Ajali ya Mwendokasi yaua eneo la Urafiki

Msanii

Platinum Member
Joined
Jul 4, 2007
Posts
25,252
Reaction score
36,513
Muda huu saa mbili ahsubuhi tarehe 11 June 2024, nimepita eneo la Urafiki jirani na Shekilango nikiwa ktk Mwendokasi kwenda Kimara, basi nililopanda lilipofika mataa ya Urafiki limechepuka kutoka njia yake na kupita barabara ya kawaida. Tumeenda mbele tunaona kuna umati ktk brbr ya mwendokasi usawa wa depo ya Kilimanjaro Express. Katikati umelala mwili wa binadamu mwenzetu. (RIP)

Tulipokuwa tunakatizi hapo, washuhuda wa ajali wanasema marehemu amegongwa na mwendokasi alipokuwa anavuka. Wanaenda mbali zaidi kumfokea dereva wetu kuwa wamezoea kuua watembea kwa miguu hivyo nao watajitwalia sheria mkononi.

Kwa kumsitiri marehemu, sikupiga picha ya ajali hiyo. Team Picha mtanisamehe

MY TAKE
Iwezekane njia ya mwendokasi iwekewe uzio watu wasivuke hadi kwenye zebra crossing. Nasema hayo kwa sababu madereva wa mwendokasi ni kama wana kinga dhidi ya makosa ya usalama barabarani.

Mwendokasi ya Mbagala itakapoanza tutakuwa na simanzi tele kwa ajali zitakazojiri

Ee Mungu tusaidie
 
Hiyo njiaa ilitakiwa iwekwe uzio koteee,kuzuia wavukaji wanajivukia sehemu holela
Mradi huo kuna mambo kibao bado yalikuwa hajakamilika

Ova
 
Kwanini isitolewe elimu tu badala ya kuingia gharama ya kutengeneza vituko.

Hivi maeneo kama Makongo kuna uzio kwenye bustani?, mbona watu wana adabu. Au huku kwingine ni kiburi, ujuaji na mazoea.
 
Back
Top Bottom