Ajiua kwa kujitumbukiza kisimani baada ya kuua mke, mtoto kisa mgogoro wa michepuko

Ajiua kwa kujitumbukiza kisimani baada ya kuua mke, mtoto kisa mgogoro wa michepuko

Huyo mtoto anaitwa Meshack Madirisha na ana miaka 11.. maana yake alimuoa huyo mwanamke akiwa na miaka 16 , wakati huo yeye akiwa na miaka 49...

Na usikute hana ela , na show za Putin haziwezi..
 
Huyo mtoto anaitwa Meshack Madirisha na ana miaka 11.. maana yake alimuoa huyo mwanamke akiwa na miaka 16 , wakati huo yeye akiwa na miaka 49...

Na usikute hana ela , na show za Putin haziwezi..
Masafwa mtoto ana miezi 11 sio miaka 11.
Ila msafwa93 kila nikikuona hua nalikumbuka lile jukwaa letu pendwa.
Inabidi tuanzishe kampeni ya kurudishwa lile jukwaa letu kwa kweli.
Maxence Melo #bring back jukwaa letu.
Mama amesharudisha uhuru wa vyombo vya habari jamani.
 
Mwanaume aliyejulikana kwa jina la Madirisha Kanyalu (60) amejiua kwa kujitumbukiza kwenye kisima baada ya kumuua mtoto wake Meshack Madirisha (miezi 11) pamoja na mkewe aitwaye Evodia Nyerere (27) kwa kutumia kitu chenye makali akimtuhumu mkewe kuchepuka na wanaume wengine.

Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, ACP Joseph Paul tukio hilo limetokea Februari 2, 2022 majira ya saa 12 asubuhi katika maeneo ya Kitongoji cha Mwamadulu, Kijiji cha Bulambila, Kata ya Mwalukwa, Wilaya ya Shinyanga.

“Evodia Nyerere (27) na mtoto wake aitwaye Meshack Madirisha mwenye umri wa miezi 11 wakazi wa kitongoji cha cha Mwamadulu, Kijiji cha Bulambila, Kata ya Mwalukwa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga waliuawa kwa kukatwa na kitu chenye makali sehemu ya shingoni na Madirisha Kanyalu (60) ambaye ni mume wa marehemu wakiwa ndani ya nyumba wanayoishi,” amesema Kaimu Kamanda Paul na kuendelea:

“Mtuhumiwa Madirisha Kanyalu alitoroka baada ya tukio na kwenda kujitumbukiza kwenye kisima cha maji kilichopo karibu na nyumba yake aliyokuwa anaishi na kufariki dunia.”

Amesema chanzo cha tukio hilo ni mgogoro wa kifamilia ambapo Madirisha Kanyalu alikuwa anamtuhumu mke wake kuwa na mahusiano ya wanaume wengine.

“Natoa wito kwa wanandoa/wenza wapeleke malalamiko yao mapema kwenye madawati ya jinsia na watoto yaliyopo vituo vya polisi pamoja ustawi wa jamii ili kupata suluhisho la migogoro yao,” amesema.


Source: Malunde
60 years unaoa 27 years lazima wamle wewe ushachoka yeye ndo kwanza ana nguvu ya kutosha
 
Back
Top Bottom