Hii biashara ni kweli pasua kichwa lkn ina uwakika wa kuingiza hela mara tu gar ikiingia road
Nimeifanya kwahiyo naijua vizur sana,kikubwa uwe na dereva mzuri,fundi mzuri hapo biashara utaiweza
Dereva mzuri ataepusha ajali zinazo tokana na uzembe wa kipumbavu na kutunza chombo chako,siku moja nilipanda daladala jinsi lilivyokuwa linaendeshwa yaani uchungu nilipata mimi na lau kungekuwa na namba za mmiliki ningemwambia huyu dereva hafai kabisa
Uwe na dereva ambaye anaweza.kukomaa mwenyewe kwa mda mrefu,hawa deiwaka wanaharibu sana gari kwakuwa ni deiwaka hawajali,ila dereva ambaye anajua haya ndio maisha yake atakitunza chombo
Fundi mzuri naye ni jambo muhimu sana,ila ukiwa na fundi kanjanja ujue utakwama,gari kila siku ikiwa inarudi gereji ujue hapo utakwama,walau ikikomaa kwa siku tano kwa wiki hela utaiona
Ukifanikiwa hapo hakika hela utaiona sana tu,zingatia service kwa wakati,kwa kawaida kila baada ya wiki mbili