Ajali ya MV Nyerere: Kangi, Jenista na Kamwelwe bado Mawaziri?

Ajali ya MV Nyerere: Kangi, Jenista na Kamwelwe bado Mawaziri?

Sijui kwa nini mkuu wa nchi ameamua kutoa political stunts?

Kama angepeleka vifaa vya uokozi mapema kusingekuwa na 'KIKI ZA KISIASA'

Kama angetoa amri kwa waliosema wanasitisha tukio la uokoaji kutokana na GIZA kusingekuwa na 'KIKI ZA KISIASA'
Kupanua mdomo kusema ni rahisi, kwa akili kilema za aina hii, nadhani adhabu ya viboko ingerudishwa kwa mtu mvivu wa kufikiri kama huyu, dakika 20 kwenye maji hata 10 tu kwa asiyefahamu kuogelea ni vigumu awe mzima akiwa ndani ya maji, jinsi kivuko kilivyo hakina vyumba vya kukaa abiria useme maji hayawezi kuingia..kazi waliyokuwa nayo baada ya nusu saa tangu kivuko kipinduke ilikuwa ni kuopoa maiti, kwa nini uhatarishe usalama wa waopozi kufanya kazi usiku ilihali uwezekano wa kupata watu wazima haupo?
 
Sijakuelewa mazuzu kwa namna ipi,kama mtu unashindwa kuongea vizuri basi bora kuwa Mtulivu tu yani bora kunyamaza tu maana sipendagi Matusi hayo ni mawazo yangu nayaheshimu Mwenyewe kadri ya mtazamo Wangu
Yaani umeongea ujinga uliokithiri karne hii na kumbe wajinga hawataisha duniani na hasa Tanzania,acha tuendelee na ujinga.
 
watu hai wangeweza kuokoka usiku ule kama uokozi madhubuti ungeendelea kwa kutumia jeshi na makampuni binafs,nadhani hapa ilitakiwa busara tu ya serikali kuamrisha uokozi uendelee kwa kuweka mazingira wezeshi
Unafikiri sawa sawa kweli?? kama wananchi waliowahi eneo la tukio walianza kuopoa maiti za watu ndani ya dk 20 tangu kivuko kizame, unadhani kulikuwa na watu wa kuokoa hapo...zaidi ya wale 40 waliookolewa na watu dk 10 baada ya kivuko kupinduka hakuna tena aliyeokolewa isipokuwa yule mhandisi alikuwa kwny chemba ya injini ambako maji hayakuweza kufika, busara gani na mazingira wezeshi yapi unayoongelea???
 
Asili ya mwanadamu yeyote ni kwamba anapoongea Pumba na akapokea feedback nzuri kutoka kwa wanao msikiliza kinachofuata hapo ni story za mbwa kala mkate wenye blue band.

Na sijui kwanini janga hili watu wengi wanaliweka kisiasa wakati halina usiasa wowote ule. Serikali aikusababisha kivuko kile kipinduke lakini naona watu mmeona serikali ni ya kutupiwa uchafu wote wa wananchi hata kama serikali haihusiki...!!

Kwanini watanzania tatizo likitokea tuna majumba ya tafuta kwanza wa kumlaumu?
 
Ajali ya Mv Nyerere: Kangi, Jenista na Kamwelwe Bado mawaziri?

Ni masikitiko makubwa kwamba, Serikali ya wanyonge imeokoa mtu mmoja, wakati wananchi wenyewe wameweza kuokoa watu 40..... hii ni aibu kubwa sana. Watu 225 wamepoteza maisha sababu ya uzembe.

Tuache kujidanganya na mapenzi ya Mungu. Mungu katupa akili, namna ya kuzitumia ni sisi wenyewe. Huwezi kupata Habari ya ajali saa nane mchana halafu ukaitisha Kamati ya Usalama mkoa saa 11 jioni ( yaani mwendo wa Dreamliner Dar-Mwanza mara 4 ). Rais naye hakuitisha Cabinet ya dharura wala Baraza la Ulinzi na Usalama Taifa kuratibu uokoaji. Uokoaji unasitishwa sababu ya GIZA? Tukihoji mnasema tunaleta Siasa? Nonsense!

Kwa nchi zilizoendelea Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Waziri wa Ujenzi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu walitakiwa wawe wamekwishafutwa kazi au wamejiuzulu wenyewe.

Miaka 57 baada ya uhuru...Jeshi la uokozi linapoishia kuwa jeshi la UOPOZI, ni wakati wa rafiki nyangu Kangi Lugola kupumzika. Waziri Kamwelwe, Jenista na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza wanapaswa kufukuzwa kazi mara moja. Bahati mbaya sana Rais amechoka na hivyo hajali tena. Wazembe Ndio wameongoza mazishi ya ndugu zetu leo.
Sijui kwanini umeona wanasiasa tu wakati Wataalamu wamefeli sana nashangaa hujawagusa TEMESA,SUMATRA, TPA , ZIMAMOTO NA UKOAJI hizo taasisi zimeonesha udhaifu wa hali ya juu hata aje waziri gani kama hawa technical people ni wabovu hivi hapatakuwa na mabadiliko yoyote. Nenda leo ukalale ukijua hata baada ya maafa huko Ukerewe kuna meli leo Ziwa Tanganyika ime overload na hizo taasisi nilizozitaja hapo juu wana waajiriwa wao huko Kigoma.
 
Yaani umeongea ujinga uliokithiri karne hii na kumbe wajinga hawataisha duniani na hasa Tanzania,acha tuendelee na ujinga.
Hii ni jamii forum,sipo humu kushinda na na mtu Bali kuchangia mawazo yangu na mtu akibisha Basi arumie hoja sio kutoa matusi wanajamii wengine waone haya mdomo ni Mali yako tukana uwezavyo

Marusi yako hayo hayanipunguzii kitu wala huniongezei kitu sana sana nikupe pole sana huenda kwenu ndo huwa wanakutegemea kutoa ushauri,wape pole ndugu zako, kizazi cha ajabu hiki
 
Hakuna wa kumzuru huyu, lakini anachokifanya ni kutumia huu msiba kuiprovoke Serikali ili aakamatwe and it is for his own gain, political stunts, and nothing else, vijana wa umri wake Europe wapo busy kubuni vitu vya msingi kwa ajiri ya Nchi zao, yeye yupo busy kuitumia elimu yake na akili yake kupigania Maslahi ya tumbo lake!
Lakini unajua kuwa anaishia kugain hiyo political stunt kwenye mtandao huku yeye ni looser in total maana vijana wamejikita kwenye siasa wasizofaidika nazo
 
Hakuna wa kumzuru huyu, lakini anachokifanya ni kutumia huu msiba kuiprovoke Serikali ili aakamatwe and it is for his own gain, political stunts, and nothing else, vijana wa umri wake Europe wapo busy kubuni vitu vya msingi kwa ajiri ya Nchi zao, yeye yupo busy kuitumia elimu yake na akili yake kupigania Maslahi ya tumbo lake!
akili yako ipo sawa na huyo aliyepo kwenye picha yako.

Katika yote aliyoeleza zito hapo kuna jambo lolote la uongo? Kuna la kutunga?
Pathetic Tanzanian
 
kajekudya unachoongea haupo sawa kama unakumbuka Mbunge wa eneo lile alizungumza kuomba msaada wa kupewa kivuko kipya muda si mrefu ingawaje yeye ni mtoa maamuzi hana uwezo wa kutoa maamuzi ya kununua kivuko harafu fikirisha ubongo zaidi wahusika katika kutoa maamuzi ndio hao wanasitisha kuokoa kisa Giza nani mwingine atakaeruhusu uokoaji hapo...mambo ya ajali yanatakiwa yajadiliwe na wataalamu sio kila mtu ndio maana wanasitisha uokoaji kwa kuwa hakuna wataalamu wa uokoaji...
mkuu huenda serikali ilishaweka kwenye mpango lakini ilivyoenda kwenye kikao cha wabunge wa ccm wakaondoa kwa vile ni jimbo la upinzani kama anavyosema lusinde kila siku . ccm mungu anawaona. yaani kodi mkusanye kote bila kujali vyama halafu kutumia msipeleke kote.
 
Hakuna wa kumzuru huyu, lakini anachokifanya ni kutumia huu msiba kuiprovoke Serikali ili aakamatwe and it is for his own gain, political stunts, and nothing else, vijana wa umri wake Europe wapo busy kubuni vitu vya msingi kwa ajiri ya Nchi zao, yeye yupo busy kuitumia elimu yake na akili yake kupigania Maslahi ya tumbo lake!

Utetezi wa kijinga sana, serekali inakusanya nauli ya abiria zaidi ya 101 wanaopaswa kuwepo chomboni, ww unasema Zitto anapigania tumbo lake!?
 
Nashukuru wananchi tumeanza kulitambua hili. Jamaa anafanya kila awezalo akamatwe.
Alafu pia inafurahisha anadai uhuru wa kujieleza umebanwa.
serikali ikimkamata nitashangaa sana. hoja za wanasiasa hazijibiwi kwa kukamatwa zinajibiwa kwa hoja. polis washughulike na uhalifu uliodhahiri na sio kukamata wapinzani wa ccm.
 
Hakuna hoja ya msingi

Nahodha kamkabidhi Chombo day worker Waziri anahusikaje?
Hata Yeye Zitto Basi angejiuzulu Kwa Matokeo ya chama chake 2015

Ina maana waziri alikuwa hajui kivuko kilikuwa kinakusanya pato kubwa kuliko abiria 101 per trip? Hivi serekali inaona kabisa hela inaongia nyingi kuliko inavyopaswa haijiulizi tu na kuchukus hatua? Hapa serekali inachomokaje kwa mfano?
 
Wanapata mapato makubwa kuliko ukubwa wa kivuko miaka yote wapo kimya imetokea ajali eti serikali nayo inastuka ni waongo wakubwa Mungu anawaona kwa mnayotenda,Mbunge kaongea mbele ya Spika,Waziri Mkuu,Waziri wa mambo ya ndani wote hawakuchukua hatua leo mnajifanya kusikitika nasi wakati ninyi ndio mngeweza kuzuia kwa kupeleka kivuko kipya au kufanya matengenezo ya ukweli sio kupitisha tuu...
 
Hakuna hoja fikirishi hapa zaidi ya kutugeuza sisi wajinga, Huyu "Mpelesi" ni Mbunge, Kiongozi kila kitu anachofanya ni kwa Kodi yetu hata hii posti aliyotuma ametumia Kodi zetu, narudia Zitto ni Kiongozi Kama walivyo hao anaowataka wajiuzuru, ni ujinga kutuaminisha eti they are not part of this simply because they are from opposition, ukweli unabaki wote ni viongozi, Kama ni serikali imekwama yeye hawezi kujiondoa, unless otherwise aje hapa atueleze kwanini analipwa mshahara na Serikali!
Hii ni personal attack akili mufilisi .badala ya kujadili hoja iliyo tolewa na Zito .hivi mtu utakufa ukijibu hoja kwa hoja !!?? Yaani sijui shetani gani katujazia ghafla malembukeni tz [emoji12] [emoji12] [emoji12]
 
1, Na swali ile ajari ya Moto iliyotokea kwenye ile nnchi ya ulaya mawazili walijiuzuru? Au mamlaka husika inayosimamia?
2, Jitaidi utumie ujana wako kama kweli unawapenda Watanzania vijana waweze kupata fursa za ajira au buni kitu cha msingi umekaa attention mda wote kukosoa ni sawa na unajikita kutafuta mabaya ya mwenzio kwa staili hii tutafika? Ndo maana wabongo wamtoendelea
3, waliosababisha ajali ni Mawazili? au mamlaka husika ndo washughulikiwe?Aseee kuwa Makini
Hizo ni siasa tu,hamna kitu
Moto watu waliokolewa mapema ataa waliokufa ni uzembe wao .na pili kuzidisha abiria wizi mkubwa na mbaya zaidi meli ya serikali inafananaje na moto !!???
 
Hakuna wa kumzuru huyu, lakini anachokifanya ni kutumia huu msiba kuiprovoke Serikali ili aakamatwe and it is for his own gain, political stunts, and nothing else, vijana wa umri wake Europe wapo busy kubuni vitu vya msingi kwa ajiri ya Nchi zao, yeye yupo busy kuitumia elimu yake na akili yake kupigania Maslahi ya tumbo lake!
Wewe umebuni nn au ni understanding 17
 
Back
Top Bottom