Ajali ya MV Nyerere: Kangi, Jenista na Kamwelwe bado Mawaziri?

Ajali ya MV Nyerere: Kangi, Jenista na Kamwelwe bado Mawaziri?

Ewe ndugu (kwa heshima nyingi nilizo nazo sitakuita Mpumbavu), kwani wewe unatumia muda wako kufanya nini? Zitto ameifanyia nchi hii mambo makubwa kuliko Magufuli...sasa ulitaka asihoji?

Kwamba kwako wewe serikali kuokoa mtu 1 kati ya 40 waliookolewa ni sahihi? Serikali imeamka siku ya 2 kwenda kuopoa maiti ziwani baada ya kulala usiku wa siku ya tukio kwa madai ni GIZA, na Rais wenu alijulishwa kuwa ni GIZA akakubali kwa sababu yeye ni Jiwe na ana moyo wa Jiwe...sasa Zitto akihoji na kuelekeza mnanuna? Kuweni na maarifa hakuna atakayewazonga!
Zitto ametaja watu wanaotakiwa kujiuzuru kutokana na tatzo, my point ni kuwa Zitto Hana tofauti nao wote no viongozi wanaolipwa kwa Kodi zake hivyo Kama anavyotaka wawajibike yeye pia hawezi kukwepa kwakuwa ni matatizo yametokea ndani ya serikali ambaye yeye Kama Kiongozi ni sehemu! Kitu kigumu kwako ni nini bingwa mbona watu mna vichwa vigumu!
 
Ewe ndugu (kwa heshima nyingi nilizo nazo sitakuita Mpumbavu), kwani wewe unatumia muda wako kufanya nini? Zitto ameifanyia nchi hii mambo makubwa kuliko Magufuli...sasa ulitaka asihoji?

Kwamba kwako wewe serikali kuokoa mtu 1 kati ya 40 waliookolewa ni sahihi? Serikali imeamka siku ya 2 kwenda kuopoa maiti ziwani baada ya kulala usiku wa siku ya tukio kwa madai ni GIZA, na Rais wenu alijulishwa kuwa ni GIZA akakubali kwa sababu yeye ni Jiwe na ana moyo wa Jiwe...sasa Zitto akihoji na kuelekeza mnanuna? Kuweni na maarifa hakuna atakayewazonga!
Nyie watu mnapoandika mnafikiri sawa sawa kweli!! ndani ya dakika 20 tangu kivuko kipinduke wananchi waliowahi kwenye tukio walishaanza kutoa maiti, hao 40 waliookolewa na wananchi ni wale walianguka kwenye maji pasipo kufunikwa na kivuko..ndivyo wanavyosema wenyewe, ni mpumba.vu na punguani kama wewe anayedhani kulikuwa na watu wazima baada ya nusu saa kupita waliofunikwa na kivuko wangeokolewa..ishu ya kuendelea na kuopoa maiti usiku na kuhatarisha usalama wa waopoaji haikuwa lazima zaidi ya kusubiri kuchwe kazi ya kuopoa maiti iendelee..hizo akili za kukariri kama kasuku kila anachosema zitto ni ulemavu wa akili.
 
Basi tena! kama taharifa walikuwa nazo muda mrefu! kutokujali na kutokukumbuka waliko toka ndio maana wao wanajiona watu lakini wengine wanyama!
 
hatuna jeshi la uokoaji wa majini na sidhani kama tutakuwa nalo inashangaza sana ukiambiwa kuna jeshi la uokoaji ila halina kambi maeneo ya maji kama vile visiwani. aibu sana ila ukisema wasiojulikana utawaj.,.,.,
 
Hakuna wa kumzuru huyu, lakini anachokifanya ni kutumia huu msiba kuiprovoke Serikali ili aakamatwe and it is for his own gain, political stunts, and nothing else, vijana wa umri wake Europe wapo busy kubuni vitu vya msingi kwa ajiri ya Nchi zao, yeye yupo busy kuitumia elimu yake na akili yake kupigania Maslahi ya tumbo lake!

Halafu ukimkamata umwambie umemkamata kwa kosa gani?

Kwa "provocation?". Unaelewa maana ya ku - provoke wewe?

There's no provocation there. Hapo kuna ukweli unlesss serikali iseme otherwise. Hata hivyo sina hakika kinyume chake itqkuwaje rofauti na ukweli huu ambao kila mtu anauona, ameuona;

Kwamba iseme;

1. Si kweli kuwa yenyewe kwa kutumia nyenzo zake haijaokoa mtu mmoja tu na wengine kuokolewa na mitumbwi ya wavuvi!?

2. Si kweli, RC aliitisha BLU - Mkoa immediately baada ya kupata taarifa ya ajali!!?

3. Si kweli kuwa, Rais to the present time hajaitisha BLU Taifa wala Cabinet ya dharura.?

4. Si kweli kuwa, Jenista, Kangi na Kamwelwe hawajafukuzwa/jiuzulu. Wameshawajibika kwa hatua hizo!?

Halafu, wakati huohuo tujue kuwa mtu kutumia uhuru wake kutoa maoni si kosa kisheria so long as maoni hayavunji sharia yoyote mfano kutukana nk?

Sasa wewe unaingiza issue ya ku - provoke, kivipi na kwa namna gani?

Viongozi lazima wafahamu kuwa wanaongoza watu siyo miti ama mawe. Wakifanya vyema watapongezwa. Lakini kunapokuwa na makosa, lazima pia wakosolewe!

Ukosoaji unafanyika kwa watu kutumia midomo yao. Tatizo liko wapi kwani?
 
Mpaka sasa sijaona hata zile Amphibious Boats wanazotumia wenzetu kwenye majanga kama haya, inawezekana hatujawa na uwezo wa kuzinunua?
Sisi tuna hela za kurudia chaguzi ili kuunga mkono "upumbavu" unaoitwa juhudi za raisi. Wenzangu na mimi hasa wafuasi wa ccm tunaona ni sawa kisa maslahi yetu binafsi
 
Ajali ya Mv Nyerere: Kangi, Jenista na Kamwelwe Bado mawaziri?

Ni masikitiko makubwa kwamba, Serikali ya wanyonge imeokoa mtu mmoja, wakati wananchi wenyewe wameweza kuokoa watu 40..... hii ni aibu kubwa sana. Watu 225 wamepoteza maisha sababu ya uzembe.

Tuache kujidanganya na mapenzi ya Mungu. Mungu katupa akili, namna ya kuzitumia ni sisi wenyewe. Huwezi kupata Habari ya ajali saa nane mchana halafu ukaitisha Kamati ya Usalama mkoa saa 11 jioni ( yaani mwendo wa Dreamliner Dar-Mwanza mara 4 ). Rais naye hakuitisha Cabinet ya dharura wala Baraza la Ulinzi na Usalama Taifa kuratibu uokoaji. Uokoaji unasitishwa sababu ya GIZA? Tukihoji mnasema tunaleta Siasa? Nonsense!

Kwa nchi zilizoendelea Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Waziri wa Ujenzi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu walitakiwa wawe wamekwishafutwa kazi au wamejiuzulu wenyewe.

Miaka 57 baada ya uhuru...Jeshi la uokozi linapoishia kuwa jeshi la UOPOZI, ni wakati wa rafiki nyangu Kangi Lugola kupumzika. Waziri Kamwelwe, Jenista na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza wanapaswa kufukuzwa kazi mara moja. Bahati mbaya sana Rais amechoka na hivyo hajali tena. Wazembe Ndio wameongoza mazishi ya ndugu zetu leo.
Tulijua mtaitumia hii kama kick ya kisiasa.Hivi Dereva wa Ferry ajisahau akiwa anachezea simu apitilize kidogo,halafu Ferry ipinduke Waziri ajiuzulu?So Rais naye ajiuzulu?Hivi kwa jinsi hii kuna kiongozi wa ngazi za huu atabaki,maana wafanyakazi wa chini wanavurunda kila kukicha.Hapana, mimi nadhani wale wanaohusika na hii case moja kwa moja ndio wawajibishwe.Tuishie wapi ni swala la kuangalia chains of command.
 
Mkuu zzk, wanasema "unaleta siasa" ni kwamba wanaogopa reaction ya mhe asije akawatumbua; wewe umefikisha UJUMBE na wengine pia tumekuelewa, big up brother.
 
Tulijua mtaitumia hii kama kick ya kisiasa.Hivi Dereva wa Ferry ajisahau akiwa anachezea simu apitilize kidogo,halafu Ferry ipinduke Waziri ajiuzulu?So Rais naye ajiuzulu?Hivi kwa jinsi hii kuna kiongozi wa ngazi za huu atabaki,maana wafanyakazi wa chini wanavurunda kila kukicha.Hapana, mimi nadhani wale wanaohusika na hii case moja kwa moja ndio wawajibishwe.Tuishie wapi ni swala la kuangalia chains of command.
Hata kama huwezi kufikiria vizuri lakini usidanganye wengine; soma tena UZI. Kasema, "ajali imetokea saa 8 mchana, kikao cha uokoaji kimeitishwa saa 11" na pia serikali imeokoa mtu mmoja (may be baada ya kikao kukaa) wakati wananchi wameokoa watu 40. Hapo captain anaingiaje? Tumia akili kufikiri
 
Ajali ingetokea bila Captain kufanya madudu mkuu?Na kwa nini mnasahau kwamba kuna mobilization tena probably of limited resources?Na kwa nini pia mnasahau kwamba JPM ameridhi system iliyo oza, which he is trying to put together na bado mnampigia makelele ya dictator huyo dictator huyo.To me,wamefanya vizuri under the circumstances.Najua CCM huko nyuma ilifanya vibaya,na I am sure hizi ni remnants of that nonsense.Tuwape muda,watu watanyooka na haya yatakuwa historia.
 
Hakuna wa kumzuru huyu, lakini anachokifanya ni kutumia huu msiba kuiprovoke Serikali ili aakamatwe and it is for his own gain, political stunts, and nothing else, vijana wa umri wake Europe wapo busy kubuni vitu vya msingi kwa ajiri ya Nchi zao, yeye yupo busy kuitumia elimu yake na akili yake kupigania Maslahi ya tumbo lake!
Kwa hiyo wewe unaona sawa tu kusitisha uokoaji mapema vile halafu siku mbili mbele anaokolewa mtu akiwa hai. Nyie akili zenu mnazijua wenyewe. Bahati mbaya mmepewa Kaya.
 
Kwa hiyo wewe unaona sawa tu kusitisha uokoaji mapema vile halafu siku mbili mbele anaokolewa mtu akiwa hai. Nyie akili zenu mnazijua wenyewe. Bahati mbaya mmepewa Kaya.
Kitu kimoja nilichogundua, hii comment imewagusa kunako!
 
Mfano wako ni wa kijinga Sana, Zitto Kabwe ni Kiongozi wa Serikali Kama hao anaowataka wajiuzuru, aanze yeye kujiuzuru kwa sababu Kama serikali imefeli kwa Hili na yeye ni sehemu ya serikali, Zitto no Kiongozi kwenye level ya decision makers Hana tofauti na hao anaotaka wajiuzuru!
Mzee kuna tofauti kati ya kiongozi wa umma, mtumishi wa umma, viongozi wa serikali etc. Huyo wa kuchaguliwa atajiuzulu vipi sasa au amekuwa kina waitara ?
 
Mzee kuna tofauti kati ya kiongozi wa umma, mtumishi wa umma, viongozi wa serikali etc. Huyo wa kuchaguliwa atajiuzulu vipi sasa au amekuwa kina waitara ?
Amechaguliwa akawe Nani, hizo pesa anazipwa na Serikali anapewa kwa sababu gani, unaweza kujibu hilo mkuu!
 
Amechaguliwa akawe Nani, hizo pesa anazipwa na Serikali anapewa kwa sababu gani, unaweza kujibu hilo mkuu!
Anawawakilisha wanajimbo wenzake kwenye tawi tendaji(serikali) ambalo lina waliopewa mamlaka ya ziada ya kutenda(wateuliwa) kwa mujibu wa katiba.
 
Mkuu Zitto muonee huruma Mzee kamwelwe anakesha siku ya 5 leo kwa umri ule sio inshu ndogo
 
Anawawakilisha wanajimbo wenzake kwenye tawi tendaji(serikali) ambalo lina waliopewa mamlaka ya ziada ya kutenda(wateuliwa) kwa mujibu wa katiba.
Ni Kiongozi si kiongozi!?
 
Tena wanapongezwa kwa kufanikisha zoez la kutoa kafara.
20180924_204011.jpg
 
Kama kuna vijana 3 nchini wenye uwezo wa kuongoza nchi hii kwa ufanisi wa juu sana, ZITTO KABWE ni lazima atakuwa mmoja wapo. Sifa kubwa ya Mh Zitto ni kuja na njia mbadala pale anapokumbwa na matatizo makubwa sana. Kwa mfano, Ni wanasiasa wachache sana walipanda juu tena kisiasa pindi walipofukuzwa katika vyama vyao kama alivyopanda chati Zitto. Wengi huishia kupiga magoti kwa mabwana zao mpaka wawarudishe huko walikotupwa bila kuwa na msimamo wa kile walichokiamini na kukipigania. Zitto kafanya hivyo toka CHADEMA MPAKA ACT.

Kila mtanzania yupo huru kuitathimini ajali iliyotokea kwa uwezo wake wote, si tu kwa vile tumezoea kulalamika na kulaumu, bali ni kwa sababu tunajua fika kuwa yaliyotoke huko Viktoria yanaweza kutokea Ziwa Tanganyika, Nyasa, kigamboni na katika ziwa lolote jingine. Kwanini tusubiri au tufungwe midomo mpaka serikali ije kutudanganya. Tuna haki ya kuhoji bila kumuogopa komike Lugola.

Zitto kaja na hoja ya msingi, kwa vile Rais kavunja bodi ya TEMESA, na baadhi ya viongozi wa chini. Swali kubwa lilikuwa je mawaziri husika bado wanakalia viti vyao au Rais kashachoka kutumbua? Hili ni swali la msingi sana kwa sababu swala la kivuko hicho lilifika bungeni huku waziri husika aliombwa kutoa jibu. Kwanini tusimuulize au Rais asimuulize kama matatizo hayo aliyatatua?

Nawaomba wasomaji wote mliopitia uzi huu, usomeni kwa kutulia na jaribuni kupanua akili zetu nje ya upenzi na ushabiki wa vyama. Ushabiki kwenye vifo haufai, wala kutumia nguvu zote kumsifia Raisi Magufuli nayo si dawa.

Kumbukeni tatizo la TANZANIA NI UONGOZI, ANZENI KWA KUJIKITA HAPO.
 
Back
Top Bottom