KERO Ajira Bila Mkataba: Haki za Wafanyakazi wa Kampuni ya Temboking yupo gizani

KERO Ajira Bila Mkataba: Haki za Wafanyakazi wa Kampuni ya Temboking yupo gizani

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Kero yangu ni kuhusu ajira katika kampuni binafsi. Nimefanya kazi kwenye kampuni inayoitwa Temboking Limited, lakini sikuwa na mkataba wa ajira licha ya kukatwa makato ya NSSF kama kawaida. Hii inanifanya nisiwe na uhakika wa kazi, maana mwajiri anaweza kunisimamisha kazi muda wowote bila utaratibu.

Pia, kuna ukataji wa fedha usio wa haki—ukichelewa hata dakika mbili unakatwa kati ya shilingi 2,000 hadi 5,000, huku mshahara ukiwa ni takribani laki mbili tu. Zaidi ya hapo, tunafanya kazi ngumu bila kulipwa muda wa ziada (overtime), hata tunapochelewa kutoka kazini.

Hali hii inawaumiza wafanyakazi wengi, na tunaomba mamlaka husika zichukue hatua kulinda haki zetu.
 
TembokingLTD hawataki kujua kuhusu kimo Cha chini Cha mshahara.. Kwa maelezo yako
 
Back
Top Bottom