Ajali ya Ndege ya Precision Air imetuvua nguo wazi wazi

Kwa kuwa dogo majaliwa ameajiriwa acha akawafundishe watu Kaz na utu
 
View attachment 2408785
Wakuu kwa mara nyingine tena nitoe pole sana kwa waliopatwa na ajali ya Ndege leo huko Bukoba baada ndege ya Shirika la Precision Air kupata hitilafu wakati wa kutua na kuingia Victoria pia wale waliopoteza maisha basi Mwenyezi Mungu awarehemu na kuzipumzisha nafsi zao pema peponi.

Kusema ukweli nashindwa kuelewa ni jambo lipi sisi kama taifa tunaweza kujivunia kulifanya kwa ukamilifu, nakosa majibu jamani. Hivi uwezo wetu wa kukabili majanga uko kwa namna ipi? hakuna siku limetokea janga nchi hii vyombo byetu vikafanikiwa kudhibiti kwa 100%. Kila wakati lazima madhara makubwa yatokee.

Leo tumeshuhudia mambo ya ajabu sana kama nchi utadhani tuko miaka 40 huko, Ndege imekaa kwenye maji zaidi ya lisaa hakuna hata helicopter ya uokoaji au boti za kuvuta ndege za kisasa zilizofika eneo la tukio matokeo yake ndege inavutwa kwa kamba na wananchi, mambo ya ajabu kuwahi kutokea.

Nashindwa kuelewa serikali inajali kweli maisha ya wananchi wake? ni mpaka afe nani ndio nchi hii itashtuka kuwa tunatakiwa kuwa tayari kukabili majanga badala ya kuripoti madhara? Inakera na inaumiza sana, narejea kukumbusha matukio makubwa ya yaliyochukua maisha ya watu wetu wengi, ni watu tu hawakuwajibika ipasavyo na kusababisha maisha ya watu kupotea.

Hii nchi inahitaji mageuzi makubwa sana ya kimfumo, viongozi wetu hawajali maisha ya wananchi, wamekuwa wabinafsi na wasio wabunifu kukabiliana na matatizo.

Leo tumeonesha dunia ni kiasi gani hatuna uwezo wowote wa kujiokoa wenyewe, hatuna vifaa, hatuna wataalamu mpaka napata shida kuwaza ni kiasi gani hii nchi iko salama kiulinzi? mbona kama siku tukikumbwa na mafuriko ya mwezi mmoja watu wote tutaelea kwenye maji jamani?

Kilichoshuhudiwa kwenye tukio la uokoaji baada ya Ndege hiyo kuanguka Ziwa Victoria kimeacha maswali mengi kuliko majibu dhidi ya Serikali na Idara za Uokoaji

Miundombinu iliyotumika wakati wa uokoaji haikuwa sahihi akitolea mfano wa Ndege kuvutwa kwa kamba na wananchi, na idadi ndogo ya maafisa wakionekana wamesimama pembeni kama watazamaji

Sasa yale mazoezi ambayo vyombo vya usalama hufanya kuonesha utayari wa kukabiliana na dharula yana maana gani ikiwa hayana msaada kwenye kukabili majanga ya ndani zikiwemo ajali?

Hawa watu hawatujali jamani, hawana muda na sisi.
Mkuu inasikitisha sana mpka unajiuliza zile helicopter au huwa ni za kupepea mabango siku ya sherehe za uhuru au sherehe ya sensa.?.? Au zile fiber ziwa victoria ni za kukimbiza tu wavuvi kuwanyang’anya nyavu au vip..? Maana hii aibu kweli
 
View attachment 2408785
Wakuu kwa mara nyingine tena nitoe pole sana kwa waliopatwa na ajali ya Ndege leo huko Bukoba baada ndege ya Shirika la Precision Air kupata hitilafu wakati wa kutua na kuingia Victoria pia wale waliopoteza maisha basi Mwenyezi Mungu awarehemu na kuzipumzisha nafsi zao pema peponi.

Kusema ukweli nashindwa kuelewa ni jambo lipi sisi kama taifa tunaweza kujivunia kulifanya kwa ukamilifu, nakosa majibu jamani. Hivi uwezo wetu wa kukabili majanga uko kwa namna ipi? hakuna siku limetokea janga nchi hii vyombo byetu vikafanikiwa kudhibiti kwa 100%. Kila wakati lazima madhara makubwa yatokee.

Leo tumeshuhudia mambo ya ajabu sana kama nchi utadhani tuko miaka 40 huko, Ndege imekaa kwenye maji zaidi ya lisaa hakuna hata helicopter ya uokoaji au boti za kuvuta ndege za kisasa zilizofika eneo la tukio matokeo yake ndege inavutwa kwa kamba na wananchi, mambo ya ajabu kuwahi kutokea.

Nashindwa kuelewa serikali inajali kweli maisha ya wananchi wake? ni mpaka afe nani ndio nchi hii itashtuka kuwa tunatakiwa kuwa tayari kukabili majanga badala ya kuripoti madhara? Inakera na inaumiza sana, narejea kukumbusha matukio makubwa ya yaliyochukua maisha ya watu wetu wengi, ni watu tu hawakuwajibika ipasavyo na kusababisha maisha ya watu kupotea.

Hii nchi inahitaji mageuzi makubwa sana ya kimfumo, viongozi wetu hawajali maisha ya wananchi, wamekuwa wabinafsi na wasio wabunifu kukabiliana na matatizo.

Leo tumeonesha dunia ni kiasi gani hatuna uwezo wowote wa kujiokoa wenyewe, hatuna vifaa, hatuna wataalamu mpaka napata shida kuwaza ni kiasi gani hii nchi iko salama kiulinzi? mbona kama siku tukikumbwa na mafuriko ya mwezi mmoja watu wote tutaelea kwenye maji jamani?

Kilichoshuhudiwa kwenye tukio la uokoaji baada ya Ndege hiyo kuanguka Ziwa Victoria kimeacha maswali mengi kuliko majibu dhidi ya Serikali na Idara za Uokoaji

Miundombinu iliyotumika wakati wa uokoaji haikuwa sahihi akitolea mfano wa Ndege kuvutwa kwa kamba na wananchi, na idadi ndogo ya maafisa wakionekana wamesimama pembeni kama watazamaji

Sasa yale mazoezi ambayo vyombo vya usalama hufanya kuonesha utayari wa kukabiliana na dharula yana maana gani ikiwa hayana msaada kwenye kukabili majanga ya ndani zikiwemo ajali?

Hawa watu hawatujali jamani, hawana muda na sisi.
...Sielewi Kwa Nini SISI tunaendelea kuwajali na Kuwaimbia Pambio kuwa Waupiga Mwingi!! UPI??? [emoji35][emoji35][emoji35]
 
Wakati CCM wanaona hivi [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Screenshot_20221107-191649.jpg
 
Mimi hii habari niliipata kupitia BBC na baadaye jf.
TBC wapo kila mkoa lakini nadhani asubuhi walikua kwenye supu ya utumbo.
...Halafu yule Dr Wao Uchwara anakuja anatulaumu kuwa Kila Mtu kwenye Mitandao ya Kijamii anajifamya Mjuaji wa Mambo ya Ndege!
Pambaf!
Hasemi lolote kuhusu Ucheleweshaji wa Uokozi wa Serikali
Hasemi chochote habari za kwanza za Ajali hiyo tumazipata kutoka kituo Binafsi Cha Ayo na Mashirika ya Nje wakati TBC kituo Cha Taifa anachokiongoza siku nzima kinasubiri mwongozo kutoka Serikali kitangaze Nini!
 
Nashindwa kuelewa serikali inajali kweli maisha ya wananchi wake? ni mpaka afe nani ndio nchi hii itashtuka kuwa tunatakiwa kuwa tayari kukabili majanga badala ya kuripoti madhara? Inakera na inaumiza sana, narejea kukumbusha matukio makubwa ya yaliyochukua maisha ya watu wetu wengi, ni watu tu hawakuwajibika ipasavyo na kusababisha maisha ya watu kupotea.
...Ndugu yangu wee! Walikuwa Watu 800 tukisubiri Waokoaji kutoka Afrika ya KUSINI, na hatukujifunza Kitu!
Marehemu 19 TU tutajifunza Kitu????[emoji35]
Hii Nchi ni Uozo.
 
Kwa Tanzania hakuna sehemu ambayo pako safi.kila sehemu ukienda lazima utakuta madudu tu.
 
Hapo hatukuvuliwa nguo, mkuu. Nguo zenyewe tumezivaa, basi? Ajali hii imetumulika na kuonesha tuko uchi na tupu 100%!!!
 
Mengine ni makafara ya viongozi wa sirikali wandugu!
 
Back
Top Bottom