Ajali ZNZ: Vodacom waanza kugomewa

Ajali ZNZ: Vodacom waanza kugomewa

Mkuu kunaweza kuwa na sababu nyingi tuu. Mojawapo Vodacom ni kampuni kubwa na maarufu sana Tanzania, so watu wanafikiri it should lead by examples. Nafikiri kati ya hao sponsors watano, Vodacom ilikuwa ndio kampuni kubwa. Sababu nyingine Vodacom imekuwa sana mstari wa mbele ku champion corporate social responsibility. Kwa sababu hii tuu yenyewe watu wengi wanadhani Vodacom ingekuwa mstari wa mbele kama walivyokuwa kwenye mabomu ya gongo la mboto. Kumbuka hii coporate social responsibility ni mojawapo ya sababu inayoifanya vodacom kulipa kodi ndogo zaidi ya Airtel japokuwa vodacom ina wateja wengi zaidi ya Airtel. Watu wanauliza where was vodacom corporate social responsibility kwenye hili janga?

Wapo wengine wanasema Vodacom haina wateja wengi Zanzibar ndio sababu waliamua kuendelea na Miss Tanzania. Sidhani hata vodacom wataikubali hii sababu b'se kibiashara haijakaa vizuri. Vipi kama janga lilikuwa limetokea Tanzania bara? Unafikiri haya mashandano yangeendelea? This event was not Miss Tanzania Mainland. It was Miss Tanzania. Kama alivyosema Mh Zitto hili janga lime test umoja na utu wetu. Kwa hili janga tumejua umoja, ushirikiano na utu wetu upo wapi.

Ku sponsor tuu Miss Tanzania itself ni corporate social responsibility. Pia kwa kampuni kusaidia watu watu waliokubwa na janga ni part ya corporate social responsibility. Na haya mambo yanapotokea kwa wakati mmoja inaweza kuwa ngumu ku make a right decision. But as a company, you will have to make a bold decision. Na katika maamuzi ya kampuni lazima itake into account its business interests presently and in future.

Lakini kama nilivyosema kwenye post yangu ya nyuma, this is problem rooted in our society. Kumbuka jana kulikuwa sio tuu na Miss Tanzania. Kulikuwa pia na ufunguzi wa kampeni za kisiasa huko Igunga. Kulikuwa pia na michezo ya mbalimbali. Tunachukulia issues very lightly. All go down kuwa kama serikali ingekuwa imetoa tamko tokea mapema haya yasingetokea. Hata hivyo vyombo vya habari hasa vya bara vimechangia sana haya kutokea. Nilishangaa Zanzibar disaster was trending worldwide on Twitter lakini kwenye vyombo vyetu vya habari vya ndani ilikuwa kama halikuwa janga kubwa.

Vyombo vyetu visingeweza kufanya lolote kwa kuwa haviko independent viko chini ya kwapa, kwa hiyo mpaka wapate ruksa ndipo watoe hiyo habari. labda ingekuwa enzi za Tido wangeweza kufanya hivyo lakini kwa sasa mpaka habari ipate baraka kutoka.....
 
Wewe kamanda unayeweka picha za Miss Tanzania ku-justify argument yako, unasahau kuwa kuna tukio la CCM ambalo lilikuwa aware na mkasa huu Zanzibar but viongozi wetu wa CCM hawakujali kitu?!

Mi nadhani kama ni kutoa lawama, basi tulaumu kwanza kampeni ya CCM na watu wanaohusika na nchi hii directly kabla ya mambo binafsi. Lakini sishangazwi kwani mapachoni pa wengine hili haliwezi kuonekana, kwani wanaohusika na jambo hilo ni "wenzetu"!!

attachment.php

attachment.php

Nafikiri jibu la swali lako linaweza kuthibitishwa na alivyojibu Kanigini hapo chini. CCM wanaweza nao kusema kuwa Pemba si NGOME yao ni ya CUF hivyo wao haiwahusu ndiyo maana wakaendelea na uzinduzi wa kampeni.
Acheni ushabiki wa kiwivu na kijinga, mbona hamzungumzii chama tawala kutoahirisha uzinduzi wa kampeni zao huko Igunga. Voda wako kwenye business, afterall that is not their target market as the area is dominated by Zantel subscribers.

Matukio haya yanaoneshwa kuwa Tanzania kuna Ombwe la uongozi kwa sasa. Ilitakiwa jana Ileile kutangaza kuanza maombolezo ya kitaifa na serikali kuagiza kusimamisha michezo na burudani zote kama walivyofanya alipofariki Mzee Nyerere. Vodacom wasingefanya shindano lile. Wa kulaumiwa hapa ni serikali ya Jamhuri kwa kuwaachia SMZ kabla ya wao kuzinduka na kutangaza maombolezo ya siku tatu. Suala la usalama ni suala la muungano. Ndiyo maana tunakata Katiba mpya iweke mambo wazi.
 
....Sidhani kwa kutokuwepo kwa tamko/taarifa rasmi ya serikali kuli justify Miss Tanzania kuendelea. Wrong plus wrong does not make it right. ...

You may be right, kwa sababu kama ni taarifa za kutokea kwa ajali zilikuwepo tangu asubuhi lakini nyingi ya taarifa hizo hazikuwa rasmi kuwezesha mtu kufanya maamuzi yoyote mazito (na hasa kama ulivyosema hakukuwepo na plan B). Nafikiria mtu anayesema shindalo hili linasimamishwa, atasema amepata wapi taarifa kama serikali/au chombo cha serikali hakijasema? Tuliona hapa juzi mtafaruku uliotokea kuhusu muandamo wa mwezi!

Hivi kwa mfano, kulikuwa na ugumu gani kwa serikali (Basata, etc) hiyo jana asubuhi/mchana kutangaza kusitisha shughuli zote za starehe/michezo? Ningetegemea wao kama serikali wangekuwa na taarifa za uhakika zaidi kwa wakati huo na hivyo kutoa tamko ambalo linakuwa basis ya mtu/kampuni kufanya maamuzi. Well, pengine ni kutokujali kwa watu maana I cant imagine huo ukumbi ulivyosheheni watu hiyo jana...na wote hawajali. Na hata vyombo vya habari vya serikali pia vimetuangusha sana na kwa kweli vinaendelea kutuangusha katika hili.
 
Tuache ushabiki wa kijinga,vodacom sio waandaaji wa miss tanzania wao ni wadhamini tu,waliotakiwa kufuta au kuhairisha tukio lile ni waandaaji ambao ni lino agent au serikali,zitto asitake umaarufu ktk hili,tena wadhamini walikuwa wengi kama redds,cfao-Dt dobbie why iwe vodacom tu?

Jamani... hakuna siku hakuna janga au msiba! Je ingekuwa kila janga/msiba tunasimamisha kila kitu ingekuwaje?
Kuna ndugu yangu alifiwa na baba yake mzazi na siku hiyo alikuwa mgeni rasmi kwa shughuli nyeti..walahi alienda kufungua na kisha kurudi nyumbani kuendelea na " msiba wake". Haiwezekani VODACOM walaumiwe kwa kutokuomboleza!
 
Nikuulize jirani yako akifiwa wewe utaweka magoma moto kusherehekea harusi au itaahirishwa kwanza kupisha msiba upite ndio wafanye harusi? Kawaida ya mila zetu waafrika ukisikia jirani amefiliwa unachukua kanga unaenda kwenye kilio au kibarakashia au shati jeusi. Hata sauti ya mziki kwako unapunguza au kuzima kabisa. For this one Vodacom deserve the blame for continuing sponsoring the show without showing any sense of remorse.

Vodacom kama sponsors they should advise akina Lundenga kuwa waiahirishe hadi hapo baadae (hata after three days au jumamosi ijayo) ili kupisha hili jambo lipite. Ila wakati ndugu zetu na majirani zetu zanzibar wanalia vilio vya msiba sisi tunaweka magoma moto na kufurahika na mtu anasimama katika jukwaa la miss na kuuliza ARE YOU ENJOYINGGG!!!! NA WATU WANA JIBU YEAH!!!!!

It is absolutely disgrace!!!!!
 
Naona extremism and radicalization is cropping fast fast within TZ, hivi miss TZ na Vodacom league si ajira za watu? na nani kikatiba ana mamlaka ya kusimamisha shughuli za kitaifa? Watu waache kumtafuta mchawi hawa wakina Jussa ni watu hatari sana katika ustawi wa jamii yetu! Mchawi ni serikali ya Zanzibar kupitia wizara ya usafirishaji! Huko ndipo malalamiko yaelekezwe...
<br />
POINT
 
Naona watu hawataki kabisa kuibebesha lawama serikali ya CCM pande zote; hawataki hata kusema kuwa CCM haikuahirisha kampeni yake licha ya taarifa toka asubuhi tena zikizinduliwa na Mkapa ambaye chini yake ajali ya Mv. Bukoba iilitokea na ambaye kwa miaka yake 10 madarakani hakufanya kitu (kumbuka ajali ilitokea mwaka wake wa kwanza wa kutawala).

Sasa watu wanakasirika na Ms. Tanzania. Labda ni kwa sababu ya hivyo vichupi na kuwa labda wanacyhukizwa na "maadili" lakini kwamba Vodacom wapate the blunt of our anger siyo sahihi hata kidogo. Ni kweli kabisa Vodacom walitakiwa wawe sensitive na tukio hili binafsi nilitarajia wangeweza kuahirisha tu for at least a week. Lakini si kwamba walilazimika kuahirisha.

Hasira yetu ielekezwe kwa serikali iliyoko madarakani kwa sababu 1001!

Mbona walikufa watoto 21 siku ya Id na RAis hata kutaja msiba huo kwenye hotuba ya kufunga mwaka na hakuna mtu aliyeuliza? HIvi mwaka huu peke yake ajali za barabarani Tanzania zimeua watu wangapi kwa sababu ya uzembe wa wasimamizi wetu wa sheria na sera mbovu za usafiri?

Hivi mnajua mwaka huu peke yake huko Bara wamekufa karibu watu 50 kwa kuzama kwa boti? Kuanzia wanafunzi wale 20 Sengerema, wengine 20 mtwara na wengine kule Rufiji na Mbinga? Au hawa hawakuwa watu wenye utu ule ule wa kutufanya tukasirike? Tena walikufa bila hata kusema kuwa kuna msiba wa aina fulani!

Labda kuna kitu I'm missing... hasira zetu ziwe dhidi ya tuliowachagua. Hivi kuna ugumu gani kusema kuwa "seriklai ya CCM bara na visiwani ziwajibike kwa hili na wananchi warudishe kadi zao kuonesha hasira yao!"?
 
Aliyesema majnga yakitokea kila kitu kinasimama?kuna watu jana wamefunga ndoa wakacelebratrete kama kawa..sasa mbona hilo amlizungumzii?Nawenyewe wangehairisha basi..

Mimi nilidhani wewe una uwezo wa kufikiri kumbe hapo ndiyo mwisho? Sisi hatuzungumzii harusi ya mtu binafsi tunazungumzia issues za kitaifa.
 
Hata mukitetea vipi akina Lundenga na wafadhili wake walikuwa insensitive kwa issue yote hii, kwani ile shughuli yao ilikuwa ni shughuli ya furaha.

Na nyinyi munaowatetea Vodacom kuwa hawana wateja huwa wanakwenda Unguja na Pemba kufanya promotion za nini?
 
Nikuulize jirani yako akifiwa wewe utaweka magoma moto kusherehekea harusi au itaahirishwa kwanza kupisha msiba upite ndio wafanye harusi?

Ndo maana nikaweka na mfano hai wa mtu aliyefiwa na baba yake mzazi! Jaribu kuweka context.Shindano halikufanyika ZNZ, lilifanyika bara. Pia kabla ya shindano ilitolewa fursa kuomboleza kwa kusimama kwa kipindi kukumbuka vifo vya waliozama kwenye MV Spices. Naelewa kiafrika tungependa sana kila kitu kisimame lakini tukumbuke kuna mambo mengi sana yangetokea ya kimikataba kama kila kitu kingesimamama.

nAKUBALIANA NAWE kuwa hakikuwa kipindi kizuri sana lakini ndio ilishatokea tusitafute mchawi wa kufa naye.Laumuni serikali kwa kushindwa kuzuia majanga yasiyo na ulazima.

Kawaida ya mila zetu waafrika ukisikia jirani amefiliwa unachukua kanga unaenda kwenye kilio au kibarakashia au shati jeusi. Hata sauti ya mziki kwako unapunguza au kuzima kabisa. For this one Vodacom deserve the blame for continuing sponsoring the show without showing any sense of remorse.

Lawama kwenda vodacom nakataa.Wangeachaje kuendelea na sponsorship? Showing remorse ?

Binafsi kama mimi kubaliaana na mtizamo wako kuomboleza lakini kibiashara nakukatalia!
 
Naona watu hawataki kabisa kuibebesha lawama serikali ya CCM pande zote; hawataki hata kusema kuwa CCM haikuahirisha kampeni yake licha ya taarifa toka asubuhi tena zikizinduliwa na Mkapa ambaye chini yake ajali ya Mv. Bukoba iilitokea na ambaye kwa miaka yake 10 madarakani hakufanya kitu (kumbuka ajali ilitokea mwaka wake wa kwanza wa kutawala).

Sasa watu wanakasirika na Ms. Tanzania. Labda ni kwa sababu ya hivyo vichupi na kuwa labda wanacyhukizwa na "maadili" lakini kwamba Vodacom wapate the blunt of our anger siyo sahihi hata kidogo. Ni kweli kabisa Vodacom walitakiwa wawe sensitive na tukio hili binafsi nilitarajia wangeweza kuahirisha tu for at least a week. Lakini si kwamba walilazimika kuahirisha.

Hasira yetu ielekezwe kwa serikali iliyoko madarakani kwa sababu 1001!

Mbona walikufa watoto 21 siku ya Id na RAis hata kutaja msiba huo kwenye hotuba ya kufunga mwaka na hakuna mtu aliyeuliza? HIvi mwaka huu peke yake ajali za barabarani Tanzania zimeua watu wangapi kwa sababu ya uzembe wa wasimamizi wetu wa sheria na sera mbovu za usafiri?

Hivi mnajua mwaka huu peke yake huko Bara wamekufa karibu watu 50 kwa kuzama kwa boti? Kuanzia wanafunzi wale 20 Sengerema, wengine 20 mtwara na wengine kule Rufiji na Mbinga? Au hawa hawakuwa watu wenye utu ule ule wa kutufanya tukasirike? Tena walikufa bila hata kusema kuwa kuna msiba wa aina fulani!

Labda kuna kitu I'm missing... hasira zetu ziwe dhidi ya tuliowachagua. Hivi kuna ugumu gani kusema kuwa "seriklai ya CCM bara na visiwani ziwajibike kwa hili na wananchi warudishe kadi zao kuonesha hasira yao!"?

Mkuu,

Kuilaumu serikali sikubaliani na wewe unless unipe sababu za kutosha nikubaliane na wewe. Hio ni kwasababu serikali imerespond to call of duty ilipotokea janga na tumejionea Rais ameahirisha safari yake na kwenda Zanzibar, Vile vile vikosi vya polisi wanamaji na hadi jeshi vimeenda kusaidia hiyo hali. Hivyo kuilaumu serikali ni kukosa shukrani.

Labda uibadilishe kauli yako useme hivi wa kulaumiwa ni watanzania na kukosekana kwa maadili ya uwajibikaji na rushwa iliyotapakaa. Hiyo ni kwasababu Tanzania sasa hivi rushwa imekuwa ni kauli mbiu na haiondoki. Kuanzia mfagizi mpaka mkurugenzi rushwa imekuwa ikinyima haki za watu, na kusababisha watu wapoteze maisha. Tuweni wakweli meli hii imekuwa ikifanya safari zake tangia 2007 na imeripotiwa iliwahi kukumbwa na mkasa kama wajuzi huko katika pwani ya Somalia ikaja kuokolewa na wamarekani na wafaransa. La kujiuliza imewezaje kufanya shughuli zake kuanzia 2007 hadi jana ilihali inajulikana hiyo meli mbovu. Ni akina nani walikuwa wakikagua hiyo meli kila baada ya miezi sita kuona ubora wake. Je vyombo vya mamlaka ya majini anga na barabara (Sumatra au sijui kama kuna chombo zanzibar) vilikuwa wapi siku zote.

Nani aliipasisha meli hii mbovu kufanya shughuli zake nchini, Waziri wa uchukuzi toka miaka ya nyuma ana taarifa zozote kuhusu hali ya usalama wa vyombo vya meli, ndege na mabasi? Kunafanyika independent audit inquiry kila mwaka kudhibitisha usalama wa watumiaji vyombo. Utagundua tatizo lipo katika mambo makuu mawili nayo ni uzembe na ufisadi. Matatizo haya ni endemic au kwajina lengine a systemic failure kiasi kwamba kuyaondoa lazima watanzania wabadilike ili yaondoke. Vyenginevyo kuilaumu serikali ni kama kuionea kwani tatizo tunalo watanzania wenyewe!!!
 
Mkuu,....Kuilaumu serikali sikubaliani na wewe unless unipe sababu za kutosha nikubaliane na wewe. Hio ni kwasababu serikali imerespond to call of duty ilipotokea janga na tumejionea Rais ameahirisha safari yake na kwenda Zanzibar, Vile vile vikosi vya polisi wanamaji na hadi jeshi vimeenda kusaidia hiyo hali. Hivyo kuilaumu serikali ni kukosa shukrani.

Mbona hapa chini unailamu serikali? Hoja kubwa hapa ni kuwa 'tunashughulika' zaidi na 'tiba'badala ya 'kinga'!

..... La kujiuliza imewezaje kufanya shughuli zake kuanzia 2007 hadi jana ilihali inajulikana hiyo meli mbovu. Ni akina nani walikuwa wakikagua hiyo meli kila baada ya miezi sita kuona ubora wake. Je vyombo vya mamlaka ya majini anga na barabara (Sumatra au sijui kama kuna chombo zanzibar) vilikuwa wapi siku zote.

Nani aliipasisha meli hii mbovu kufanya shughuli zake nchini, Waziri wa uchukuzi toka miaka ya nyuma ana taarifa zozote kuhusu hali ya usalama wa vyombo vya meli, ndege na mabasi? Kunafanyika independent audit inquiry kila mwaka kudhibitisha usalama wa watumiaji vyombo. Utagundua tatizo lipo katika mambo makuu mawili nayo ni uzembe na ufisadi. Matatizo haya ni endemic au kwajina lengine a systemic failure kiasi kwamba kuyaondoa lazima watanzania wabadilike ili yaondoke. Vyenginevyo kuilaumu serikali ni kama kuionea kwani tatizo tunalo watanzania wenyewe!!!
Nani wa kulaumiwa kwanza katika haya kama sio serikali ya/za CCM?
 
Acheni ushabiki wa kiwivu na kijinga, mbona hamzungumzii chama tawala kutoahirisha uzinduzi wa kampeni zao huko Igunga. Voda wako kwenye business, afterall that is not their target market as the area is dominated by Zantel subscribers.
<br />
<br />
usijaribu kuhalalisha kosa la voda kwa mwavuli wa ccm. hiki chama nacho kimekosea sana, sasa kiunganishe kwenye dhambi hii. kwa kuiadhibu voda naitupa line yangu ya voda, ndugu na jamaa msinitafute huko.
 
Ndo maana nikaweka na mfano hai wa mtu aliyefiwa na baba yake mzazi! Jaribu kuweka context.Shindano halikufanyika ZNZ, lilifanyika bara. Pia kabla ya shindano ilitolewa fursa kuomboleza kwa kusimama kwa kipindi kukumbuka vifo vya waliozama kwenye MV Spices. Naelewa kiafrika tungependa sana kila kitu kisimame lakini tukumbuke kuna mambo mengi sana yangetokea ya kimikataba kama kila kitu kingesimamama.

nAKUBALIANA NAWE kuwa hakikuwa kipindi kizuri sana lakini ndio ilishatokea tusitafute mchawi wa kufa naye.Laumuni serikali kwa kushindwa kuzuia majanga yasiyo na ulazima.

Lawama kwenda vodacom nakataa.Wangeachaje kuendelea na sponsorship? Showing remorse ?

Binafsi kama mimi kubaliaana na mtizamo wako kuomboleza lakini kibiashara nakukatalia!

Kibiashara they would have done a sensible thing kusogeza mbele Miss Tanzania.

Siamini na sikubaliani na kusema kuwa mikataba ingelikuwa tabu kubadilisha. Tuseme ajali ingelitokea Dar Miss Tanzania ingeliendelea? Jibu lake lingekuwa hapana. Katika mkataba wa kibiashara lazima kuna kipengele kinasema vp mkataba unakuwa wakati janga. Ndio maana hata ilipotokea janga la terrorism UK baadhi ya biashara zilisimama kwa muda. Pia hata New York waliposhambulia September 11 shughuli zilisimama kwa muda. Vodacom kama sponsor wangeliwashauri akina Lundega kama duty yao ya Corporate social responsibility kuwa kwakuwa nchi iko katika msiba basi si mbaya tukaahirisha shughuli mpaka next week.

Sikubaliani nawe kuwa hilo lingelikuwa ngumu na any additional costs of it would have been negotiated including wageni waliokuja for that event and etc.

Therefore Vodacom had showed no sense of remorse kuendelea kukubali show iendelee despite the fact walikuwa wakijua kuna janga limetokea. To me this is failure of Vodacom duty of being responsible to the society (corporate social responsibility) but wait tuko Africa no one cares ila ingelikuwa nchi za magharibi CEO wa Vodacom angelikuwa kazi hana mfano mzuri tu CEO wa BP marekani aliipata fresh ilipotokea kumwagika oil yeye akajibu jibu ovyo katika TV na baadae kwenda holiday kuendesha meli kilichotokea kila mtu anajua BP Marekani walimsack na kuleta CEO mpya.

Huo ndio uwajibikaji kwa jamii na sio unaenda kusmile mbele za watu wakati nchi iko kwenye msiba sikubaliani na wewe.
 
SO DO I!
 
Mbona hapa chini unailamu serikali? Hoja kubwa hapa ni kuwa 'tunashughulika' zaidi na 'tiba'badala ya 'kinga'!

Nani wa kulaumiwa kwanza katika haya kama sio serikali ya/za CCM?

Mkuu Serikali utailaumu vp wakati hii nchi siku hizi imekuwa ya kitu kidogo! Ukienda kila mahali jamaa wanaulizia kitu kidogo na rushwa imetapakaa kila mahali! To me this is systemic failure rather than a government failure. Lazima tuonyeshe kwanza sisi wenyewe tunabadilika ndio serikali itabadilika vyenginevyo mnatwanga maji kwenye kinu au kuifanya hii ajali suala la kisiasa. Hembu nieleze serikali inalaumika vp kujazana kwa abiria katika meli zaidi ya kipimo chake? Ukichunguza undani utakuja kukuta askari na wahusika wa bandari walimezea baada ya kupewa mlungula wakapandisha abiria kupita uwezo. Vile vile watoaji rushwa nao walitoa rushwa wakidhani wajanja kumbe wamepatikana na ajali imewaumiza, vile vile mmiliki wa meli bila shaka anajua kinachoendelea ila ndio hivyo tena pesa mbele mauti nyuma. This is systemic failure brother !!!!
 
Back
Top Bottom