A
Anonymous
Guest
Ajira mpya katika Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko tunaomba kufikisha kilio chetu kuhusu utata uliojitokeza katika malipo ya fedha za kujikimu baada ya kuripoti kazini.
Tulipokuwa tunaripoti, tuliagizwa kuandika barua za kuomba fedha za kujikimu, maelekezo tuliyopewa, tuliambiwa kiwango cha fedha kingezingatia salary scale ya mtumishi. Kwa mfano, mimi ambaye nina Diploma nilielekezwa kuandika kiwango cha shilingi 130,000 kwa siku kwa muda wa siku saba, pamoja na gharama za usafiri kwa kuwasilisha tiketi za safari, jambo ambalo tulifanya kama tulivyoelekezwa.
Baada ya kuripoti kazini, tulikabidhi tiketi zetu na tukasubiri malipo. Hata hivyo, hivi karibuni tumeelezwa kuwa fedha hizo hazitalipwa kwa kuzingatia salary scale kama tulivyoelekezwa awali, bali zitalipwa kwa kuzingatia kituo cha kazi alichopangiwa mtumishi.
Hapo ndipo mkanganyiko ulipoanza. Kwa mfano, watumishi wawili wenye elimu ya Diploma, salary scale inayofanana na walioajiriwa na mwajiri mmoja, wanaweza kulipwa viwango tofauti kwa sababu mmoja amepangiwa Hospitali ya Wilaya na mwingine amepangiwa zahanati ndani ya halmashauri hiyo hiyo. Anayefanya kazi Hospitali ya Wilaya anaambiwa atalipwa shilingi 130,000 kwa siku, wakati aliyepangiwa zahanati atalipwa 80,000 kwa siku.
Kinachotushangaza ni kwamba kama utaratibu ulikuwa ni kulipa kwa kuzingatia kituo cha kazi, kwa nini tulielekezwa tangu mwanzo kuandika maombi kwa kuzingatia salary scale? Pia tunaelezwa kuwa mwongozo unaotumika ulianza kutekelezwa mwaka 2022, hivyo tunashindwa kuelewa kwa nini maelekezo ya awali yalikuwa tofauti na yanayotekelezwa sasa.
Tunachoomba si kingine bali ni ufafanuzi kutoka kwa mamlaka husika kuhusu utaratibu unaopaswa kufuatwa. Ikiwa mwongozo unasema fedha za kujikimu zilipwe kwa kuzingatia salary scale, basi tunaomba utekelezwe hivyo kwa watumishi wote ili kuwe na usawa. Kama kuna mabadiliko ya mwongozo, basi yaelezwe rasmi ili kuondoa sintofahamu na kuhakikisha haki inatendeka kwa watumishi wote wa ajira mpya.