Ajiua kwa kujitumbukiza kisimani baada ya kuua mke, mtoto kisa mgogoro wa michepuko

John Haramba

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2022
Posts
365
Reaction score
1,374
Mwanaume aliyejulikana kwa jina la Madirisha Kanyalu (60) amejiua kwa kujitumbukiza kwenye kisima baada ya kumuua mtoto wake Meshack Madirisha (miezi 11) pamoja na mkewe aitwaye Evodia Nyerere (27) kwa kutumia kitu chenye makali akimtuhumu mkewe kuchepuka na wanaume wengine.

Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, ACP Joseph Paul tukio hilo limetokea Februari 2, 2022 majira ya saa 12 asubuhi katika maeneo ya Kitongoji cha Mwamadulu, Kijiji cha Bulambila, Kata ya Mwalukwa, Wilaya ya Shinyanga.

“Evodia Nyerere (27) na mtoto wake aitwaye Meshack Madirisha mwenye umri wa miezi 11 wakazi wa kitongoji cha cha Mwamadulu, Kijiji cha Bulambila, Kata ya Mwalukwa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga waliuawa kwa kukatwa na kitu chenye makali sehemu ya shingoni na Madirisha Kanyalu (60) ambaye ni mume wa marehemu wakiwa ndani ya nyumba wanayoishi,” amesema Kaimu Kamanda Paul na kuendelea:

“Mtuhumiwa Madirisha Kanyalu alitoroka baada ya tukio na kwenda kujitumbukiza kwenye kisima cha maji kilichopo karibu na nyumba yake aliyokuwa anaishi na kufariki dunia.”

Amesema chanzo cha tukio hilo ni mgogoro wa kifamilia ambapo Madirisha Kanyalu alikuwa anamtuhumu mke wake kuwa na mahusiano ya wanaume wengine.

“Natoa wito kwa wanandoa/wenza wapeleke malalamiko yao mapema kwenye madawati ya jinsia na watoto yaliyopo vituo vya polisi pamoja ustawi wa jamii ili kupata suluhisho la migogoro yao,” amesema.

Source: Malunde
 
Mtoto amekosa nini hapo jamani
 
Kama Kawa ni kutoka Kanda ya wasiojielewa.

Screenshot_20220304-112737.png
 
Mzee naona aliamua kuanza kusolve Calculus akiwa na miaka 60.

Mtu wa umri wa miaka 60 maana yake amezaliwa 1962 ( Mwaka mmoja baada ya Uhuru wa Tanganyika). Hu

Anao mwanamke mwenye umri wa miaka 27 maana yake amezaliwa mwaka 1995 ( Yaani huyu amekuta tumeshaanza mfumo wa vyama vingi) .

Kuna tatizo katika jamii zetu, hawa mabinti wanahitaji huduma za kimwili na kihisia.

Poleni kwa msiba wana familia.
 
No comment
 
Mwanaume aliyejulikana kwa jina la Madirisha Kanyalu (60) amejiua kwa kujitumbukiza kwenye kisima baada ya kumuua mtoto wake Meshack Madirisha (miezi 11) pamoja na mkewe aitwaye Evodia Nyerere (27) kwa kutumia kitu chenye makali akimtuhumu mkewe kuchepuka na wanaume wengine.

Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, ACP Joseph Paul tukio hilo limetokea Februari 2, 2022 majira ya saa 12 asubuhi katika maeneo ya Kitongoji cha Mwamadulu, Kijiji cha Bulambila, Kata ya Mwalukwa, Wilaya ya Shinyanga.

“Evodia Nyerere (27) na mtoto wake aitwaye Meshack Madirisha mwenye umri wa miezi 11 wakazi wa kitongoji cha cha Mwamadulu, Kijiji cha Bulambila, Kata ya Mwalukwa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga waliuawa kwa kukatwa na kitu chenye makali sehemu ya shingoni na Madirisha Kanyalu (60) ambaye ni mume wa marehemu wakiwa ndani ya nyumba wanayoishi,” amesema Kaimu Kamanda Paul na kuendelea:

“Mtuhumiwa Madirisha Kanyalu alitoroka baada ya tukio na kwenda kujitumbukiza kwenye kisima cha maji kilichopo karibu na nyumba yake aliyokuwa anaishi na kufariki dunia.”

Amesema chanzo cha tukio hilo ni mgogoro wa kifamilia ambapo Madirisha Kanyalu alikuwa anamtuhumu mke wake kuwa na mahusiano ya wanaume wengine.

“Natoa wito kwa wanandoa/wenza wapeleke malalamiko yao mapema kwenye madawati ya jinsia na watoto yaliyopo vituo vya polisi pamoja ustawi wa jamii ili kupata suluhisho la migogoro yao,” amesema.

Source: Malunde
Huyu jamaa lazima alikuwa kada wa CCM.
Wanawake acheni tamaa, zee la miaka 60 litakutosheleza vipi hamu zako za kingono binti wa miaka 27?
 
Hapa angekuwa mwanaume ni mzungu yangemwagwa matusi na kejeli za kufa mtu kwa age gap hii. Lakini nashangaa comment za kistaarabu kwenye watu 2 weusi. 🤔
 
Mzee kachelewa kuoa..alikuwa anakusanya ng'ombe wa mahari..sasa kaoa mnaanza kumlaumu na kumuibia kabisa..

Kaona Bora ahamie upande wa pili huko na familia yake labda ataishi kwa amani!
 
Mzee kaona isiwe tabu

Hawa dada zetu hawa[emoji16][emoji16][emoji119][emoji119]
 
Daah mapenzi!mapenzi!mapenzi ogopa hii kitu unaeza kucomment hapa unalaumu kesho tukasikia umeua kisa wivu wa mapenzi tusaliii.
 
Back
Top Bottom