Ajali ya mabasi kutokana na kutokujali kwa dereva? Teknolojia barabarani ni suluhisho pekee

Ajali ya mabasi kutokana na kutokujali kwa dereva? Teknolojia barabarani ni suluhisho pekee

emperor

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Posts
253
Reaction score
186
Habarini Wanajamvi wenzangu,

Gharama kubwa watanzania wanazolipa kila uchwao juu ya ajali za barabarani inaleta maswali lukuki. Pamoja na jitihafa za Jeshi la Polisi, bado kuna haja ya kama Taifa tukubali kufanya mageuzi makubwa katika matumizi ya teknolojia katika jeshi hili.

Takwimu zilizopo zinaonesha kuwa ajali hizi zinachangiwa na mwendokasi wa madereva pamoja na kutokufuata alama za usalama barabarani.

Nimekua najiuliza sana ni kwa jinsi gani madereva wanaweza lazimika kuzifuata alama hizi muhimu kwa lazima kwa sababu trafiki polisi hawezi kuwepo maeneo yote ya barabara.

Suluhisho ji moja tu; nalo ni kuwekeza katika teknolojia za usalama barabarani. Mfano kama tukiwa na camera katika maeneo yote yenye makatazo ya overtake na mwendo wa 50km/h, picha za camera zitawasiliana moja kwa moja na kanzidata za mamlaka zingine na dereva wa chombo atakuwa billed fine bila mazungumzo yoyote kwa sababu ushahidi wa picha utakuwepo. Makosa haya huwa hayana mjadala (kisheria tunayaita "per se illegal").

Chondechonde serikali watu wanakufa na tuna njia mbadala wa kutokomeza ajali hizi.

Screenshot_20240526_103904_Instagram.jpg
 
Uzuri wa technology huwa haina kupindapinda.
Hiyo technology ikianza kutumika Tanzania itapunguza ajali Kwa asilimia 75%
 
Back
Top Bottom