Watu wengi wanajiuliza kwa nini Idara ya Usalama wa Taifa TISS haitangazi kazi hadharani kama idara za nje?? Tatizo ni kitu gani?
Ukweli ni kuwa muundo na utendaji kazi wa idara za usalama wa Taifa duniani unachanganya sana (uko very complex), na haufanani kama A na A, au 1 na 1 kama watu wengi wanavyodhania. Utofauti huo unatokana na mambo mengi yanayozifinyanga idara hizo ikiwa pamoja na (but not limited to) muundo na asili ya Taifa husika, hali na mfumo wa kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiulinzi, changamoto zinazokabili nchi husika, msimamo wa kiongozi wa nchi (RAIS), na pia hali ya usalama ya ndani na nje ya nchi. Kwa sababu hiyo mfumo, muundo na hata utendaji kazi wa idara ya MOSSAD ya Israel unatofautiana (kwa namna fulani) na CIA ingawa wajomba hao ni marafiki sana, na pia idara ya Usalama ya Tanzania (TISS) inatofautiana vilivyo na idara za nchi jirani zetu. Kwa sababu hiyo utaratibu wa kuajiri watumishi wapya (majasusi) unaofanywa na TISS sio lazima ufanane na ule wa CIA, MOSSAD, au KGB kwa sababu zilizotajwa.
Vilevile ni lazima ieleweke kuwa nchi zilizoendelea zinazo vyombo vingi vya ujasusi vinavyofanya kazi kwa namna na mtindo mbalimbali na pia kwa kutumia vifuniko vingi(cover). kwa mfano Marekani wana National Security Agency (NSA), Central Intelligence Agence (CIA) na makachelo wa Federal Bureau of Investigation (FBI) ambao kwa asili kazi yao ilikuwa upelelezi wa ndani (kama ilivyo CID ya Tanzania) lakini kutokana na ongezeko la ugaidi duniani, mashujaa hao hivi sasa wanafanya kazi nyingi zakijasusi/upelelezi hata nje ya nchi kwa kushirikiana na idara nyingine. Mashirika haya yanapoajili watu huweza kutangaza waziwazi kwa sababu sheria za nchi zao zinawaruhusu kufanya hivyo.
Hata hivyo ni vema kutambua kuwa waajiliwa wote wanaopatikana kwa mkurulo (kwa matangazo) huishia kufanya kazi za wazi (overtly operations) na sio zile za ujasusi hasa (covertly operations) ambazo ndizo zenye msisimko zaidi. Hawa ndio wale wanaoweza kuwekwa mwenye maofisi ya wazi...mawizara, ikulu na au kufanya kazi za ufundi (technical) Hii ni kwa sababu watu wanaoandaliwa kuwa majajusi (spies) hutakiwa kufanyiwa upekuzi (vetting) wa kina na kwa muda mrefu ili kujua uwezo wao wa kimwili, kiakili, kisaikolojia na mambo mengine mengi yanayoweza kuwapunguzia sifa za kuwa jasusi. Maafisa hawa hata mafunzo yao hufanywa kwa siri na mara nyingine hata maafisa wengine wa idara za usalama hutakiwa wasiwaone au kuwajua ili kupunguza uwezekano wa kuwaumbua,
Kumbe basi, kama unataka kuwa JASUSI wa uhakika (kama Jack Bauer, au Jason Bourne) usihangaike kusubili matangazo ya uajili wa idara. Badala yake ishi maisha ya kujiheshimu na kujitunza sana, usijiingize kwenye scandal za kipumbavu, usijiingize kwenye malumbano ya vyama vya siasa (Naam hata chama tawala), na fanya mazoezi ya ku kujenga kimwili, kiakili na kisaikolojia....JAMAA watakuja kukufuata nyumbani kwako.
Godwin Chilewa
Mwandishi
Idara ya Usalama wa Taifa - Ni chombo cha mauaji?