Ajira Portal inahitaji mabadiliko, inakatisha ndoto za vijana wengi kwenye kuomba ajira

Ajira Portal inahitaji mabadiliko, inakatisha ndoto za vijana wengi kwenye kuomba ajira

Kwema wa ndugu,

Binafsi nilikuwa naomba msaada kwa yeyote anayefahamu kujiunga maana mie nimefungua mwanzoni nimeweka email yangu na wakanitumia email ya kuactivate shida ilianza hapa kwenye kuactivate mara iandike failed to activate au nikijaribu na email nyingine inaambia activated na ukitaka kulog in ili uweze kuendelea na mambo mengine inanianikia incorrect sasa inakuaje hapo wataalam wanao fahamu
Ingia kwenye Gmail yako ndo utaka activate mkuu
 
Utumishi wasenge sana nimewapigia simu nawaelezea tatizo wananiambia niwasiliane na Ajiraportal yaani leo nimeshinda nawapigia simu Ajiraportal namba muda wote inatumika na kuna muda inaita bila kupokelewa na kuna muda haipatikani kabisa na ni muda wa kazi na mwendo ni huo huo kila siku.
Mimi nina wiki sasa kila siku napiga ajiraportal nakutana adha kama yako. Kuna siku napiga lisaa limoja mfululizo hadi simu inaisha chaji ila ni hayohayo.
 
Mimi nina wiki sasa kila siku napiga ajiraportal nakutana adha kama yako. Kuna siku napiga lisaa limoja mfululizo hadi simu inaisha chaji ila ni hayohayo.
Mkuu kwani unapatikana mkoa gani?
 
Mimi nina wiki sasa kila siku napiga ajiraportal nakutana adha kama yako. Kuna siku napiga lisaa limoja mfululizo hadi simu inaisha chaji ila ni hayohayo.
Endelea kupiga non stop hadi wapokee
 
Mkuu nadhani ni kwa yule ambaye alikuwa anafanya au anayefanya kazi sehemu fulani ndo anaambatanisha.

Maana kama ulivyoona pale pana working experience, kama ulifanya na kama unaendelea fanya.So kigezo hiki ndo kinapelelea kuambatanisha recommendation letter.

Taarifa zangu zimefika 92% kabla ya hii letter, sasa sijui zitatimia 100%? Na je ni lazima zifike 100?
70% na kuendelea unaweza fanya application na ikakubali.
 
Mkuu nadhani ni kwa yule ambaye alikuwa anafanya au anayefanya kazi sehemu fulani ndo anaambatanisha.

Maana kama ulivyoona pale pana working experience, kama ulifanya na kama unaendelea fanya.So kigezo hiki ndo kinapelelea kuambatanisha recommendation letter.

Taarifa zangu zimefika 92% kabla ya hii letter, sasa sijui zitatimia 100%? Na je ni lazima zifike 100?
Mm sjaweka recommendation letter iko 95%,na siweki kwakwel not necessary nishaona wngi wamepata kaz without izo recommendation letter, wamepass tu interview zote wakaitwa
 
Mm sjaweka recommendation letter iko 95%,na siweki kwakwel not necessary nishaona wngi wamepata kaz without izo recommendation letter, wamepass tu interview zote wakaitwa
Sawa mkuu,tunapeana maarifa na namna nzuri ya kufanya vzr.Me nipo nahangaika kujaza vyeti,sema nilijaza but kumbe vinatakiwa vilivyokuwa certified. Sasa kutoa hivi imekuwa ngumu ili niweke certified.
 
Sawa mkuu,tunapeana maarifa na namna nzuri ya kufanya vzr.Me nipo nahangaika kujaza vyeti,sema nilijaza but kumbe vinatakiwa vilivyokuwa certified. Sasa kutoa hivi imekuwa ngumu ili niweke certified.
Ongezea Tu vilivyo certified vikikataa kutoka..maana apo unatakiwa uedit uwek vilivyo certified so vikikataa wka na vilivyo certified hakuna shida ata vikijirudia mara 2
 
Ongezea Tu vilivyo certified vikikataa kutoka..maana apo unatakiwa uedit uwek vilivyo certified so vikikataa wka na vilivyo certified hakuna shida ata vikijirudia mara 2
Sawa mkuu ngoja nipambane.
 
Punguza hasira, kuhusu suala la kusign in hilo unawaonea labda kwenye suala la equivalent qualifications kutokuzingatiwa.
Mtalam.. unapozungumzia equivalent qualifications inamaana levels na sio course. Advance diploma ni equivalent to Bachelor... Ila ukisoma imeandikwa 'related' inamaana masomo yanayoendana na sio levels.
 
Hivi kweli hiki chombo mhimu ya Ajira nchini kina Wabobezi wa IT?

Yaani Website yao Iko hovyo sana linapo kuja suala la ku apply. Website, appearance ina vutia kwa nje. Ila sasa ingia ndani ktk ku chakata taarifa, ni website ya hovyo!!

Inawezeka kabisa kutokana na poor design ya Website hii, vijana wengi wenye sifa wakawa wana kosa ajira kisa kuondolewa na mfumo mbovu automatically. Mfumo utamwambia hana sifa, haja timiza vigezo, nk ili hali vigezo vyote anavyo. Baadhi ya matatizo nili kumbana nayo leo.

Mfano 1. Nafasi za LGTI -Assistant Lecturers Accounting & Finance. Eti Qualifiaction ni Master's Degree in Law? Law na Accounting uka ona dunia gani?

Hawa jamaa wanaweza kuwa wana fanya makosa haya kwa makusudi ili watu washindwe ku apply na wachukue watu wao kimya kimya au part time wa chuo. Kwa kosa hili, kila ata kae omba hiyo kazi. System ita mjibu hana Sifa!!

Mfano 2. Post ime andikwa applicant Must be a holder of Master degree in Finance. Mtu mwenye Bachelor degree in Accounting & Finance na Master of Business Admninistration (Specialization : FINANCE) ila website yao ina mkataa eti hana vigezo. Hii ina onesha ni jinsi gani website yao ilivyo karirishwa!!

Mfano no 3. Ku search Key words ya Kazi haikubali. Ila inakubali tu key word ya Taasisi ina maana kama taasisi ina kazi 200 upitie page zote kuperuzi kazi 1 baada ya nyingine, kwa sababu heading za kazi ziko hidden. Ku apply ambako kunge tumia dk 30. Una tumia siku 1 hadi 2.

Mfano 4. Kuna tatizo la Backward. Mfano ume click Vacancies page 32. U click kusoma moja wapo ya kazi ktk page 32.e.g. row 1. Uki rudi nyuma kidogo ili uende row 2, kosa!!! Ina kutoa moja kwa moja toka page 32 hadi page 1 ya Vacancies(yaani home page ya Vacancies).

Kwani hawawezi kuandika openly Taasisi...then row 1 kazi namba 1 jina la kazi namba 1. Then, Row 2 kazi namba 2 jina lake...nk. ili mtu aende direct. Yaani wame fanya ku apply kazi nako kume kuwa kama kutafta kazi!! Unnecessary disturbances.

Mfano 5. Issue ya GPA. Una kuta kazi inataka 3.5 au 3.8 ila ww una 4.0. masters wana taka GPA ya 3.8 au 4.0 ila ww una zaidi ya hizo. Vyuo vingi vya nje Master's au PhD hawana mambo ya GPA ni Distinction, Credit au Pass (au A, B+, B-, C na Pass). Designer wa hii website na maboresho yake ina onesha yupo local sana. Hiyo ni kazi ya Recruitment committee siyo Website. Vyuo vinajua 3.5 to 3.9 ni equivalent na upper second class, nk.
Kwanza hiyo system nime ona haina huwezo wa kusoma GPA ktk vyeti. Hii kazi ifanywe na selection team.

Mfano 6. Kazi ya Tutor II Financial Management-(ADEM). Requirements ni B. Education in Commerce, or Bachelor of Arts in related fields. Pia uwe na masters in related fields. Mtu una B. Arts in Business (Accounting &Finance) na MBA ( Finance) na ufaulu wote wa GPA unao. Mfumo una kwambia huna vigezo. Duuh. Hii portal ime kuwa designed na mtu local sana. Ili paswa Key words za Programme/Course ndio itumike ku screen. Sasa wao uta kuta wame limit Education!

Tuna omba kama kuna technical problems mseme na mu extend application deadline na mrudishe kwenye default settings , Au kama na ninyi mmerecruit watu wasio na sifa ya kazi zao, nanyie mtangaze kazi zenu tuziombe upya. Deadline za kazi zinafika. Ila ku appy kuwezekani.
 
msaada ajira portal kila kitu nimejaza vizuri ila score haipandi,haifiki 70% na namba za msaada hakuna inayopatikana..naomba mwenye wazo tafadhari.
 
Mkuu umeeleza vizuri sana, yaan wameilipua tu na wala hawana mpango wa kuiboresha.

Mfano ni hiyo point yako namba 2, sijui wanashindwa ku link vipi sifa za ziada muombaji anazokuwa nazo.

Mfano mtu ana shahada ya uhasibu, na stashahada ya uzamili katika ya utawala wa lakin anakataliwa kwenye nafasi inayomtaka mtu mwenye sifa ya shahada ya utawala wa biashara.
 
Back
Top Bottom