Ajali ya Mwendokasi yaua eneo la Urafiki

Ajali ya Mwendokasi yaua eneo la Urafiki

Muda huu saa mbili ahsubuhi tarehe 11 June 2024, nimepita eneo la Urafiki jirani na Shekilango nikiwa ktk Mwendokasi kwenda Kimara, basi nililopanda lilipofika mataa ya Urafiki limechepuka kutoka njia yake na kupita barabara ya kawaida. Tumeenda mbele tunaona kuna umati ktk brbr ya mwendokasi usawa wa depo ya Kilimanjaro Express. Katikati umelala mwili wa binadamu mwenzetu. (RIP)

Tulipokuwa tunakatizi hapo, washuhuda wa ajali wanasema marehemu amegongwa na mwendokasi alipokuwa anavuka. Wanaenda mbali zaidi kumfokea dereva wetu kuwa wamezoea kuua watembea kwa miguu hivyo nao watajitwalia sheria mkononi.

Kwa kumsitiri marehemu, sikupiga picha ya ajali hiyo. Team Picha mtanisamehe

MY TAKE
Iwezekane njia ya mwendokasi iwekewe uzio watu wasivuke hadi kwenye zebra crossing. Nasema hayo kwa sababu madereva wa mwendokasi ni kama wana kinga dhidi ya makosa ya usalama barabarani.

Mwendokasi ya Mbagala itakapoanza tutakuwa na simanzi tele kwa ajali zitakazojiri

Ee Mungu tusaidie
sitaisahau siku ile mchana wa saa saba maeneo ya BIAFRA KINONDONI. Niliposhuhudia BODABODA akipora uhai wa mama lishe aliyekuwa amebeba jagi la juice katikakati ya barabara ya mwendo kasi na kisha akakimbia
 
Naongelea kulinda maisha na usalama wa mtu pasi na kujali amekosea
Kutoa adhabu ya ulemavu au mauti kwa mtu kisa kaingia kwenye barabara Yako si sawa
Njia ya treni ilipaswa kuwa na closing gate Kila treni inapokaribia eneo husika ili kulinda maisha ya raia
Kuuwa bila kukusudia (ajali).
 
Mwendokasi ya Mbagala itakapoanza tutakuwa na simanzi tele kwa ajali zitakazojiri
Mstari huu tu na mimi nikawaza kama wewe Mungu atuvushe salama, Mbagala asee , subahan Allah

Ingawa kuna watu hawazingatii sheria kama taa lakini madereva wa mwendo kasi hawa fare driving
 
Mstari huu tu na mimi nikawaza kama wewe Mungu atuvushe salama, Mbagala asee , subahan Allah

Ingawa kuna watu hawazingatii sheria kama taa lakini madereva wa mwendo kasi hawa fare driving
Kwanini Mbagala?
 
Muda huu saa mbili ahsubuhi tarehe 11 June 2024, nimepita eneo la Urafiki jirani na Shekilango nikiwa ktk Mwendokasi kwenda Kimara, basi nililopanda lilipofika mataa ya Urafiki limechepuka kutoka njia yake na kupita barabara ya kawaida. Tumeenda mbele tunaona kuna umati ktk brbr ya mwendokasi usawa wa depo ya Kilimanjaro Express. Katikati umelala mwili wa binadamu mwenzetu. (RIP)

Tulipokuwa tunakatizi hapo, washuhuda wa ajali wanasema marehemu amegongwa na mwendokasi alipokuwa anavuka. Wanaenda mbali zaidi kumfokea dereva wetu kuwa wamezoea kuua watembea kwa miguu hivyo nao watajitwalia sheria mkononi.

Kwa kumsitiri marehemu, sikupiga picha ya ajali hiyo. Team Picha mtanisamehe

MY TAKE
Iwezekane njia ya mwendokasi iwekewe uzio watu wasivuke hadi kwenye zebra crossing. Nasema hayo kwa sababu madereva wa mwendokasi ni kama wana kinga dhidi ya makosa ya usalama barabarani.

Mwendokasi ya Mbagala itakapoanza tutakuwa na simanzi tele kwa ajali zitakazojiri

Ee Mungu tusaidie
Kwanza kabisa natoa pole kwa waliofikwa na msiba huu wa mpendwa wao, ila shida ni moja taa ya kijani inaweza kuwa imewaka kuruhusu magari mfano taa za yrafiki hapo then hapo usawa wa kilimanjaro bus watu wanavuka bila kuchukua taadhari kuwa taa zimeruhusu magari kupita likitokea la kutokea lawama kwa madereva japokuwa siwatetei sana maana nao kwa kuvunja sheria hawajambo ila watumiaji wote wa barabara tukizingatia sheria tutapunguza haya madhara na hata vifo.
 
Kwanini Mbagala?
Geography ilivyo watu wengi kuvuka Yani Mbagala hasa rangi 3 inataka kufanana na kariakoo, changamoto ni kuwa Mbagala ni makazi hivyo wanaovuka ikiwemo watoto ni wengi
 
Uzio wa nini? Watu wanapita kwenye flyover hapa Ubungo wakitokea University Rd waamie upande wa pili na kuna uzio. Tunahitaji elimu na kustaarabika tu.
Tena waling'oa hapo, kama buguruni wanavopita katikati ya vile vyuma
 
Geography ilivyo watu wengi kuvuka Yani Mbagala hasa rangi 3 inataka kufanana na kariakoo, changamoto ni kuwa Mbagala ni makazi hivyo wanaovuka ikiwemo watoto ni wengi
Ruti Mbagala sehemu yenye watu wengi ndio hio rangi tatu na ni mwisho wa ruti hivyo hayo mabasi hayatakuwa na speed kubwa. Kuanzia Gerezani,Kivukoni mpaka Saba saba hakuna watu wa kuvuka barabarani isipokuwa wachache sana ni maeneo ya viwanda. Kuanzia kwa Azizi Ali ndio kuko busy na hapakaribii Rangi Tatu. Ila hio njia ya Kimara kuanzia Mbezi hadi Fire kuko busy watu wengi sana wanavuka hio barabara. Kwa kifupi hio ya Kimara ni hatari kuliko ya Mbagala.
 
Unakuta raia anajiamni kabisa anasimama kwenye kingo za vitofali vinavyotofautisha mwendo kasi na barabara ya kawaida kitu ambacho ni hatari sana
 
Kwanini isitolewe elimu tu badala ya kuingia gharama ya kutengeneza vituko.

Hivi maeneo kama Makongo kuna uzio kwenye bustani?, mbona watu wana adabu. Au huku kwingine ni kiburi, ujuaji na mazoea.
Mifumo na mamlaka vimepigwa na stroke
 
Watanzania wengi ni wajuaji hasa hawa wanaoishi Dar es salaam,wengi hawavuki barabara bali wanakatisha barabara!

Kuna utofauti mkubwa kati ya KUVUKA na KUKATISHA

1.KUVUKA BARABARA- Unavuka barabara kwenye eneo maalumu lililotengwa kwa watembea kwa miguu kama kwenye Alama za watembea kwa Miguu (ZEBRA)

2.KUKATISHA BARABARA -Mtembea kwa miguu anaamua kwa makusudi kutoka upande mmoja wa barabara kwenda upande mwingine bila kuzingatia sehemu maalumu au alama zilizotengwa kwa ajili ya watembea kwa miguu.

Hiyo barabara ya mwendokasi inajitegemea na kama kuna mtu amegongwa katikati ya hiyo njia it means yeye ndiye mwenye tatizo siyo dereva aliyemgonga!

Ifike sehemu watanzania hasa watembea kwa miguu waheshimu na kufuata sheria/alama/Michoro ya barabarani,waache ujuaji na mazoea ya kijinga.
Umeandika vyema sana mkuu.
Hakaka mwenye kuelewa na aelewe
 
Dogo mwenyewe huyu bado ni Kijana mdogo alikua anapambana na duka lake la vifaa vya mabasi haya ya mikoani pale BM inasikitisha taifa likipoteza nguvukazi kama hii inayoanza kuibukia
 
Attachments

  • Screenshot_20240611-230332_WhatsAppBusiness.jpg
    Screenshot_20240611-230332_WhatsAppBusiness.jpg
    570.5 KB · Views: 2
Hata mwendokasi ya Gongo la mboto itakapoanza itakua vilio na kusaga meno maana Raia hawachukui tahadhali ni kuvuka vuka tu kwa haraka ya kukimbilia magari
Maendeleo yana gharama zake! Elimu itolewe kwa mapana zaidi!!
 
NI kweli hata sisi tulipita pale tukiwa ndani ya bajaji tukaona umati wa watu na mwili ukiwa umelala pale!
Mungu atusaidie! Siku ya kufa ni kama mtego tu.
 
Back
Top Bottom