A
Anonymous
Guest
Mimi ni Mtumishi wa Serikali sina siku nyingi kazini lakini tangu siku nimeripoti nimekuwa nikisumbuliwa na hawa watu wa mikopo, wamekuwa wakipiga simu na kutuma ujumbe wakiomba nikakope kwenye taasisi yao na wakati huo sijawahi kwenda kwenye ofisi zao hata mara moja.
Tunajua pengine biashara matangazo lakin wanapopiga simu na kutuma text kwa namba tofauti inakuwa kama ni kero maana kila ikitumwa meseji au kupiga simu anajitambulisha mtu tofauti kutoka kwenye taasisi ileile ya mikopo, hii inatukumba sana Watu ambao ni ajira mpya ambao hatujawahi kufika kwenye taasisi yao na hatukuwapa namba zetu wametolea wapi?
Mimi nipo Halmashauri ya Bukombe Mkoani Geita, kibaya zaidi wakipiga simu hawasemi wamepata wapi namba, na binafsi sijawahi kuomba mkopo huko hata mara moja, na tupo Ajira Moya wengi tunaopata kero kama hiyo.
Hawa watu ni kama wana-deal na ajira mpya kwa kuwa wakipiga simu wanakwambia kabisa kuwa “hata kama hujathibitishwa kazini sisi tunaweza kukukopesha”.
Ushauri wangu kwa hizi taasisi kama wanataka wateja na wanajua ni ajira mpya ni bora watembelee hizo taasisi physically na kushawishi watapata watu wenye utayari kuliko kupiga simu na meseji maana matapeli ni wengi kupitia taarifa za mitandao.