Akamatwa kwa kujenga mahandaki sita bila kibali Mwanza

TheCrocodile

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2021
Posts
1,864
Reaction score
5,254
Jeshi la Polisi mkoani Mwanza linamshikilia Evance Ndeka Bisesagu (47), mfanyabiashara na mkazi wa Bupumula wilayani Ilemela kwa tuhuma za kuchimba mahandaki sita bila kufuata taratibu za kisheria.

Mtuhumiwa huyo amekamatwa Aprili 22, 2026 kufuatia taarifa za wananchi kuhusu uwepo wa mahandaki hayo yanayohatarisha usalama wa wakazi wa maeneo ya jirani huku uchunguzi wa awali ukionesha kuwa ujenzi wa mahandaki haukufuata utaratibu wa sheria za ujenzi ikiwemo kutolewa kwa taarifa kwa mamlaka husika na kupata vibali Vya ujenzi husika.

Mbali na Bisesagu ambaye ni mmiliki wa eneo hilo pia Polisi inawashikilia watu wengine wawili Ngasa Kasuka na Hamad Juma Kashinje waliokuwa vibarua wa ujenzi sambamba na kuendelea na msako wa mafundi na watu wengine waliokuwa wakishirikiana nao katika ujenzi na uchimbaji wa mahandaki hayo.
 

Attachments

  • FB_IMG_1776974616842.jpg
    32.3 KB · Views: 24
  • FB_IMG_1776974621526.jpg
    66.1 KB · Views: 20
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…