana mkuu,
 
Nimeipata hii taarifa, nabishana na watu juzi Serikali inasema wamekufa watatu tu, watu wananiambia wamekufa wengi, leo napata taarifa mtu wangu wa karibu kabisa amefariki.

Hafai ni wakumzika kesho mapema. Nimeumia sana. Nikasema ajali niliyoiona yakupita kumbe imepita na vijana wadogo kabisa wenye ndoto zao. Pole sana na Mungu watangulie vijana wote waliopoteza maisha.
 
Pole
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…