Basi labda tuko tofauti sana mkuu.
Mimi binafsi wivu ninao lakini napingana sana na wanaosema wanaweza kuuwa kisa mkee.
Huwenda tumeumbwa tofautiii,mke hawezi kuniuma kiasi nimtoe uhai.
Kama yeye ndo furaha yangu,nikimuua nitaipata wapi furaha?
Kama nakubali kwamba yeye ni furaha yangu basi vipi nimuue?
Kama sio furaha yangu sasa huo wivu unatoka wapi?
Au ni kukomoa na kulipa kisasi?
Hakuna mantiki juu ya hilo,ni roho ya kipuuzi na kikatili tu ambayo mtu imemjaa kutokana eidha na mazingira alozaliwa au namna alivyojikuza...
Alafu kuhusu mahari ya kuolea labda nikudokeze jambo moja kwambaa.... Haina maaana ya kwamba kutoa mahari kubwa ndo unampenda sana mwanamke,na wala haina maana kutoa mahari ndogo haumpendi mwanamke.
Kama ni hivyo basi jua kwamba uliyemuoa kwa mahari kubwa hakupendi kwa nini ujuee ? Kwa sababu kama anakupenda mahari kubwa ya nini ?
Kakupenda wewe ama kazipenda pesa zako ?
Hivyo kama umeoa kwa mahari kubwa basi tafsiri yake(kwa mujibu wa kauli yako)ni kuwa huyo mke hakupendi na kama hakupendi kwa nini asichepuke kutafuta anaowapenda?
Kwa sababu si ndo tunasema mwanamke anayekupenda wewe hajali pesa zako wala hakuombi ombi pesa,sasa iweje mwanamke anayekupenda atake mahari nyingi ?
Basi kwa huo msemo wako jua kwamba akitaka mahari kubwa hakupendi na hapo zinduka wewe sasa uone kwamba kama anataka mahari kubwa =hanipendi.na kama hanipendi basi nikimuoa atachepuka kuwatafuta anaowapenda.
Ebu kuwa siriaz mkuu haya mambo siriaz usiingize mzaha kabisaa
Huyo asisingizie wivu kabisa.
Sikukatalii kwamba hujaoa ila inawezekana umeoa kiwepesi sana say mahari 50,000 na gharama za ndoa 150,000 hapo mke hawezi kukuuma.
Ila kama umeoa kwa mbinde tena kwa kuhustle miaka kadhaa ili uoe... Ndugu yangu mke anauma kuliko msiba. Mtu anafiwa halii lakini kusalitiwa analia kwa kuomboleza jamaa yangu