Ajali zinaondoshwa kwa kusali kwa kukaa barabarani? Waafrika bhana!

Ajali zinaondoshwa kwa kusali kwa kukaa barabarani? Waafrika bhana!

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2015
Posts
8,018
Reaction score
16,802
Viongozi wa dini mkoani Mbeya, kwa kushirikiana na serikali, wamefanya ibada maalum katika mteremko mkali wa Inyala, kuomba Mungu aepushe ajali ambazo zimekuwa zikitokea mara kwa mara katika eneo hilo na kusababisha maafa.

ITV

===

Acheni tu wazungu watudharau 24/7.
 
Hata Wazungu humtegemea Mungu pia labda kama haujasafiri kwenye Christian Countries, wakijenga Madaraja wanaweka sanamu ya Bikira Maria juu ya Daraja, Highways nyingi kwa Wazungu kwenye Christian countries zina mpaka chapel au Kanisa dogo la kusalia ukiwa njiani.

Labda kama haujaelewa Christianity, huwezi kumtenganisha Mungu na maisha yako ya kila siku kama wewe ni Christian, hivyo kama ni Wakristu hakuna shida yoyote kuombea barabara.

Shida kubwa, Wazungu hamuwaelewi ingawaje mnajifanya Wazungu!
 
itvtz

Tuna uninga mwingi sana.
 
Tuna ujinga mwingi sana, utamkuta mwingine hafanyi kazi yoyote, kutwa anashinda nyumbani kupiga umbea na kusikiliza nyumba za injili, huku anaamini ataletewa miujiza na Mungu ya kupata kazi.
 
1 Wakorintho 2
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹⁴ Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni.

¹⁵ Lakini mtu wa rohoni huyatambua yote, wala yeye hatambuliwi na mtu.

¹⁶ Maana, Ni nani aliyeifahamu nia ya Bwana, amwelimishe? Lakini sisi tunayo nia ya Kristo.
 
Viongozi wa dini mkoani Mbeya, kwa kushirikiana na serikali, wamefanya ibada maalum katika mteremko mkali wa Inyala, kuomba Mungu aepushe ajali ambazo zimekuwa zikitokea mara kwa mara katika eneo hilo na kusababisha maafa.

ITV

===

Acheni tu wazungu watudharau 24/7.
Achana na Inyala,Mbeya.
Mji mkuu wa kobiashara Dar es salam, watu wamekivuruga kiwanda cha nyama Tanganyika Packers, wakajenga kanisa kuubwa la Mwamposa ili waumini waombewe kupata kazi.
 
Hata Wazungu humtegemea Mungu pia labda kama haujasafiri kwenye Christian Countries, wakijenga Madaraja wanaweka sanamu ya Bikira Maria juu ya Daraja, Highways nyingi kwa Wazungu kwenye Christian countries zina mpaka chapel au Kanisa dogo la kusalia ukiwa njiani.

Labda kama haujaelewa Christianity, huwezi kumtenganisha Mungu na maisha yako ya kila siku kama wewe ni Christian, hivyo kama ni Wakristu hakuna shida yoyote kuombea barabara.

Shida kubwa, Wazungu hamuwaelewi ingawaje mnajifanya Wazungu!
Wazungu hawana huu UJUHA ( STUPIDITY ) tulionao / tuliyonao Waafrika ( hasa Waswahili ) wengi sawa?
 
Wazungu hawana huu UJUHA ( STUPIDITY ) tulionao Waafrika ( hasa Waswahili ) wengi sawa?

Ujuha gani unaouongelea? Ndiyo maana nikasema Wazungu hauwaelewi, kuna shida gani kwa Wakristo kusali? Unaweza ukashutumu mengine mengi lkn siyo kwa Wakristo kuomba, Sala ni sehemu ya maisha ya watu wa Dini, na ndiyo maana karibia nchi zote za Wazungu bendera zao zina alama ya Msalaba, unajua ni kwa nini?
Ni symbol of christianity!
 
Binafsi siwezi dharau ibada. Hakika ibada ina nguvu sana. Hata hivyo, Hayo maeneo hatarishi yanahitaji hatua za kisayansi zaidi kuliko za kiimani. Baadhi ya maeneo ambayo ni hatarishi sana suluhisho ni kujenga njia tofauti za kwenda na kurudi na zinaweza kutofautishwa hata kwa umbali wa mita 20 ili zisiingiliane kabisa hata gari ikifeli breki haileti madhara kwa wanaokuja opposite direction
 
Viongozi wa dini mkoani Mbeya, kwa kushirikiana na serikali, wamefanya ibada maalum katika mteremko mkali wa Inyala, kuomba Mungu aepushe ajali ambazo zimekuwa zikitokea mara kwa mara katika eneo hilo na kusababisha maafa.

ITV

===

Acheni tu wazungu watudharau 24/7.
Ungekuwa unaendesha gari mara kwa mara kwenda mikoani ungeeelewa ukweli wa kuwa sio kila ajali inatokana na uzembe.Kuna maeneo kabla hujaingia unamwaga chumvi na ukimaliza hicho kipande unamwaga chumvi vinginevyo hutoki salama. Ushajiuliza why is that? Ni kwa sababu kuna nguvu za kiroho zinazorun maeneo hayo na kwa mtu mwenye ufahamu mzuri hakuna njia bora zaidi ya kudeal na nguvu za kiroho kama ya kumshirikisha Mungu.
 
Viongozi wa dini mkoani Mbeya, kwa kushirikiana na serikali, wamefanya ibada maalum katika mteremko mkali wa Inyala, kuomba Mungu aepushe ajali ambazo zimekuwa zikitokea mara kwa mara katika eneo hilo na kusababisha maafa.

ITV

===

Acheni tu wazungu watudharau 24/7.
Vipi zile ibada za mteremko wa Mbalizi zilizaa matunda?
 
Kama ule mlima iwambi ajali zinatokea kila mwaka na serikali haifanyi chochote sasa wananchi wafanye nini zaidi kumwomba Mungu..?
 
Back
Top Bottom