Ajali ya Mwendokasi yaua eneo la Urafiki

Ajali ya Mwendokasi yaua eneo la Urafiki

Hata hii Sgt tunayoitegemea Haina fense tutegemee vifo vya wanadamu na mifugo hasa Kwa sie wagogo lkn ni muhimu watu lazima wafe ili wengine wajifunze maendeleo yoyote Yana changamoto mfano uingiaji wa pikipiki za kichina vifo vimekuwa vingi mnoooo lkn kabla ya kuwepo Kwa pikipiki hizo vifo kama Israel alikuwa likizo
 
Pamoja na kua dereva wa mwendokasi anaweza kua na makosa ila na watembea kwa miguu hua ni viburi sana sometimes.

Mtu anavuka kwa madoido as if ana ubia za vyombo vya moto, hata kama upo kwenye zebra we chapa raba chap uvuke, hawa bodaboda na madereva wengi hawajielewi.
Mbaya zaidi hizi boda hazieleweki zinatokea upande gani, zinashusha au zinapanda zenyewe kotekote.

Unavuka kimadoido unashangaa chuma imekuvaa.

Ni kheri uwe chap kidogo kwenye kuvuka, vukia kwenye alama sahihi za kuvuka, usitegemee mataa na zebra ndo zikisimamishie magari. Usiache kuangalia kulia na kushoto na kuchukua tahadhari wakati wote ukiwa inavuka.
Dar watembea kwa miguu wanaogopa MVUA tuu
Mvua ikinyesha huoni mtu njian.
Viburi ndivyo vinachangia vifo na uzembe ulopitiliza pia na ulevi.
Kwan ilr elimu ya kuvuka barabara si ile ile ya
UNAANGALIA KUSHOTO
UNAANGALIA KULIA
UNAMALIZIA KUSHOTO ALAFU KAMA NI SALAMA NDO UNAVUKA?
 
Pia ukiwa dereva utakutana na hii kero.

Unakuta dereva amesimama kupisha watu wavuke lakini kuna mtu anavuka kwa kunyata ama anaandika sms.

Kuna wavukaji wanakera sana.
Ndo ivo mkuu hata tusio na magari tunayaona haya tukiwa kwenye daladala mbele pale.

Dereva kiroho safi tena sometimes hata sio kwenye zebra, kasimama mvuke unakuta jitu linavuka kwa kujivuuuta, akiambiwa vuka chap hamna zebbra hapa anaishia kutukana.
 
Sawa, ila kwanini mtu upite sehemu usiyoruhusiwa?. Muda mwingi waenda kwa miguu huwa ndio tatizo.
Nina uhakika alipogongewa huyu mtu ni sehemu yenye kingo nyembamba na haina zebra.

Ila kwa mbele kama unatokea Shekilango kwenda Urafiki kuna sehemu japo haina zebra lakini ni pana na salama kuvukia kuliko hapo alipogongewa.
 
Dar watembea kwa miguu wanaogopa MVUA tuu
Mvua ikinyesha huoni mtu njian.
Viburi ndivyo vinachangia vifo na uzembe ulopitiliza pia na ulevi.
Kwan ilr elimu ya kuvuka barabara si ile ile ya
UNAANGALIA KUSHOTO
UNAANGALIA KULIA
UNAMALIZIA KUSHOTO ALAFU KAMA NI SALAMA NDO UNAVUKA?
Hiyo elimu inafuatwa vizuri na watoto wa shule za msingi ila hawa watu wazima ni changamoto
 
Watanzania wengi ni wajuaji hasa hawa wanaoishi Dar es salaam,wengi hawavuki barabara bali wanakatisha barabara!

Kuna utofauti mkubwa kati ya KUVUKA na KUKATISHA

1.KUVUKA BARABARA- Unavuka barabara kwenye eneo maalumu lililotengwa kwa watembea kwa miguu kama kwenye Alama za watembea kwa Miguu (ZEBRA)

2.KUKATISHA BARABARA -Mtembea kwa miguu anaamua kwa makusudi kutoka upande mmoja wa barabara kwenda upande mwingine bila kuzingatia sehemu maalumu au alama zilizotengwa kwa ajili ya watembea kwa miguu.

Hiyo barabara ya mwendokasi inajitegemea na kama kuna mtu amegongwa katikati ya hiyo njia it means yeye ndiye mwenye tatizo siyo dereva aliyemgonga!

Ifike sehemu watanzania hasa watembea kwa miguu waheshimu na kufuata sheria/alama/Michoro ya barabarani,waache ujuaji na mazoea ya kijinga.
 
Hata mwendokasi ya Gongo la mboto itakapoanza itakua vilio na kusaga meno maana Raia hawachukui tahadhali ni kuvuka vuka tu kwa haraka ya kukimbilia magari
Wanasema wamezoea magari.Wanachoogopa Dar es salaam ni panyaroad na mvua tu.Magari wao Wala hawajali.Jana Pugu Kona Lori ilitaka kupitia na Boda Boda ikiwa na abiria nyuma Tena ni mwanamke.
 
Muda huu saa mbili ahsubuhi tarehe 11 June 2024, nimepita eneo la Urafiki jirani na Shekilango nikiwa ktk Mwendokasi kwenda Kimara, basi nililopanda lilipofika mataa ya Urafiki limechepuka kutoka njia yake na kupita barabara ya kawaida. Tumeenda mbele tunaona kuna umati ktk brbr ya mwendokasi usawa wa depo ya Kilimanjaro Express. Katikati umelala mwili wa binadamu mwenzetu. (RIP)

Tulipokuwa tunakatizi hapo, washuhuda wa ajali wanasema marehemu amegongwa na mwendokasi alipokuwa anavuka. Wanaenda mbali zaidi kumfokea dereva wetu kuwa wamezoea kuua watembea kwa miguu hivyo nao watajitwalia sheria mkononi.

Kwa kumsitiri marehemu, sikupiga picha ya ajali hiyo. Team Picha mtanisamehe


MY TAKE
Iwezekane njia ya mwendokasi iwekewe uzio watu wasivuke hadi kwenye zebra crossing. Nasema hayo kwa sababu madereva wa mwendokasi ni kama wana kinga dhidi ya makosa ya usalama barabarani.

Mwendokasi ya Mbagala itakapoanza tutakuwa na simanzi tele kwa ajali zitakazojiri

Ee Mungu tusaidie
Haraka + mawazo, Allah amsamehe zambi zake aliyetangulia!
 
Wapuuzi sana, wanajiona kama wanaendesha treni vile,kuna haja ya kuchukuliwa hatua kwa kutochukua tahadhari
kwa kweli ni wapuuzi na hawana elimu ya kutosha kuendesha magari ya mwendokasi. Kuendesha mwendokasi haina maana utimue maspeed tuu bila kujali watumiaji wengine wa barabara. Lazima uzingatie maeneo ya watumiaji wengi wa barabara.
Jaribu kufikiria umemgonga mtu (tena anayetegemewa)... sawa alikuwa na makosa, lakini wewe umesababisha kifo chake... utaishi kwa kuumia siku zako zote. Sitetei wanaoingia barabarani kimakosa lakini jitahidi wewe dereva usiwe mtu wa mwisho kukatisha uhai wao kwa uzembe wao.
 
Wanasema wamezoea magari.Wanachoogopa Dar es salaam ni panyaroad na mvua tu.Magari wao Wala hawajali.Jana Pugu Kona Lori ilitaka kupitia na Boda Boda ikiwa na abiria nyuma Tena ni mwanamke.
Tena pale kko kuanzia msimbazi
Wanavyojazana pembeni ngoja siku gari likose njiaa litawafata watu pembeni huko

Ova
 
Back
Top Bottom