...Ndugu yangu, ninadhani tunauzoefu tofauti juu ya mambo haya. Nina kuhakikisha Kuna machinga anafanya kazi yake hiyo, na anapata hela ya Mtaji wake, hela ya chakula, hela ya usafiri, hela ya huduma nyingine kwa familia yake na anaweka akiba.
Pia yupo mmachinga wa aina uliyoeleza. Bahati mbaya sana Kuna na wale unaoitwa wameajiriwa serikalini ama Kampuni binafsi Wana kipato cha "hand to mouth". Unapata mshahara kwa mwezi unamkopo benki/ vikoba utakao uumaliza wakati ajira yako itakapo koma, na bado unagongea TIMiZa, songesha, salary advance...bado unajitapa kuwa huna kazi ya " Mkono kinywani"!?
Tusidanganye Watanzania wenzetu na walimwengu kwa ujumla. Tusema ukweli kama tunataka kuvuka kwa pamoja lakini kama Nia ni kushamirisha ubepari kandamizi tuendelee na uongo.