Ajali ya Ndege ya Precision Air imetuvua nguo wazi wazi

It's as if we are GOOD FOR NOTHING !!!
 
Polisi wa doria ziwa Victoria kazi yao ni nini sasa

Jwtz - Navy kazi yao ni nini sasa

Tanzania yangu ina safari ndefu sana haki tena [emoji174][emoji174][emoji706][emoji706]
Majeshi yetu ni ya kupita mbele ya rais na kumfanyia michezo ya kuigiza kama vile walivyokuwa porini wiki iliyopita. Ila katika uhalisia wa matukio, ni watupu.
 
Toka enzi za MV Bukoba hatujawahi kua na boti/meli ya uokoaji kweli? Labda hii kitu itabadilisha mtazamo wa umuhimu wakua nayo maana dah aise hapana. Mungu atupe busara kama nchi kuzingatia hivi vitu kabla hayajatokea.

Ingekuwa nchi ya wenzetu kuna kiongozi angejiuzulu kutokana na maafa ya aina hii.
 
Hakuna helicopter ya kunyenyua tani 20 Tanzania, Eastna Central Afrika

Hakuna tugboat ingesaidia kwenye kile kina kifupi.
Pia watu walikuwa washakufa tayari kabla hawajaokolewa, na hii ni kutokana na impact ya ndege kupiga maji
 
Kwa ufupi hamna wizara hata Moja yenye mikakati yakudumu na yenye kuendana na maisha ya Sasa tuliyonayo, mambo yanafanywa kwa matukio ya dharura ila hatuna mipango Wala njia yakutukomboa ni kitu chakushangaza watu wanaangalia matumbo yao tuu,swala la moto kule Kilimanjaro na hili la precision linanifanya kuishangaa hii nchi kwa siku hizi chache Bado umeme na maji ni mambo ya ajabu
 
Nashindwa kuelewa serikali inajali kweli maisha ya wananchi wake? ni mpaka afe nani ndio nchi hii itashtuka kuwa tunatakiwa kuwa tayari kukabili majanga badala ya kuripoti madhara? Inakera na inaumiza sana, narejea kukumbusha matukio makubwa ya yaliyochukua maisha ya watu wetu wengi, ni watu tu hawakuwajibika ipasavyo na kusababisha maisha ya watu kupotea.
 
Polisi wa doria ziwa Victoria kazi yao ni nini sasa

Jwtz - Navy kazi yao ni nini sasa

Tanzania yangu ina safari ndefu sana haki tena [emoji174][emoji174][emoji706][emoji706]
Navy wapo busy kgamboni uko wanasimamia LONGONI BEACH
 
Sasa yale mazoezi ambayo vyombo vya usalama hufanya kuonesha utayari wa kukabiliana na dharula yana maana gani ikiwa hayana msaada kwenye kukabili majanga ya ndani zikiwemo ajali?
Ili kumfurahisha mgeni rasmi, wageni na wananchi waliojitokeza. Ili kijiweni wanapopata kahawa, mihogo na chai wakasema Tz ina makomando wengi sana ipo vizuri ni ya 3 kwa ujasusi duniani.
 
Usitegemee jambo jipya toka kwenye serikali ya chama cha mapnduzi.Walipindua mambo mengi ndo maana vitu vingi viko kichwa chini miguu juu.Ni vile tu vichwa vyetu vizito kuelewa ila hawa watu walishashindwa toka kitambo.Ndo maana wanalamba asali tu sasa mambo mengine ya wananchi yatajiset yenyewe yatakavyojua.Ndo maana tumewekeza zaidi kwenye kupongezana na kusifiana badala ya kukosoana wakati kimsingi hakuna lolote kubwa tuliloliweza.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…