Ajira za Walimu: Kigezo cha kujitolea ni kichaka cha rushwa, upendeleo na udanganyifu. Rais Samia kimulike

Ajira za Walimu: Kigezo cha kujitolea ni kichaka cha rushwa, upendeleo na udanganyifu. Rais Samia kimulike

Nilishacomment kwenye post fulani hii ishu, hivi serikali inafikiri wahitimu wote wakiamua kujitolea hizo shule zitatosha?

Hiki ni kichaka cha rushwa full stop!
Kwasababu mwisho wa siku hata kujitolea kutakua ni dili (mpaka uhonge ndio upate na huku unafanya kazi bure).

Kujitolea kisiwe kigezo, serikali iache kupenda mtelezo kuwafanyisha watu kazi bila ujira.

Kama wahitimu ni wengi wawafanyishe interview basi. Mwenye uwezo ashinde.

Narudia tena, kujitolea ni rushwa. Na TAKUKURU walitakiwa wawe walishanusa hili mapema ila wapo wapo tu.
 
Mtu ajitolee alafu kigezo kitolewe acha Tamaa boss
 
Yale yale! Kwani wakati huyo Jiwe akiwa Rais, huyo Samia alikuwa wapi? Na unadhani chanzo cha haya yote ni hayo majituu, au ni Hayati?...
Mtu haajiri eti kwa sababu Familia yake masikini... hata hivyo ni vema waliojitolea wakazingatiwa
 
K
Mtu haajiri eti kwa sababu Familia yake masikini... hata hivyo ni vema waliojitolea wakazingatiwa
Kujitolea hakujawahi kutangazwa awali kuwa ni kigezo cha kuajiriwa ualimu!! Wakitaka watangaze hivyo sasa kwa ajira za huko mbeleni maana wote watakuwa wanafahamu kigezo hicho. Kwa sasa utumike utaratibu wa siku zote wa kutoa kipaumbele aliyehitimu mapema.
 
Nilishacomment kwenye post fulani hii ishu, hivi serikali inafikiri wahitimu wote wakiamua kujitolea hizo shule zitatosha?...
Dah! Mzee naye ametuachia Legacy ya aina gani hii sasa!! Enzi zile watu walikua wanaamua wakaripoti, au wapotezee! Leo hii wahitimu wanataka kutoana ngeu!!

Aisee pambaneni tu mpaka kieleweke. Hakuna namna sasa.
 
Kujitolea Ni Added advantage.

Sehem yoyote IPO hii kitu,
Tena private sector ndo imetamalaki sana.

Unaenda Kwenye interview watu 500, Nafas 30. Ila tayar Kuna watu 60 wanajitolea pale Miaka zaidi ya mitano.

Izi mbinu za kupunguza ushindani maana watu 85,000 kwa elfu6 Lazima uchambuz wa kina ufanyike.

Vigezo vikiisha,
Lazima tu watafuta na walisahau kuweka nukta baada ya Aya Kwenye barua za maombi.
Au walioattach vyeti vya la Saba.

Sasa ukichujwa usije lalamika kwanini awajasema na vyeti vya lasaba tuweke wkt ulitakiwa ujikamilishe mweyewe.
 
Kwa suala la kuchuja waombaji 130,000 kujaza nafasi elfu 6 Lina ugumu kiasi chake.

Lazima TU utafute namna ya kupunguza watu kwa Lazima.

Ata Kama ni wewe mwajili,
Lazima ungetoa TU kipaumbele kwa waliojitolea Kwanza.

mtoa mada jalibu kuvaa viatu vya Mwajili, Ungekua wewe ungefanyaje
 
Kumekuwa na upendeleo wa dhahiri katika ajira za ualimu kwa siku za hivi karibuni. Utakuta imetangazwa ajira ya waalimu wa hesabu na fizikia lakini majina yakitoka unakuta wa Biology wamo...
Wakuu wa shule wamewabeba ndgu Zhao wingine wamewatengenezea had I mahudhurio,waonekane walikuwa wanajitolea Kumbe hakuna.
 
Katika pitapita zangu naambiwa ajira za hivi karibuni zilizotangazwa rushwa inayotembea ndani kwa ndani sio za dunia hii
 
Kwa suala la kuchuja waombaji 130,000 kujaza nafasi elfu 6 Lina ugumu kiasi chake.

Lazima TU utafute namna ya kupunguza watu kwa Lazima.

Ata Kama ni wewe mwajili,
Lazima ungetoa TU kipaumbele kwa waliojitolea Kwanza.

mtoa mada jalibu kuvaa viatu vya Mwajili, Ungekua wewe ungefanyaje
Mkuu, kwa mfumo wetu wa elimu inajulikana kuwa mwenye matokeo ya juu akishindanishwa na mwenye matoke ya chini basi mwenye matokeo ya juu anashinda.

Sasa hili suala unaajiri mtu ana gpa ya 2.1 kisa tu amejitolea kwa kuunganishwa na baba ake mdogo wakati unamuacha mwenye gpa ya 4.4 eti kisa tu hakujitolea hili sio sawa.

Mazingira ya nchi yetu bado hayajawa fair kiasi hicho kuajiri kwa kuangalia kigezo cha kwanza kiwe kujitolea. Ni rushwa tu hapa itatamalaki.

Anza kuchuja kwa gpa, fuata matokeo ya form 6 fuata matokeo ya form 4. Na kama bado basi waite oral interview umalize kabisa utata.

Halafu pia hili la kujitolea litadumaza mno mno elimu yetu. Vijana watakuwa hawasomi vyuoni, anajua akitoka na gpa yake ya 2.1 ataenda kuunganishwa na mjomba kujitolea halafu ataajiriwa.

Siungi mkono suala la kujitolea liwe kigezo cha kuajiri hawa vijana.
 
Iyo sehemu ya kuweka cheti cha lasaba uliitengeneza wewe kwenye system au unafikiri kuna lisehemu tu kubwa unaweka chochote
 
Nyie munaoleta GPA hii sio Private sector vipi nyie
 
K

Kujitolea hakujawahi kutangazwa awali kuwa ni kigezo cha kuajiriwa ualimu!! Wakitaka watangaze hivyo sasa kwa ajira za huko mbeleni maana wote watakuwa wanafahamu kigezo hicho. Kwa sasa utumike utaratibu wa siku zote wa kutoa kipaumbele aliyehitimu mapema.
Sasa huoni kwamba waliojitolea kipindi hawakuombwa ni wazalendo kukuzidi wewe unaesubiri uitwe...
 
Mungu ampe JK maisha marefu, enzi zake anatoa ajira 40000 Kwa mpigo Hakuna kugombania.

Hizo Barua za kujitolea zinauzwa na Wakuu wa shule hela yako tu
 
Back
Top Bottom