Ajali ya ndege Bukoba ni matokeo ya uzembe na kufanya kazi kwa mazoea.Tuwajibishane ili tusirudie makosa

Ajali ya ndege Bukoba ni matokeo ya uzembe na kufanya kazi kwa mazoea.Tuwajibishane ili tusirudie makosa

Kitu anbacho sijasikia ni nafasi ya Air Traffic Controllers. Ninachojua ( niko tayari kusahihishwa) ni kuwa hawa ndio wanaotoa kibali kwa rubani kutua au kupaa kwenye uwanja wa ndege.

Hawa wanatikiwa kujua kinachoendelea kwenye kiwanja hata kama wako Mwanza maana teknoloji za siku hizi kuona kutokea mbali sio tatizo.

Aidha, nadhani kuna taa na transmitter ambazo huwa zinawekwa kwenye runway ili kuiongoza ndege kama haionekani.

Amandla...
 
Afadhar mleta uzi amekuja kiweredi!
Ila watanzania kuna mifumo yetu ya ufikiri haifanyi kazi vizuri. Tunahitaji overhaul!
HAIWEZEKANI KATIKA AJARI HII TUKAJIKITA KWA SUALA LA MAJALIWA NA MLANGO NA KUACHA MAMBO YA MSINGI ILI ISIJIRUDIE TENA! na KUWAJIBISHANA...
Big Up for your Clear and short but educative Comments!
 
Kitu anbacho sijasikia ni nafasi ya Air Traffic Controllers. Ninachojua ( niko tayari kusahihishwa) ni kuwa hawa ndio wanaotoa kibali kwa rubani kutua au kupaa kwenye uwanja wa ndege.

Hawa wanatikiwa kujua kinachoendelea kwenye kiwanja hata kama wako Mwanza maana teknoloji za siku hizi kuona kutokea mbali sio tatizo.

Aidha, nadhani kuna taa na transmitter ambazo huwa zinawekwa kwenye runway ili kuiongoza ndege kama haionekani.

Amandla...
Hizo taa sio kwa Category ya kiwanja cha BK...ndio maana kipo Category 3C
 
Hizo taa sio kwa Category ya kiwanja cha BK...ndio maana kipo Category 3C
Inaelekea uko fixated na Categories. Vinavyowekwa kwenye category ni vitu minimum vinavyohitajika. Kwa mfano nyumba yenye ghorofa pungufu ya nne hailazimiki kuwa na lifti. Lakini kama una ulemavu (hata ka ma huna) hauzuiwi kuweka lifti( kwenye nyumba yako ya ghorofa moja. Hivyo TAA haitaadhibiwa ikiweka threshold na edge light katika uwanja cha category 3C kama cha Bukoba ambacho mara nyingi visibility ya runway ni tatizo. In fwakt wao wenyewe wanasema kama kiwanja kina historia ya low visibility ni shurti kiwekwe Touchdown Zone lights hata kama ni cha Category 3C. Viwango ni vya ujumla lakini kila wakati vinaruhusu mabadiliko katika mazingira maalum.

Amandla...
 
Yataka pia ifahamike abiria wengi waliokaa mbele walikufa on impact na wengine walikufa maji,, means,, walikua bado wamefunga mikanda tayari kwa kutua,, ndani ya sekunde kadhaa wamejikuta ndani ya maji, yaani wamezama ndani, hapo huwezi kujifungua mkanda huku pia uko majini, hupati pumzi,, kifo kilikua within one minute to three kwa maoni yangu,
Waliopona ni wale wa mkiani, maana huko ndege haikuwa imezama, japo maji yalikua yanajaa kwa speed,
Hao ndio walifanikiwa kutoka wakiwa hai,,
Ukifuatilia utaona waliopona wote walikaa seat za nyuma,,
Wavuvi walifika area within five minutes, means kama wa mbele wangekua bado hai, wangeweza kuokolewa, chumba cha rubani kilichelewa kujaa maji japo kilikuwa kimezama pia,, ndio maana rubani walichelewa kupoteza uhai kwa dakika kadhaa,,
 
Hayo mambo yote uliyoyataja ni theory tu na hayatumiki Tanzania, tungeanza na bajeti, Serikali inatenga bajeti kiasi gani kwa kikosi cha uokoaji na usalama wa wananchi hata tu kwenye huo uwanja? Meneja wa Uwanja ana bajeti kiasi gani kwa ajili ya dharura?

Serikali imetumia Mabilioni kwa ajili ya matabgazo tu ya majibu sensa.
Serikali KUU inawajibika kwa yaliyotokea kwa 100% kwani walipaswa kuokoa watu na siyo sijui vidagaa kama Meneja wa Kiwanja, shida iko kwa Kiongozi Mkuu na siyo vidagaa!

Swali langu kwako Meneja wa Uwanja ana bajeti ya kiasi gani kuweza kutoa huduma za dharura? Je, ana vifaa na manpower yenye ujuzi wa kutosha kudili na maafa?
Wameanza kutoa ajira katika jeshi la Zimamoto na Uokoaji. Kama jina lilivyo mara nyingi maamuzi yao huwa ya zimamoto tu.
 
Hawa watu wenye ujuzi na mambo ya Usimamizi wa miradi ya ndege ndio wanapewa kupewa vitengo. Lakini hapa kwetu si ajabu kukuta mtu anayesimamia viwanja vya ndege hana utaalam wowote na mambo ya ndege! Barafu mama kuonesha akupe majukumu akutoe huko uliko!

Serikali haitaki wabobezi inataka watu watu wa kuabudu na kusifu tu.
 
Hongera sana Barafu kwa ufafanuzi murua, umekata kiu yangu haya maelezo yalipaswa kuchapishwa na kubandikwa kila kona ya jiji kila Mtanzania ayasome,

Umegusia suala jema sala kuhusu Majaliwa upo sahihi uliposema wanaomponda wamekosa shukrani ni kweli sababu ushujaa wa huyo kijana ni kufika eneo la tukio na kuonesha nia ya kusaidia na matokeo yake na yeye kupata majanga akiwa katika juhudi za uokozi, wangapi wenye Moyo kama huo??? Majaliwa atabaki kua Shujaa hakuna atakayebadilisha hayo.
 
Inaelekea uko fixated na Categories. Vinavyowekwa kwenye category ni vitu minimum vinavyohitajika. Kwa mfano nyumba yenye ghorofa pungufu ya nne hailazimiki kuwa na lifti. Lakini kama una ulemavu (hata ka ma huna) hauzuiwi kuweka lifti( kwenye nyumba yako ya ghorofa moja. Hivyo TAA haitaadhibiwa ikiweka threshold na edge light katika uwanja cha category 3C kama cha Bukoba ambacho mara nyingi visibility ya runway ni tatizo. In fwakt wao wenyewe wanasema kama kiwanja kina historia ya low visibility ni shurti kiwekwe Touchdown Zone lights hata kama ni cha Category 3C. Viwango ni vya ujumla lakini kila wakati vinaruhusu mabadiliko katika mazingira maalum.

Amandla...
Sijawa na uraibu wa kategoria,nadhani nilikuwa najaribu tu kufafanua kuwa kwa BK kuwa tu hiyo kategoria maanake hizo recommended standards ulizoainisha ni ndoto.Hivyo kuwa tu ni kiwanja kinacho-operate toka mawio mpaka machweo,maanake hizo standard haina.Mengine uliyoandika ni sahihi pia...sijapinga
 
Kuokoa maisha ya abiria ni ndoto? Ukishasema recommended tayari ina maana unaweza kuongeza. Hizo taa ni za kufanya runway ionekane wakati mwanga haupo. Sasa kama kiwanja kinakawaida ya kuwa na fog kiasi kuwa hakionekani utakataa kuweka taa kwa sababu tu haulazimiki? Unaona bora uwekeze kwenye mavieti kuliko vitu ambavyo vinaweza kuokoa maisha? Kwa bahati mbaya mawazo kama hayo ndio yanatawala. Maisha kwetu hayana thamani.

Mkuu mbona unaongea na mimi kama ndio mwenye dhamana na mamlaka?Punguza munkali...Sihusiki kwa lolote katika kutoa maamuzi.Hapa tunabadilishana tu mawazo
 
Mkuu mbona unaongea na mimi kama ndio mwenye dhamana na mamlaka?Punguza munkali...Sihusiki kwa lolote katika kutoa maamuzi.Hapa tunabadilishana tu mawazo
Munkali iko wapi? Mimi hapa najibu hoja ulizoleta wewe mtaalam wala sio za wenye dhamana na mamlaka. Ndio maana nimestuka uliponiambia kuweka taa za tahadhari ni ndoto.
Mimi sina uwezo wa kuwafikia wenye mamlaka ya kutoa maamuzi. Uwezo wangu unaishia humu humu tu.

Amandla..
 
Andiko la barafu linatoa mwanga mkubwa. Tunaposema bajeti ya uokoaji haitoshi siyo sahihi. Zoezi la mwisho la drill kuanguka ndege Bukoba limefanyika miezi kama 10 iliyopita. Tulioko Bukoba tuliambiwa ndege imeanguka majini ikitua. Waokoaji walipelekwa kutoa msaada.
Swali, je baada ya drill hawakugundua ikitokea kweli, Bukoba hamna wazamiaji wa kuokoa maisha ya watu majini? Waokoaji kama Majaliwa tutaendelea kuwapongeza. Hata kama Majaliwa hakufungua mlango wa ndege, lakini bila kupeleka mitumbwi, waliopona toka kwenye ndege wangezama majini. Boti za doria zinaangaika kukamata wavuvi wasiokidhi vigezo.
 
Ukiondoa mambo ya Categories na taratibu za ujumla za usafiri wa anga, mambo mengi aliyoandika mleta mada ni mambo ya kufikirika, maoni yake na siasa.

Kuhusu Majaliwa, mleta mada amerudi kulekule (kumzungumzia) kama watu wengine pia aliowakosoa kuwa wanapoteza muda kumzungumzia Majaliwa, hivyo mleta ameharibu mantiki ya hoja yake.
 
Munkali iko wapi? Mimi hapa najibu hoja ulizoleta wewe mtaalam wala sio za wenye dhamana na mamlaka. Ndio maana nimestuka uliponiambia kuweka taa za tahadhari ni ndoto.
Mimi sina uwezo wa kuwafikia wenye mamlaka ya kutoa maamuzi. Uwezo wangu unaishia humu humu tu.

Amandla..
Tofauti yako na barafu ipo katika hili! Yeye anaongelea hali halisi ilivyo on the ground na wewe unaongelea jinsi ilivyopaswa kuwa. Yaani recommendations baada ya tatizo.
 
Ukiondoa mambo ya Categories na taratibu za ujumla za usafiri wa anga, mambo mengi aliyoandika mleta mada ni mambo ya kufikirika, maoni yake na siasa.

Kuhusu Majaliwa, mleta mada amerudi kulekule (kumzungumzia) kama watu wengine pia aliowakosoa kuwa wanapoteza muda kumzungumzia Majaliwa, hivyo mleta ameharibu mantiki ya hoja yake.
Una wazimu si bure! Unaambiwa bila msaada wa kasia huo mlango usingefunguka! Hapo MAJALIWA siyo wa muhimu?
 
Kwa kuwa kiini cha ajali nzima kunagusia suala la uokozi, na Majaliwa kutajwa kama shujaa wa uokozi huku akivikwa sifa kedekede, hatuna namna ya kukwepa kumzumngumzia. Binafsi nitamkosoa kwa 100% mleta mada kwa kumtaja Majaliwa kama Shujaa wa kushukuriwa. Hoja kwa hoja.

1. Mlango wa ndege kufunguliwa.
Mlango wa ile ndege ya dharula hufunguka kutokea ndani, na wala hauhitaji msaada kutokea nje ili uweze kufunguka. Wahudumu na abiria waliookoka kwenye hiyo ajali wanathibitisha hilo na Demo video za ndege ya namna hiyo zipo mtandaoni na zinathibitisha hilo. Majaliwa hakuufungua ule mlango wa ndege.

2. Shughuli ya uokoaji wa maisha.
Manusura wote wa ajali wanasema, shughuli yote ya kupambania maisha yao ili kuweza kutoka ndani ya ndege ilifanywa na abiria wenyewe kwa kushirikiana na wahudumu wa ndege, wavuvi walifika muda mchache baadaye na kufanikiwa kuwahamisha kutoka kwenye bawa la ndege na kuwaingiza kwenye mitumbwi yao ili kuletwa pwani. Hakuna mahali popote manusura wa ile ajali wanamtaja Majaliwa kwa upekee.

3. Majaliwa anakosolewa kwa chuki binafsi?
Nani alikuwa anamjua Majaliwa kabla ya ajali hii, kwanini sasa maelezo yake yakikosolewa watu waseme ni chuki binafsi?

Kila abiria alihojiwa kwa muda wake, hakuna kikao rasmi cha abiria kilikaa kupanga namna ya kuongea, lakini maelezo yao yanakinzana na maneno ya Majaliwa aliyotueleza. Kwanini tusihoji maelezo ya Majaliwa?

Maelezo ya Majaliwa yamekosa mantiki na uhalisia, yanapotosha habari nzima. Kwanini tusiyakosoe na kuyapinga?
 
Back
Top Bottom