Akifanya mzungu inaitwa 'Teknolojia', akifanya Mwafrika inaitwa 'Uchawi', kwanini inakuwa hivi lakini?

Akifanya mzungu inaitwa 'Teknolojia', akifanya Mwafrika inaitwa 'Uchawi', kwanini inakuwa hivi lakini?

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2013
Posts
38,920
Reaction score
44,970
Binafsi naamini 'Uchawi' ni teknolojia usiyoijua. Teknolojia yeyote kama huielewi ni 'Uchawi'.

Fikiria enzi za Yesu uende na smartphone uanze kupiga watu picha au uanze kupiga video call , hapo hapo utadakwa na kuchomwa moto na Kanisa kwa shutuma za uchawi.

Ni kama wale waliosema Dunia haipo katikati, au Dunia sio 'Flat'; kanisa liliwafanya kitu mbaya sana.
 
Kwahiyo hirizi pumuzi ni teknolojia..? Muache kupanda ndege mpande ungo Tena uchi mseme ni teknolojia!

Wenzenu wanaweka var nyie mnawasha moto kiwanjani eti mlikuwa mnasikia baridi..😂
Wewe umewahi kuona mtu akiruka na ungo, una ushahidi gani?, hivyo vingine ni tricks tu, ila kwakuwa huijui ndio unaita "uchawi', hiyo trick usiyoijua ndio technique/technology yenyewe
 
Kwani hujawahi sikia mambo ya kimila yanayofanyika na kweli mvua inanyesha? hiyo ni teknolojia tusiyoijua, na ni uchawi pia..
ndo ubaya unapoanzia hapo, nimesikia ila nataka nione, bila kuona hatuwezi kuamini
 
wafanye maombi na nione mvua ikinyesha, sio stori za vijieweni
Ni mara ngapi maombi yanafanyiaka na misikitini na makanisani na wote tunaona na mvua kweli inanyesha? wewe hukuona?
 
msimu wa mvua ukifika mvua itanyesha, hiyo ni jografia
Wewe unajua ni Jiographia, hivyo utaita teknolojia, upo sahihi. Ni kama ROBERT HERIEL alivyotabiri kuanza kwa mvua na joto kali kipindi cha equinox, kesho yake kweli mvua zilianza, kwa watu ambao wangekuwa hawajui hii teknolojia kwao ingeweza kuwa ni kama ‘uchawi’, ila kwakuwa wote tumesoma jiografia, tunaita ni ‘teknolojia’, kwa sababu tunajua how the sun, moon work kuleta athari za hali ya hewa, ila ‘teknolojia / ujuzi’ kama huujui/ huna, basi utamuita ROBERT HERIEL mchawi.

Nakazia, ‘uchawi’ ni ‘teknolojia’ usiyoijua.
 
Back
Top Bottom