mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 13,897
- 18,477
Kumekuwa na upendeleo wa dhahiri katika ajira za ualimu kwa siku za hivi karibuni. Utakuta imetangazwa ajira ya waalimu wa hesabu na fizikia lakini majina yakitoka unakuta wa Biology wamo!
Utakuta imetangazwa waalimu wanaotakiwa ni wale waliomaliza masomo mwisho 2017, lakini unakuta waliomaliza hadi 2018 wamo!! Sasa hayo ni makosa ya upendeleo ya dhahiri na yakilalamikiwa wakubwa wanakosa mahali pa kuficha nyuso zao!! Unakuta jina moja limetoka zaidi ya m,ara moja, hapo ujue nafasi imetunzwa kinyemela ya mtu fulani
Sasa imebuniwa njia rahisi ya kupendelea ambayo mtu hatalazimika kuficha uso wake!! Kwanza huwezi kuweka sheria ya mchezo wakati wa mchezo ukiwa umeshafika.
Ilipaswa itangazwe mapema baada tu ya ajira zilizopita kuwa safari ijayo tutatumia kigezo cha kujitolea kama sharti mojawapo la kupata ajira ya ualimu.
Inawezekana walioandaliwa kupendelewa walipewa siri hii mapema na wakatafuta hizo nafasi za kujitolea ili tu waje wawe na sifa ya ziada kuliko wenzao. Lakini pia hapa utafunguka mlango mkubwa wa rushwa. Watu watapata barua za kujitolea wakati siyo.
Ushauri wangu: Kigezo hiki cha kujitolea KISITUMIKE awamu hii maana wengi walikuwa hawakijui. Ila kama itaonekana ni cha muhimu, basi itangazwe SASA kuwa safari IJAYO zikitokea nafasi za ualimu, kigezo hicho kitatumika.
Halafu uwekwe utaratibu wa wazi na Tamisemi wa kuomba hizo nafasi za kujitolea kama nafasi za ajira zinavyoombwa na majina yatoke kwa wazi na shule walizopangiwa kujitolea ziwe wazi. Hii itapunguza rushwa na udanganyifu.
Utaratibu mzuri wa kugawa ajira utumike ule ule uliokuwa unatumika. Aliyehitimu kwanza anafikiriwa kwanza. Haiingii akilini mtu aliyehitimu 2019 akapata ajira na mtu aliyehitimu mapema zaidi kama 2017 au 2018 akakosa kwa masomo yale yale.
Rais wetu tunakuomba ulifuatilie hilo maana hao uliowapa dhamana wamekuja na vigezo ambavyo wengine waliandaliwa navyo kwa siri!