Ajira ni utumwa, mshahara wa kila mwezi ni adui mkubwa wa ndoto za wengi

Ajira ni utumwa, mshahara wa kila mwezi ni adui mkubwa wa ndoto za wengi

Sio hivyo tu, ajira pia ni biashara. Unapiga hesabu gharama vs mshahara kinachobaki ni faida. Sasa kama ajira inakubakisha na M20 kwa mwaka na kuna mafao yanakusubiri, kwanini uchague kubaki na M5 ili uitwe mfanyabiashara? Si ukichaa huo?

Wafanyabiashara kuna saa hesabu zinagoma tunakuwa kama tumechanganyikiwa maana kuna muda unalipa kodi na mishahara wewe unabaki na sifuri na kuna rejesho la mkopo ulilokopa ili uendeshe hiyo biashara.

Unamuangalia mhasibu wako akiweka milioni yake mfukoni na ushampelekea 10% yake hifadhi za jamii ukijitazama wewe rejesho linakusubiri na hukupata kitu.
Kweli mkuu mimi nimeshaacha kazi mara kadhaa ili nifanye business, ila muda wote najikuta narudi ajirani 😆😆😆
 
Kipi kifanyike,nani atatuhudumia ikiwa Kila mtu atakuwa na mawazo kama haya,dunia inajiendesha yenye ili kujitosheleza,ndo maana hadi dunia kuisha binadamu hatakuwa na mtazamo wa aina Moja.
 
Kwa maneno matamu uliyonena ningekuwa nina ajira ningeandika barua ya kuacha kazi ili nikae mtaani kuendelea kuwacheka wenye kazi.
 
Ukiisha ajiriwa sahau kutajirika. Hakuna tajiri muajiriwa, matajiri wanaajiri
Inategemea umeajiriwa wapi mkuu. Kuna watu wanalipwa zaidi ya 5m kwa mwezi ambayo ni faida ya mfanyabiashara mwenye turnover ya zaidi ya 30m kwa mwezi. Yaani kama una duka la nguo uwe na mauzo yasiyopungua 1m kwa mwezi. Wafanyabiashara wachache wanaoweza kupata hiyo hela.

Sio kila mfanyabiashara anamzidi mwajiriwa. Na sio kila mfanyabiashara anaweza kuwa tajiri.
 
Kuna jamaa ali wahi kuwa mhasibu kiwanda cha sukari, oya ni fogo siku hizi
Ukiona mtu anasema ukiajiriwa hauwezi kuwa tajiri basi jua huyo hayupo wala haijui circle ya juu ya hela na hapo ni anajifariji tu baada ya kuzikosa ajira.

Ajira tena hizi za serikali mtu anaingia ofisini saa mbili anatoka saa tisa mchana sio kizuizi kabisa cha mtu kuwa tajiri. Ni vile tu wengi wana relax sana
 
Back
Top Bottom