Ajira Portal inahitaji mabadiliko, inakatisha ndoto za vijana wengi kwenye kuomba ajira

Ajira Portal inahitaji mabadiliko, inakatisha ndoto za vijana wengi kwenye kuomba ajira

shida inaleta hiv na ukianza kua apply unaambiwa uwez appy
Screenshot_20211104-202850.jpg
 
na ukiendelea kuongeza vyet vinaongezeka tu hakuna option ya delet
 
unakuwa over qualified, lakini kazi inayohitaji bachelor. hata ukiomba na una zote mbili diploma na bachelor inakubali tu
 
Ni kwa sababu ni over qualified, umepindukiza vigezo system imekuwa designed kwa kuchanganua vigezo husika kwa maana huwezi kuomba chini ya vigezo ulivyokuwa navyo inaangalia kigezo cha juu zaidi, kama vile huwezi kuomba nafasi ya kazi isiyoendana na elimu yako.

Alaf sidhan kama utaweza ku delete cheti chako uombe nafas ya diploma au chini yake, system pia inakataa hvyo, ukiwa cheti cha degree umeweka.
Logic yake ni nini hasa? Yaani mfano kuna nafasi ya mwalimu inatakiwa kufundisha sekondari sasa kuna watu wawili mwenye diploma na mwenye digrii kwa hiyo digrii anaachwa?? Kwa nini isiwe ni added advantage kumpata mwenye digrii kwa position ya diploma?? Aliye design huo mfumo ni kiazi kweli kweli.
 
Sina uhakika sana, mie ninavyojua kiserikali elimu ya mwisho ya ulazima ni degree ya kwanza, nyenginezo zinakuwa kama added advantage, na ndio maana vigezo vya mshahara wa serikal mwisho ni kwa degree, ukiachilia mbali kwa zile kazi zinazotaka specific requirements kama assistant lecture ambazo huanzia master's degree na lecture kwa Phd.

Kwa upande mwengine naona ni just kudhibiti idadi ya wanaomba kazi, imagine kama kazi za diploma alaf mtu wa degree wanaomba wao kipi watakachopata ijapokuwa inaaminika kuwa mwenye degree atakuwa vzur zaidi katika ufundishaji.
Hii nadhan ndio logic and yao, kishule shule ukiwa na elimu kubwa zaidi pamoja na matokeo mazur nadhan ndio inamata zaidi, tofaut na hizi kazi za pata sote.
 
Ku apply sio tatizo pamoja na kuitwa interview , shida kuipata kazi hiyo kama huna connection saa hv mtu utachina, wahitimu wamekuwa wengi kama kumbi kumbi, kipindi hicho nasoma nlikuwa siamini sana kitu connection, saa hv nimejionea mwenyewe mamaee 😂😂
 
System iko very systematic, kama wametangaza nafasi ni ya diploma wewe una degree ukaomba diploma inakutema automatically. Na kama unadiploma na degree kwa pamoja ukaomba Diploma kwa CV uliojaza unadegree system inakucheuwa... Yani wakitaka Diploma chomoa degree ombea Diploma, wakitaka Degree chomoa Diploma ombea Degree... kinyume na hapo tegemea kupata hilo bango...
 
Hii kero ya accounts za ajira portal nani anazitatua mbona kama imeundwa kutupa vikwazo tu lengo hasa ni lipi hasa maana hakuna mawasiliano nao mbona tunapelekana ovyo sana wadau
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
Ndio ukubwa huo.
 
Hii kero ya accounts za ajira portal nani anazitatua mbona kama imeundwa kutupa vikwazo tu lengo hasa ni lipi hasa maana hakuna mawasiliano nao mbona tunapelekana ovyo sana wadau
Mkuu kipi kimekusibu haswa...maana huenda changamoto uliuonayo suluhu yake ikapatkana hapa hapa kwenye kisima Cha maarifa...jf...maana mbona wengi wanatesa tu...
 
Back
Top Bottom