Ajali ya Mwendokasi yaua eneo la Urafiki

Ajali ya Mwendokasi yaua eneo la Urafiki

Najua tupo kwenye majonzi lakini hili pia linapaswa kuongelewa, watu wa Dar hawaogopi magari wao wanaogopa matone ya mvua, mtu kabisa anaona mwendokasi inakuja anavuka tena huku anatembea, muda wote tunajitia tunaharaka hatuwezi kusubiri, tena waenda kwa miguu wengi tukiona gari tunakasumba ya "si ananiona, anigonge aone", tutaisha sana, tubadilike.
 
Sawa, ila kwanini mtu upite sehemu usiyoruhusiwa?. Muda mwingi waenda kwa miguu huwa ndio tatizo.
Tunapenda kulea ujinga. Watu wanaamua kuvuka hovyo kama mbuzi tunalaumu madereva. Manzese wameweka uzio sehemu nyingine wamevunja uzio ili wavuke kisa zebra iko 300m away. Mwendokasi akigonga mtu kwenye zebra sheria imshughulikie lakini sehemu nyingine ni ajali kama magari mengine yanavyogonga watu, Akiyumba kumkwepa huyo mtu kuna kingo za barabara akiigusa tu hio linabinuka na watu zaidi ya 100 maisha yao yatakuwa hatarini.
 
watu wasivuke hadi kwenye zebra crossing.
Hivi unafahamu kuwa madereva wa bongo hawaheshimu zebra crossing?

Madereva wa bongo Wanaheshimu matuta tu na sio zebra, pahali palipo na zebra bila matuta hao madereva hupita kwa speed ya 60 kph +

Ukijichanganya ukatia mguu wanapitia na wewe, kuanzia pale kimara mwisho hadi Kibaha hakuna tuta madereva hufanya ligi hadi kwenye traffic light hupita ilhali taa nyekundu imewaka.
 
Hiyo njiaa ilitakiwa iwekwe uzio koteee,kuzuia wavukaji wanajivukia sehemu holela
Mradi huo kuna mambo kibao bado yalikuwa hajakamilika

Ova
Sio kama nafurahia haya mauaji,lkn waswahili tunapenda sana shortcut hata kama inahatarisha maisha yetu,pale Mbezi mwisho umewekwa uzio ili watu wapite kule juu darajani lkn wameukata ili wapite pale ambapo sasa hivi hakuna zebra.tutagongwa sana kwa uswahili wetu huu.
 
Back
Top Bottom